Erdogan anaongoza kwa kuwa Rais Ndumilakuwili duniani

Akili zahovyo kutoka kwakijana wahovyo kabisa[emoji2309]
Yaani lijinga hili.NATO na EU wapi na wapi?Kwenye NATO kuna US,Canada ambao hata hawapo bara la Ulaya. Mzee hajui NATO kwa nini ilianzishwa,na nini?Hivi atajua USSR kweli?Halafu ana udini jamaa.
 
That will never happen, tatizo waislamu ni ngumu kuassimilate Ulaya. Wazungu wamelijua hilo.Sasa mlengo wa kulia wanaongoza/wataongoza nchi na uislamu hauna nafasi kwa nchi zenye mlengo wa kulia .
 
Kashindikana...lakini sijui kama ana succession plan nzuri ..
Erdogan hana haja ya kuwa na succession plan, Uturuki ni nchi mojawapo yenye demokrasia ya wastani ila utaratibu mzuri sana wa kupata Rais.
 
Mturuki ndie mzalishaji mkubwa wa nguo,vifaa vya ujenzi n.k,walianzia soko lao east europe na kwa sasa soko lao limeenea hadi ulaya yote,wao ndio ufunguo wa kutoka na kuingia black hawataki kuegemea upande wowote kwa maslahi ya nchi yao
 
Naifahamu vizuri sana Geoengineering, ninachojiuliza ni kama inatumika kutengeneza matetemeko ya ardhi
Uturuki ipo kwenye ukanda wa tetemeko na huwa inayapata mara kadhaa, hata Iran ndio iko eneo hatari zaidi kwenye weak joints za earth's crust. Na Japan nayo iko eneo hatari la tectonic plates za baharini. Hivyo Uturuki na Iran kupata matetemeko sio suala la ajabu wala Japan kupata tsunami halitafutiwi mchawi.

Hayo matukio yana mamilioni ya miaka yanatokea. Marekani yenyewe inakumbwa na dhoruba na tufani mara nyingi tu. Mambo ya kusingizia HAARP kwa matukio ya kijiografia ni conspiracy theories, no evidence at all.
 
Alafu mbona hizo ndio sera za Uturuki kutokuwa na upande. Tangu vita ya kwanza ya dunia walivyojichanganya kwenye alliance yao na kusababisha kuvunjika rasmi kwa Ottoman empire wakagundua kuingia kwenye migogoro ya mataifa mengine kwa kiherehere hailipi, wakaanza kutanguliza maslahi yao kwanza.

Hata Mustafa Kemal alivyoona udini haulipi akauondoa na kuifanya nchi iwe secular, wakaondokana na tamaduni za Kiarabu na kuchanganya na za kizungu. Uturuki kwanza haiwapendi Waarabu kama ambavyo hawaipendi, ndio maana ina mchango mkubwa sana kwenye Uislamu duniani ila haipewi credit sababu wenye dini yao hawataki Uturuki ipewe sifa.

Erdogan ni kigeugeu kweli anafanya maamuzi kwa kutazama maslahi. Hata hivyo ni vigumu kuunga mkono uvamizi wa Putin kwa Ukraine, ingekuwa rahisi hata China ingekubali. Sababu za msingi za Urusi kuingia Ukraine hata hazipo, wanataja hizi kesho wanataja zile. Ila hapo kwa kutorosha mateka atafanya Uturuki isiaminiwe tena kwenye kusuluhisha migogoro.
 
Well said. Haya majanga yamekuwepo wayback, na kuna maeneo ni hatarishi kiasi huwa yanakua discouraged kuwa na population kubwa sababu even if tukio litakuja kutokea miaka 50 hadi 100 ijayo bado jamii ya sasa inakua na wajibu wa kuilinda jamii inayokuja kwa kuwa na protective plans.
Bahati mbaya wengi hupuuzia. Leo hii kama suyo sababu za utalii, basi watu wangeshavamia na kujenga around Mt. Oldonyo Lengai pamoja na kuambiwa volcano yako ipo active and it erupts
 
Kama ni hivyo kwanini wanang'ang'ania kuishi huko na hofu tele.Waje huku kwetu tuishi pamoja nao.
 

Una elimu ndogo kuhuau global diplomacy, uturuki ina approach za china, yaani just because wana ukaribu na urusi haimaanishi eti ndio wasifanye business na ukraine nope.
Nchi zina vipaombele vyake
 
Uturuki anacheza both sides Kwa maslahi yake...wala sio unafiki....

Hao NATO waliizuia Uturuki kuingia European Union kisa ni dini tu...
Wakati wako nao NATO...

Wamarekani wamesababisha tetemeko ili Erdogan atoke na wameshindwa

Werakani wamesababisha tetemeko? Seriously man [emoji23]
 
Una elimu ndogo kuhuau global diplomacy, uturuki ina approach za china, yaani just because wana ukaribu na urusi haimaanishi eti ndio wasifanye business na ukraine nope.
Nchi zina vipaombele vyake
Kwa elimu yako wewe.Sisi na Uturuki tunafanana kwa lipi na kipi cha kujifunza kutoka kwao.
 
Nato ni kijeshi tu.Ila EU kumbuka kuna free mouvement of people and goods kati ya wananchi wa nchi member wa EU.Yaani Uturuki wakiruhusiwa EU maana yake waturuki wanaweza kwenda kuishi Ujerumani, France,Italia,Grèce nk.
Ulokole ukizidi saaana ni tatizo pia
 
Umekasirika kweli... wachezaji Saba Tu wamekuuma...hebu nenda katoe pongezi kule Kwa Kardinali mpya...ukimaliza uanzishe thread ya kumtukana Samia 🤣
Utapata nafuu I am sure
Walokole na kadinali na vitu viwili tofauti. Kanda ya ziwa wengi ni walokole na wasabato
 
Kama ni hivyo kwanini wanang'ang'ania kuishi huko na hofu tele.Waje huku kwetu tuishi pamoja nao.
Nchi zote zisizo na changamoto nyingi za asili huwa za kipuuzi na zinaishi kwa tabu.
Nchi ambayo hata usipolima unaweza kula matunda pori basi ina watu wadumavu, akili ya mtu anayeishi sehemu inakuwa na winter vyakula vinakosa na mifugo inakufa njaa haiwezi kuwa sawa na akili ya mtu mwaka mzima jiografia yake inampa chakula bure.

Human development index inakuwa kubwa kwa nchi zenye shida. Kuna mzungu aliamua kutengeneza njia za kuhifadhi maziwa, mwingine akatengeneza njia ya kuhifadhi nyasi za malisho ya winter, mwingine akagundua sufi inazuia baridi na baadae wakagundua kuna bara la watu wanaishi dezo ukilima pamba kule watu watapata nguo. Ukishalima hizo pamba utazibeba mgongoni? Wakatakiwa kuwa na meli na treni. Watu wakafia viwandani kwa mazingira mabovu sheria za kazi zikatungwa, maslahi, mazingira rafiki yakaboreshwa, huduma za afya kama upasuaji na kuunga mifupa.
Waligundua nyumba inakuwa na baridi sana winter na watoto wanakufa kwa pneumonia wakajenga za mbao na kuweka heating system. Mambo mengi sana wameendelea sababu ya necessity.

Hao Iran wanatajwa ni mojawapo ya nchi zenye ufahamu mzuri kuhusu cement. Grades zao za cement ni kubwa sana sababu wanaishi kwenye tetemeko na ukitaka cement kali duniani katika options zako tatu ihusishe Iran hasa wale IRGC wanayotumia kujengea underground military facilities. Sasa unakuja kwa nchi kama Tanzania imepata tetemeko Bukoba limeua watu hata 20 hawafiki vilio nchi nzima na visingizio kibao hadi michango serikali ilikula.
Wakati Uturuki watu zaidi ya 50,000 wamekufa mwaka huu na maisha yanaendelea kama hamna kilichotokea, na uchaguzi wamefanya alafu shangwe mtaani kama kawaida na Erdogan ile Ijumaa ya mwisho kabla ya uchaguzi kakusanya watu zaidi ya milioni mbili uwanjani kutoa hotuba ya mwisho. Muda huohuo bado kuna miili ilikuwa haijapatikana.
 

ACHA UONGO WEWE ALAAA!

ULAYA NZIMA UISLAM HAUZIDI 25% SASA HIYO 2050 HAO 75% AMBAO SIYO WAISLAM ITAWAWEKA WAPI??

HALAFU UNAJIITA DR??

HOVYOOOOOO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…