Enyi wazazi wapeni na waonesheni upendo watoto wenu

Enyi wazazi wapeni na waonesheni upendo watoto wenu

Ushimen

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
40,828
Reaction score
99,523
Good morning to all parents,

Straight to the point, wazazi wenzangu nawasihi sana tuwapende sana watoto wetu katika hali yeyote ile.

Tukiwa na fedha ama fukara, kitu pekee ambacho mtoto anahitaji zaidi kutoka kwa wazazi/mzazi ni upendo. Hayo mengine yote Mungu hubariki na huyafanya kwa wakati wake.

Ndugu wazazi wenzangu tusisahau kwamba; mafanikio ya mtoto huja kwa namna ama kupitia milango mingi, na kama ni fedha, utajiri, kipaji na mambo yote mazuri. Mtoto atayapata ikiwa tu ataupata UPENDO.

Niwatakie siku njema, yenye baraka, mafanikio na amani tele.
 
Mwanangu wamama wa stress za mikopo yaani watoto wanapigwa over and over.

Kina baba muwe mnawatupia macho sana hao watoto.
 
Mwanangu wamama wa stress za mikopo yaani watoto wanapigwa over and over.

Kina baba muwe mnawatupia macho sana hao watoto.
Wamama wa skuizi wakiamka wanawahi kuwasha simu badala ya kiwasha moto..🤣
 
Mwanangu wamama wa stress za mikopo yaani watoto wanapigwa over and over.

Kina baba muwe mnawatupia macho sana hao watoto.
Ni kweli madam, hasa maeneo ya uswahilini watoto hupokea vipigo mithili ya wezi, lkn chanzo kikubwa ni stress za maisha na hizo kausha damu
 
Ni kweli madam, hasa maeneo ya uswahilini watoto hupokea vipigo mithili ya wezi, lkn chanzo kikubwa ni stress za maisha na hizo kausha damu
Mkuu....
Haya yooote ni mkusanyiko wa mzazi kushindwa kumpa upendo mtoto wake.
Na watoto wanao nyanyaswa sana utotoni, matikeo yake hua wanakua wakatili sana ukubwani.
 
Back
Top Bottom