kenzi
JF-Expert Member
- Oct 19, 2015
- 425
- 461
Hivi sage kwa kiswahili ni majani ya nn?Jamani [emoji15] [emoji15] [emoji5] [emoji5] [emoji39] [emoji39] [emoji39] [emoji144] [emoji144] [emoji144]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi sage kwa kiswahili ni majani ya nn?Jamani [emoji15] [emoji15] [emoji5] [emoji5] [emoji39] [emoji39] [emoji39] [emoji144] [emoji144] [emoji144]
Ushirikina mtupu, total vanity.Niwatakie weekend njema! Najua hizi ndio zile tarehe pendwa... Tarehe za kuitwa majina yote matamu[emoji3] [emoji3] [emoji3]
Nina hakika wengi wetu tumeshawahi kuchoma udi ama kuvukiza mavumba... Wakati mwingine ni taratibu za kiimani kimila ama hata masharti ya mganga
Nimevutika kuandika mada hii kutokana na reply ya mdau Ray 4 real kwenye moja ya mada zangu...
Nitaandika kwa mtazamo wa kijamii zaidi kuliko kiimani kwa maana ya dini![]()
Kwanza ni lazima utambue kuwa kuchoma UDI na kuvukiza mavumba kunajumuisha mambo mane makuu
1. Moshi wake ni alama ya hewa na pumzi yaani uhai.. Ukiashiria nguvu zisizoonekana kwa kusambaa na kutoweka milele
2. Moshi husika unatokana na moto, moto ni alama ya jua yaani mwanga
3. Kinachotoa moshi kinatokana na ardhi, ardhi ni msingi, ni mhimili wa dunia... Miti hupandwa ardhini
4. Moshi wake ni zao la maji, bila maji wala unyevu mti hauwezi kumea na kukua ukastawi na kutoa mazao yanayotumika kutengeneza udi
Hivi vinne vinakamilisha uumbaji katika misingi yake.
![]()
Sasa matumizi makubwa ya UDI na kuvukiza mavumba ni yapi?
-kutoa gesi asili ambayo
:italeta harufu anuwai zitakazotumika kwenye mambo ya kiroho, manuizi, matambiko na maagano
:kualika mizimu na mapepo na majini kwa nia ya kutengeneza ama kuharibu
:kuvuta ama kufukuza ukitakacho ama usichokitaka... Maranyingi hapa ni ishu za mahusiano na mapenzi
Lakini kumbuka kwamba si kila mti unaweza kutoa malighafi ifaayo kwa kutengeneza UDI na mavumba.. Miti ama malighafi zifaazo ni kama hizi
(A)Miti ya ubani, yaani miti itoayo malighafi ya ubani... Hii hutumika kutakasa, shughuli za kiroho na kiimani... Maana ya ubani kiroho ni jua na jua ni mwanga ambao unatafsiriwa kama NGUVU ya kiroho
(B) Mti utoao manemane... Mane mane kiroho ni alama ya uponyaji, ulinzi mvuto, na tunu.... Inahusishwa na mwezi ambao kiroho ni nguvu ya mwanamke
(C) Msandali/sandalwood, hutumika kwenye shughuli za kiroho na utakaso
(D) Msandarusi, hutumika kutakasa na mambo ya kiroho pia zana zake kuu ni rangi nyeupe nyeusi na dhahabu... Utakaso wake si wa kiroho tu bali hata kwenye vitu vinavyoonekana.. Huu ndio hutengeneza vanish ya kung'arisha fenicha
(E)Mwerezi/[emoji268] pine tree kutakasa na kinga dhidi ya nguvu hasi zote
(F) Joka mti damu. Hii hutumika kuimarisha mahusiano, kuleta uthubutu na kujiamini lakini mbaya zaidi ikitumika kinyume kwa kunuia husababisha uhanithi wa jinsia zote mbili
Kwahiyo ndugu zangu tunapoenda kutafuta tiba mbadala jihadharini sana na kupewa mavumba na nyudi... Kwakuwa sometimes mganga hukupa malighafi isiyo sahihi na yenye madhara makubwa
![]()
Alamsiki
Jr[emoji769]
Mmh kwa maelezo yako pale juu na haya hapa most likely unao hawa wapangaji na hawapendi harufu ya udiAu na mi ninao? Maana nilimpa mwanamke mmoja lift akiwa ameombewa na mtu ninayemheshimu. Tulitembea takribani km 33. Kwanza nililazimika kuzima AC na kufungua vioo lakini bado harufu ilinisumbua sana na baadae kumuomba mama ashuke. Maana tayari kichwa kilikuwa kinauma. Ma kawaida kweli sipendi harufu ya udi ila ubani unaowashwa kwa ajili ya kusoma dua haunisumbui. Je, ninaweza kuwa na matatizo ninayohitaji kushughulikiwa? Ushauri tafadhali. Ndo maana nikasema nilikuta harufu ya udi ndani ya ofisi na mtu alikuwa ameingia ni secretary. Sijawa na amani kwamba labda either hakuwa na nia nzuri kwangu au alikuwa na manuizo yake anayoyajua.
Jaribu kugoogle sage herb
Tatizo ni kwamba hata niliokuwa naomkwenye gari walisema harufu ilikuwa inawatesa.Mmh kwa maelezo yako pale juu na haya hapa most likely unao hawa wapangaji na hawapendi harufu ya udi
Halafu nilichogundua kwenye hii mada anayependa ubani hapendi udi na anayependa udi hapendi ubani
😀😀😀😀😀.Mshana nimekua nikiona UDI ukitumiwa na wavuta bangi hii imekaaje? Na pia Mimi hua napenda harufu yake sana na nikifukiza siku yangu hua inaenda vizuri sana na hua nanunua hizi za dukani kwa ajili ya sala japo ni mkristo hunifanya nijiskie amani ya roho vipi kuna lolote nisilolitambua hapa?