Engine oil gani ni nzuri kwa Gari aina ya IST?

Engine oil gani ni nzuri kwa Gari aina ya IST?

Tofauti ya Hz oil ni viscosity,na inategemea unaishi ukanda gani ukiachilia sababu nyinginezo,kwa nchi za baridi 5w 20 ni nzuri ila kwa nchi yenye joto Kali above 30 Celsius it's better to use yenye viscosity kubwa like 20W 50 Kwa high mileage,ingawa ukitumia 20W 50 fuel consumption inaongezeka kwenye gari.Kingine ni kwamba Technology inabadilika everyday nw and then,hvyo haya makampuni ya kutengeneza oil yanabadilisha oil products based on circumstances ingawa gari linabaki kuwa lile lile for hundred years to come,ndiyo maana hata gari iliyokuwa recommended kutuma petrol Leo zinatumia gas systems tofauti,mf DIT na VETA wanachofanya.
Pia usitumie 20W kwenye low mileage cars na newest cars,inaweza pelekea damage kwenye engine.Kwa kuongezea ni kwamba engine components nyingi za high mileage cars Huwa zinakuwa zimechoka na hivyo kupelekea leaks,lakini kutokana na 20W oil kuwa nzito hupunguza chance ya leakage at high temperatures.Its a tricky topic in fact my friend.
 
Naomba kuuliza kidogo, ikiwa gar ina km laki 2 zen nikabadili injin na kuweka nyingine, bado maswala ya kilometa kwenye matumiz ya oil yana husika tenaaa
Pia usitumie 20W kwenye low mileage cars na newest cars,inaweza pelekea damage kwenye engine.Kwa kuongezea ni kwamba engine components nyingi za high mileage cars Huwa zinakuwa zimechoka na hivyo kupelekea leaks,lakini kutokana na 20W oil kuwa nzito hupunguza chance ya leakage at high temperatures.Its a tricky topic in fact my friend.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi namba kila moja ina tafsiri yake...
Unapokuta mfano 5W 30...
Namba ya kwanza kabla ya W inawakilisha uzito wa oil. Kadri namba inavyozidi kuwa ndogo, ndivyo oil inavyozidi kuwa thin hivyo kuwezesha better performance at the cold start...

W simply inawakilisha winter wengine wanasema Weight wengine wanasema Watt...lakini inawakilisha Winter..

30 inawakilisha viscosity ( ile hali ya oil kuwa kama ina nata nata fulani hivi.)
Hii ina maana kwamba injini inpopata joto lake la juu ambalo linatakiwa ili ifanye kazi vizuri, viscosity ya oil hii bado itabaki katika kipimo hicho cha 30 ambacho kimewekwa na watengenezaji, hali kadhalika kwa oil namba 40 au 50

Kwa mantic hii oil 5w 30 ni nyepesi kuliko 10w 30..

Oil hizi zenye namba mbili yaani 5w 30 kwa lugha nyingine zinaitwa multi grade oils....ni oil ambayo imetengenezwa kufanya kazi katika mazingira ya baridi sana na joto sana...

Lakini hizi SAE 40 za kawaida ni mono garde....hizi ni maalumu kwa mazingira ya joto tu...na ndiyo maana kwa siai tulioko huku Arusha ikifika lile baridi la mwezi wa saba, kama gari ni ndogo na umeweka SAE 40, ukiliwasha asubuhi utasikia injini inavuma sana kwa muda mrefu...injini ikishafikia joto kiasi fulani ndiyo unaona inatulia...wakati unasubiri injini ipate moto, unakuwa unasaga vyuma..

Ukifuatilia zamani nchi zenye baridi kama huko Ulaya, walikuwa na oil za aina mbili..nzito kwa ajili ya msimj wa joto na nyepesi kwa ajili ya msimu wa baridi....watu walilazimika kumwaga oil msimu wa bari na kuweka oil nyepesi ya kukabiliana na baridi...hali kadhalika msimu wa joto, walimwaga oil nyepesi na kuweka nzito...

Kuepuka purikushani hizo, ndiyo Society of Automobiles Engineers (SAE) wakaja na oil ambayo ni mult grade mfano 5w30, 10w 30,10w40 n.k....oil hii ukishaiweka haichagui baridi wala joto wewe ni kuangalia tu muda wa service ukifika unaimwaga.

Hatari ya SAE 40 kwa garo dogo, haijalishi unaishi Dar au Arusha.... ukiwasha gari asubuhi wakati injini imepoa, oil hii kitaalam huchelewa kufika sehemu za juu za injini kutokana na uzito wake...pale inapichelewa, vyuma vinaendelea kusagana na unaendelea kuua injini yako taratibu...

SAE 40 ukitumia kwa magari makuu kuu sana haina shida...mfano madaladala au gari ambalo mileage imeenda juu sana pengine zaidi ya 180000km..
Safi sana mkuu kwa maelezo yako.

Naipenda Jf kwa mambo kama haya!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ndo unampotosha kwenye utumiaji wa oil na ndo unataka kufanya mwamba aue engine yake mapema mtu anatakiwa kutumia recommended oil kulingana na watengenezaji walivyo shauri na sio dhana ya km kama ambavyo mwamba anashauri watu

Sent using Jamii Forums mobile app
Fact! Kinachotakiwa ni recommended oil by manufacturer na sio vinginevyo. Masuala yakuambiaana abadili kwa ajili ya mileage sio kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Whether you choose high mileage 20W-50 or conventional 20W-50 motor oil, they will both flow like a 20 Weight oil in cold weather, then with the viscosity of a 50 Weight oil once the engine is up to full temperature. Choose Castrol[emoji2400] GTX[emoji2400] 20W-50 to protect against sludge and Castrol[emoji2400] GTX[emoji2400] High Mileage for older vehicles with over 75,000 miles on the odometer.

Castrol[emoji2400] GTX[emoji2400] High Mileage 20W-50 is specially formulated for vehicles with over 75,000 miles. It contains Phosphorus Replacement Technology, which reduces the level of phosphorus and replaces it with a proprietary additive that preserves your emission system while maintaining robust wear protection. Castrol[emoji2400] GTX[emoji2400] 20W-50 is formulated to clean away existing sludge while preventing new sludge formation to help extend engine life. It is also liquid engineered to resist viscosity and thermal breakdown".
Mkuu kwa post yako hii Nimegundua wewe kuna kitu hujakielewa. Hata 5w30 grade high mileage zipo. Kwa kifupi kila grade inayo high mileage yake bro. Kwa mimi nashauri atumie oil recommended by manufacturer na iwe made special for high mileage cars. Kwa IST nadhani castrol edge high mileage 5w30 itamfaa. Castrol wanazo kwa kila grade ya oil.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwa post yako hii Nimegundua wewe kuna kitu hujakielewa. Hata 5w30 high mileage zipo. Kwa kifupi kila grade inayo high mileage yake bro. Kwa mimi nashauri atumie oil recommended by manufacturer na iwe made special fir high mileage cars. Catrol wanazo kwa kila grade ya oil

Sent using Jamii Forums mobile app
Na isitoshe most of modern engines recommend SAE viscosity ni 5w 30...hii ndiyo imepewa kipaumbele kwa makampuni mengi yanayozalisha magari bila kujalisha mileage...

Tatizo watanzania sisi ni wavivu wa kusoma..kuna watu gari zao zimebahatika kuja na user manual lakini hawazisomi....online kuna resources nyingi tu, watu tujenge utamaduni wa kusoma.

Fact! Mimi pia nilisoma manual ya gari yangu nikakuta ni 5w30 isipokuwa maeneo yenye joto zaidi ya 40 ndio unaweza weka 10w30, ila conclusion yao wakasema recommended oil grade ni 5w30. Watu wasome manual za magari yao, weingie hata online, wasiwe wavivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu tumia oil kulingana na recommendations ya watengenezaji na oil nzuri kwa gari ambayo haijafikisha km 180000 unashauriwa kutumia 5w30 au umekoswa sana tumia 10w30 basi na kuhusu kampuni hata Toyota wao wana oli zao zilizotengenezwa kwa ajili ya magari yao unaweza kuzipata madukani mfano wa hilo duka ni JO GENUINE SPARE PARTS AND ACCESSORIES lipo kinondoni vijana barabara ya mwananyamala karibu na meridian hotel fika hapo utashauriwa oil nzuri ila angalizo oil hizo zinakuaga na bei ya juu sana kuliko oil nyingine ile pia kuhusu synthetic na mineral ni aina mbili za oil tofauti na zimetengenezwa kwa material tofauti pia na kuhusu 15w40 Mara nyingi oil hii ni nzito hivyo inashauriwa itumiwe na magari yanayotumia diesel
Fact.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elimu ya bure..
Kwa gari lako na kwa mazingira ya Tanzania tumia 5w 30,
Ukikosa nenda 10w 30.....
.Anayekuambia hizi oil ni za nchi za baridi amekariri bila kusoma...

Iko hivi..
5w 30 ina uwezo wa kuhimili baridi kali kuanzia -30°C bila kupoteza viscosity yake...pia oil hii ina uwezo wa kuhimili kiwango cha juu cha joto ambacho ni +40 °C bila kupoteza viscosity yake..
Hiki kiwango cha joto nilichotaja ni joto la mazingira unayoishi (outside temperature)

10w 30 ina iwezo wa kufanya vizuri kuanzia joto la -20°C mpaka joto la +40°C...

Hii ina maana kwamba oil 5w30 na 10w 30 zina uwezo wa kusambaa haraka sehemu za injini hata kama gari limewashwa kwenye mazingira ya baridi sana kibongo bongo tunasema Arusha, Iringa, Mbeya na maeneo mengine yenye baridi.
Pia inahimili joto kali kama la Dar, Zanzibar nk.

Kwa hiyo hizi oil zinamudu mazingira yote na ndiyo maana car manufacturers wa siku hizi wana recommend oil hizi zaidi siyo Nissan, Toyota,Honda, Subaru,Mazda n.k...

Ukinunua nunua full synthetic ukikosa ndiyo ununue hizi mineral oil ambazo usivushe 3000 km.

Synthetic unaweza ukaenda km 5000 na zaidi kama umefunga oil filler genuine ndiyo ufanye service nyingine..

Full synthetic inahimili dhoruba ngumu kama milima, matope, joto, baridi, racing bila kupoyeza viscosity yake....na bei yake imesimamia kucha.

Agalia fundi wa mwembeni asikushauri uweke SAE 40 ya kawaida...hii oil ni nzito sana na utakuwa unalitesa gari bila wewe kujua...

Oil ndiyo DAMU ya engine.....zingatia if you love your car.
Umekamilisha elimu. Comments mbili za juu zimetoa elimu kamilifu including hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
umejaribu ila ungegoogle kuhusu hizi grade za oil ungeelewa zaidi tena google forums za magari katika nchi za joto mfano uarabuni huko Saudia, Dubai, Qatar uone wao wanatumia oil za grade gani zingatia kwamba huko wana joto zaidi yetu sisi na ni all year around wao ni joto tu na napenda kukwambia wao wanafuata recommendation za manual books zinavyosema most of them kama sio wote wanatumia 5w30 kwenye gari za petrol na sio 20w50 hata japan kwenyewe summer kuna joto kama la huku na bado wanatumia the same 5w30 ila kwenye winter ndo wanatumia 5w20 au 0w20 hii mimi nimefuatilia sana na nikagundua watz wanapenda 20w50 sababu ni cheaper tu na sio zaidi ila kwa gari kama IST yenye 1NZ au 2NZ kuweka 20w50 ni kuua engine taratibu bila kujua.
Tofauti ya Hz oil ni viscosity,na inategemea unaishi ukanda gani ukiachilia sababu nyinginezo,kwa nchi za baridi 5w 20 ni nzuri ila kwa nchi yenye joto Kali above 30 Celsius it's better to use yenye viscosity kubwa like 20W 50 Kwa high mileage,ingawa ukitumia 20W 50 fuel consumption inaongezeka kwenye gari.Kingine ni kwamba Technology inabadilika everyday nw and then,hvyo haya makampuni ya kutengeneza oil yanabadilisha oil products based on circumstances ingawa gari linabaki kuwa lile lile for hundred years to come,ndiyo maana hata gari iliyokuwa recommended kutuma petrol Leo zinatumia gas systems tofauti,mf DIT na VETA wanachofanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
umejaribu ila ungegoogle kuhusu hizi grade za oil ungeelewa zaidi tena google forums za magari katika nchi za joto mfano uarabuni huko Saudia, Dubai, Qatar uone wao wanatumia oil za grade gani zingatia kwamba huko wana joto zaidi yetu sisi na ni all year around wao ni joto tu na napenda kukwambia wao wanafuata recommendation za manual books zinavyosema most of them kama sio wote wanatumia 5w30 kwenye gari za petrol na sio 20w50 hata japan kwenyewe summer kuna joto kama la huku na bado wanatumia the same 5w30 ila kwenye winter ndo wanatumia 5w20 au 0w20 hii mimi nimefuatilia sana na nikagundua watz wanapenda 20w50 sababu ni cheaper tu na sio zaidi ila kwa gari kama IST yenye 1NZ au 2NZ kuweka 20w50 ni kuua engine taratibu bila kujua.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabisa mkuu ahsante kwa ufafanuzi huu wanapenda hizo sababu ya urahisi wa bei tu na pia watz wengi tumetawaliwa na kupenda vitu rahisi rahisi sana na ambacho vitatupa madhara makubwa huko mbeleni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu tumia oil kulingana na recommendations ya watengenezaji na oil nzuri kwa gari ambayo haijafikisha km 180000 unashauriwa kutumia 5w30 au umekoswa sana tumia 10w30 basi na kuhusu kampuni hata Toyota wao wana oli zao zilizotengenezwa kwa ajili ya magari yao unaweza kuzipata madukani mfano wa hilo duka ni JO GENUINE SPARE PARTS AND ACCESSORIES lipo kinondoni vijana barabara ya mwananyamala karibu na meridian hotel fika hapo utashauriwa oil nzuri ila angalizo oil hizo zinakuaga na bei ya juu sana kuliko oil nyingine ile pia kuhusu synthetic na mineral ni aina mbili za oil tofauti na zimetengenezwa kwa material tofauti pia na kuhusu 15w40 Mara nyingi oil hii ni nzito hivyo inashauriwa itumiwe na magari yanayotumia diesel
Ningekuwa dar ningefika kununua oil ya toyota. Maelezo yako yapo sahihi mkuu, umemshauri kwa usahihi kabisa mkuu
 
Elimu ya bure..
Kwa gari lako na kwa mazingira ya Tanzania tumia 5w 30,
Ukikosa nenda 10w 30.....
.Anayekuambia hizi oil ni za nchi za baridi amekariri bila kusoma...

Iko hivi..
5w 30 ina uwezo wa kuhimili baridi kali kuanzia -30°C bila kupoteza viscosity yake...pia oil hii ina uwezo wa kuhimili kiwango cha juu cha joto ambacho ni +40 °C bila kupoteza viscosity yake..
Hiki kiwango cha joto nilichotaja ni joto la mazingira unayoishi (outside temperature)

10w 30 ina iwezo wa kufanya vizuri kuanzia joto la -20°C mpaka joto la +40°C...

Hii ina maana kwamba oil 5w30 na 10w 30 zina uwezo wa kusambaa haraka sehemu za injini hata kama gari limewashwa kwenye mazingira ya baridi sana kibongo bongo tunasema Arusha, Iringa, Mbeya na maeneo mengine yenye baridi.
Pia inahimili joto kali kama la Dar, Zanzibar nk.

Kwa hiyo hizi oil zinamudu mazingira yote na ndiyo maana car manufacturers wa siku hizi wana recommend oil hizi zaidi siyo Nissan, Toyota,Honda, Subaru,Mazda n.k...

Ukinunua nunua full synthetic ukikosa ndiyo ununue hizi mineral oil ambazo usivushe 3000 km.

Synthetic unaweza ukaenda km 5000 na zaidi kama umefunga oil filler genuine ndiyo ufanye service nyingine..

Full synthetic inahimili dhoruba ngumu kama milima, matope, joto, baridi, racing bila kupoyeza viscosity yake....na bei yake imesimamia kucha.

Agalia fundi wa mwembeni asikushauri uweke SAE 40 ya kawaida...hii oil ni nzito sana na utakuwa unalitesa gari bila wewe kujua...

Oil ndiyo DAMU ya engine.....zingatia if you love your car.
Mkuu nakuelewa sana... vp Carina Si nitumie engine oil gani???
 
Nimefuatilia kwa makini hii post...huwa nawekaga sae 40...gari imetembea 181k+km...vp bado hiyo 5w30 inafaa???
Yes jaribu kutumia 5W30, angalizo oil hii bei yake ni mara mbili ya sae 40 kwa kampuni yoyote ile ya oil na mm ninazo ofsn kwangu kwa kampuni zote genuine
 
Back
Top Bottom