TANZIA ERICK ADAMU (Nezo B-Msanii wa Bongo Fleva) Auawa kisa kudaiwa pesa ya umeme (LUKU)

TANZIA ERICK ADAMU (Nezo B-Msanii wa Bongo Fleva) Auawa kisa kudaiwa pesa ya umeme (LUKU)

Vifo asaivi ni kama timing,
Unagombana na mtu ukiona kashika siraha, tumia miguu yako vzr,

Sio zamani mtu katoa panga upo hapo unamuambia nikate sasa, nikateee....

Sikuhizi watu hawatanii, kitu ikitoka hairudi kavu, unageuzwa mishkaki, unapelekwa pluto fasta.

Usiwe na shaka kuhusu mbio zako katika kuokoa uhai, hutajiamini hio siku, nishawahi pita NOAH kama ipo Parking na ile ndio ilikua pona yangu serious, sijawahi rudi ile sehemu as long najua nilizingua mwenyewe.
[emoji16] [emoji16] [emoji16]
 
Umoufia Kwenu wana JF,

Msanii wa Bongo fleva usiku wa kuamkia leo ameuwawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali huko sanawari Atown ,chanzo cha ugomvi ni mchango wa Buku ya umeme ambayo ilitakiwa achange kwenye nyumba aliyopanga,baada ya mvurugano ndipo mwanadada akatoka aliporudi akaja na kitu chenye ncha kali na kumchoma na kupelekea umauti.

View attachment 2663242

Cc: Bushmamy
Noma sanaa aisee, bidada alikuwa ashameza vitu adimu
 
Ndugu zangu kuwenu makini na ugomvi ,tunajaribu ku-control hasira zetu ...Hasira huleta majuto baadae .


Mambo ya ugomvi haswa ukiwa mtu mzima sio mambo ya kujisifu ndo maana vijana wa huo mkoa wanajifanya wagomvi ,wababe kitu ambacho wengine tunaona kama ni utoto na ushambwa wa vijijini ..

Ugomvi sio mzuri faida hakuna ni matatizo tu.!!
 
Sema habari kama hizi huishia juu juu tu, hapo waandishi washamaliza.
Kilichojiri kimeripotiwa juu juu tu halafu wanapita ivi hakuna muendelezo.
 
Mwanamke anayefahamika kwa jina la Blandinda Fredi Mkazi wa Kijiji cha Ilkrevi Kata ya Olturoto Wilayani Arumeru Mkoani Arusha anatuhumiwa kumuua Erick Adam ambaye ni Msanii wa Bongofleva na Mfanyakazi wa kiwanda cha mikate chanzo kikidaiwa kuwa ni kudaiana pesa ya LUKU (umeme).

Mashuhuda wa tukio hilo wanasema walishuhudia ugomvi ukiwa unaendela ambapo baadaye walimkuta Kijana huyo akiwa tayari ameshachomwa kisu.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho Mollel amesema ni kweli Kijana huyo amefariki na wamempeleka katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Rufaaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru.


Lazima ni wa Meru0
 
Back
Top Bottom