Eric Mandala akamatwa na kilo 200 za Cocaine

Eric Mandala akamatwa na kilo 200 za Cocaine

Ukishafika kwenye kilo 200 maana yake huo ni mzigo wa cartel za huko south america
hao wajuba ukibugi stepu wanaua mpaka bibi yako mzaa babu....
Ndio kitete cha kuukabidhi mwenyewe kimemlostisha
Halafu ukiangalia Spain kwa cartel ndio capital city yao.....
 
Pichani ni Eric Mandala Kizenga, raia wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Fally Ipupa alitunga wimbo maarufu kumsifia mkewe, Maria Piron Mandala (PM). Wimbo huu ulizua gumzo sana, na kuonyesha namna alivyokuwa akimpenda mkewe.

Hata hivyo, kuanzia juzi, habari kuhusu Eric Mandala zimekuwa tofauti kabisa. Mtu huyu ambaye alikuwa akitajwa kuwa na utajiri mkubwa nchini Kongo sasa amekumbwa na kashfa kubwa. Juzi, akiwa nchini Colombia, Eric Mandala alikamatwa akiwa na kilo 200 za cocaine ndani ya gari lililokuwa limeegeshwa kwenye moja ya malls maarufu nchini humo.

Cocaine hiyo inadaiwa ilitoka Ecuador na ilikuwa inaelekea Morocco kupitia bandari ya Algeciras, Hispania.

Mandala alikamatwa pamoja na mwanamke wa Kikolombia, na walikamatwa wakiwa na kiasi cha dola 50,000 za kimarekani taslimu. Polisi waligundua kuwa Eric Mandala alikuwa akifuatiliwa na maafisa wa kudhibiti dawa za kulevya tangu Agosti mwaka jana, na hatimaye alikamatwa juzi kwenye mtego wao.

Zaidi ya hayo, mwaka 2020, Eric Mandala alijivunia kununua nyumba ya kifahari katika jengo refu zaidi duniani, Burj Khalifa, jijini Dubai, kwa kiasi cha Euro milioni 1.85 cash, jambo ambalo lilishangaza wengi na kuacha vinywa wazi.

Wakati Eric Mandala akisota kwenye mikono ya polisi, maswali yanajitokeza kuhusu kama Adolphe Muteba Tshilamwina ataungana na mzozo huu au ataepuka mtego huu. Hali inavyokuwa ni ngumu kusema, lakini ni wazi kuwa hadithi hii itazidi kutoa makala nyingi.

View attachment 3214542

yeah, mwisho wa ubaya (dhambi) ni aibu.

Ingekuwa China mambo yangenoga zaidi
 
Nenda pale BOT waulize kwa pesa hio wanakupa mawe mangapi ya dhahabu tupu, wakikupa jibu njoo hapa utuletee mrejesho
Wala sina haja ya kufanya hivyo mkuu. Kwa sababu nijuavyo mtu yeyote mwenye fedha nyingi haramu kutumia TZS 5b kwenye jambo lolote hata liwe la kipuuzi siyo ajabu sembuse kununua penthouse kwenye jengo tajwa. Yaani watu wawe wanamjua fulani kwamba ni tajiri halafu wakisikia kuwa mtu huyo katumia Euro 1.85m ambazo ni around TZS 5b kununua penthouse mahali fulani washangae na kubaki midomo wazi? Mzaha huo.
 
Le boss,
walikua wanamfwatilia yeye alijsahau tu..
Mandala kaimbwa sana na Emilia Elyas,Ferre gola , mwaka juzi alidakwa na wakamuachia kaenda kufanya ushumbwanda tena.
Swala kumuachia ilikua kupata ushahidi usio na mashaka.hakujua hilo.
 
Ukishskuwa kwenye circle kuba hivyo ujue kuacha ni ngumu. Yeye n boss ila kuna maboss wakubwa zaidi yake. Na hao ndio wanao mpushi kwa lazima. Wakiamini hela itasafisha njia
 
Watakaomtoa ni mapapa wake huko Spain. Naamini penye hela sheria ni kama bigjii tu.
Unaweza kuta hata kukamatwa kwake alitaka kuleta nyodo kwa vibopa wakataka wampe funzo. Ukifanya biashara hiyo kuna nyakati utataka uache. Maboss wanakubembeleza kisha unawaambia nafanya kwa mara ya mwisho. Ukisema hivyo tu.. Jiandae kuchomeshwa
 
Watakaomtoa ni mapapa wake huko Spain. Naamini penye hela sheria ni kama bigjii tu.
Ndio hivyo mkuu huyo jamaa anatoka watamtoa mapapa wanaosimamia mchezo ila angedakwa China ndio ingekua kwakheri ya kuonana, Colombia rushwa inatembea km Banana Republic
 
Unaweza kuta hata kukamatwa kwake alitaka kuketa nyodo kwa vibopa wakataka wampe funzo. Ukifana biashara hiyo kuna nyakati utataka uache. Maboss wanakubembeleza kisha unawaambia nafanya kwa mara ya mwisho. Ukisema hivyo tu.. Jiandae kuchomeshwa
Ndio hapa umesema jambo kwa hio hapo wanakutana mahabusu na mwanasheria anaenda kumsorondesha vipi ndio mara ya mwisho ulale ndani miaka yote au unaendelea na mzigo tukutoe baada ya wiki moja?
 
Ingekuwa rahisi hivyo hata Hush Puppy angetoka. Wauza madawa wote wakubwa wapo kwenye rada za Wamarekani
Hush Puppy hakua muuza Madawa ila alikua kijana mmoja masikini limbukeni wa kinaijeria Tapeli wa kimtandao aliekubuhu aliewaumiza wengi kwa muda mrefu kwa kuwaibia mabilioni ya dollars na kujionyesha mitandaoni, na usichojua kafungwa muda mfupi sana sababu kawauzia ramani nzima ya mchezo ili wengine nao wanaocheza michezo km yake wadakwe watiwe ndani bila hivyo angechezea mvua nyinyi sana nyuma ya nondo
 
Back
Top Bottom