Nifah
JF-Expert Member
- Feb 12, 2014
- 34,020
- 79,098
Poa best, utupe taarifa ukipata chochote.Mambo vipi Best, ngoja kwanza tuone,hii ingekua Kinshasa ningesema kitu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Poa best, utupe taarifa ukipata chochote.Mambo vipi Best, ngoja kwanza tuone,hii ingekua Kinshasa ningesema kitu
Mimi ndio wimbo wangu bora kwa Fally Ipupa, naupenda mno!Ila katika huu wimbo fally ipupa alituliza sana akili kumtungia mke wa jamaa na nadhan alipewa mkwanja mrefu sana .
Maana katika nyimbo 10 bora za fally MARIA PM imo.
hizo ni billion 16 bila kupepesa machoKilo Moja ya Cocaine inafika milioni 80 mpaka 90 aiseee iplus mara mia mbili 😂😂 uone maajabu
Yeaaah mimi kwenye list zangu ni maria pm, mayday,mon amour,service,aime moi na 1000%MAWA baada ya hapo nd lbda masebene yake hayo.Mimi ndio wimbo wangu bora kwa Fally Ipupa, naupenda mno!
Haa Haa Drugs DealerMarole model wa vijana wetu huko social networks.
Si huwa wanasema ukiwa boss wewe unaagiza tu vijana wanabeba, wakikamatwa unawapambania kuwatoa kazi iendelee! Sasa boss Mandala akaingia fronline yeye mwenyewe! Nani atampambania sasa!Pichani ni Eric Mandala Kizenga, raia wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Fally Ipupa alitunga wimbo maarufu kumsifia mkewe, Maria Piron Mandala (PM). Wimbo huu ulizua gumzo sana, na kuonyesha namna alivyokuwa akimpenda mkewe.
Hata hivyo, kuanzia juzi, habari kuhusu Eric Mandala zimekuwa tofauti kabisa. Mtu huyu ambaye alikuwa akitajwa kuwa na utajiri mkubwa nchini Kongo sasa amekumbwa na kashfa kubwa. Juzi, akiwa nchini Colombia, Eric Mandala alikamatwa akiwa na kilo 200 za cocaine ndani ya gari lililokuwa limeegeshwa kwenye moja ya malls maarufu nchini humo.
Cocaine hiyo inadaiwa ilitoka Ecuador na ilikuwa inaelekea Morocco kupitia bandari ya Algeciras, Hispania.
Mandala alikamatwa pamoja na mwanamke wa Kikolombia, na walikamatwa wakiwa na kiasi cha dola 50,000 za kimarekani taslimu. Polisi waligundua kuwa Eric Mandala alikuwa akifuatiliwa na maafisa wa kudhibiti dawa za kulevya tangu Agosti mwaka jana, na hatimaye alikamatwa juzi kwenye mtego wao.
Zaidi ya hayo, mwaka 2020, Eric Mandala alijivunia kununua nyumba ya kifahari katika jengo refu zaidi duniani, Burj Khalifa, jijini Dubai, kwa kiasi cha Euro milioni 1.85 cash, jambo ambalo lilishangaza wengi na kuacha vinywa wazi.
Wakati Eric Mandala akisota kwenye mikono ya polisi, maswali yanajitokeza kuhusu kama Adolphe Muteba Tshilamwina ataungana na mzozo huu au ataepuka mtego huu. Hali inavyokuwa ni ngumu kusema, lakini ni wazi kuwa hadithi hii itazidi kutoa makala nyingi.
View attachment 3214542
AngeKamatwa Congo ingekua rahis kuzima bati kakamatiwa mbele, japo sio mbele kivilee!Hapo amechoreshwa t na wafanyabiashara wenzie,ila nakuhakikishia, hautakuja kusikia tena hii kesi imeendelea. Mwenye pesa sio mwenzio.
Sawa sawa..Nadhan na yeye ana boss wake
Nilikuwa najiuliza hilo jina niliwah kulisikia kwenye wimbo upi unaosound kidiamond diamond nikashindwa kuukumbuka,asante kwa kunikumbusha kumbe ni wimbo wa huyu dogoBoss, Eric Mandala🕺🏿
View attachment 3214543
Mmhhh hatariPichani ni Eric Mandala Kizenga, raia wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Fally Ipupa alitunga wimbo maarufu kumsifia mkewe, Maria Piron Mandala (PM). Wimbo huu ulizua gumzo sana, na kuonyesha namna alivyokuwa akimpenda mkewe.
Hata hivyo, kuanzia juzi, habari kuhusu Eric Mandala zimekuwa tofauti kabisa. Mtu huyu ambaye alikuwa akitajwa kuwa na utajiri mkubwa nchini Kongo sasa amekumbwa na kashfa kubwa. Juzi, akiwa nchini Colombia, Eric Mandala alikamatwa akiwa na kilo 200 za cocaine ndani ya gari lililokuwa limeegeshwa kwenye moja ya malls maarufu nchini humo.
Cocaine hiyo inadaiwa ilitoka Ecuador na ilikuwa inaelekea Morocco kupitia bandari ya Algeciras, Hispania.
Mandala alikamatwa pamoja na mwanamke wa Kikolombia, na walikamatwa wakiwa na kiasi cha dola 50,000 za kimarekani taslimu. Polisi waligundua kuwa Eric Mandala alikuwa akifuatiliwa na maafisa wa kudhibiti dawa za kulevya tangu Agosti mwaka jana, na hatimaye alikamatwa juzi kwenye mtego wao.
Zaidi ya hayo, mwaka 2020, Eric Mandala alijivunia kununua nyumba ya kifahari katika jengo refu zaidi duniani, Burj Khalifa, jijini Dubai, kwa kiasi cha Euro milioni 1.85 cash, jambo ambalo lilishangaza wengi na kuacha vinywa wazi.
Wakati Eric Mandala akisota kwenye mikono ya polisi, maswali yanajitokeza kuhusu kama Adolphe Muteba Tshilamwina ataungana na mzozo huu au ataepuka mtego huu. Hali inavyokuwa ni ngumu kusema, lakini ni wazi kuwa hadithi hii itazidi kutoa makala nyingi.
View attachment 3214542
Inamaana prezidaa kaonyesha uzalendoView attachment 3214931
Akiwa na Félix Tshisekedi,raisi wa Democratic Republic of the Congo