TANZIA ERICK ADAMU (Nezo B-Msanii wa Bongo Fleva) Auawa kisa kudaiwa pesa ya umeme (LUKU)

TANZIA ERICK ADAMU (Nezo B-Msanii wa Bongo Fleva) Auawa kisa kudaiwa pesa ya umeme (LUKU)

JESHI la Polisi mkoani Arusha, linamshikia Blandina Fred mkazi wa Kijiji cha IIkirev, Kata ya Olturoto wilayani Arumeru, kwa tuhuma za kumuua kwa kumchoma kisu mpangaji mwenzake, Erick Adam kisa shilingi 1000 ya mchango wa umeme.

Tukio hilo limetokea Jana baada ya kutokea ugomvi baina ya wapangaji hao wawili ambapo inadaiwa marehemu Adam aligoma kulipia deni la umeme ambao kwa kawaida wapangaji huchangia.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Justine Masejo akizungumza na chombo kimoja cha habari leo, June 20, 2023, amesema tukio hilo lilitokea majira ya mchana wakati, Blandina akiwa na kisu akijiandaa kupika.

"Kilichotokea ni kwamba wote ni wapangaji walikuwa wakigombana huyu binti alikuwa na kisu kwa kuwa alikuwa jikoni, sasa ndio alimchoma mwenzake," amesema.

Amesema Adam alifariki kutokana na kutokwa na damu nyingi baada ya kuchomwa kisu, huku mtuhumiwa bado yupo chini yaulinzi kwa mahijiano zaidi, na taratibu zikikamilika atafikishwa mahakamani.
 
Unajua hii kitu umeme unaweza ndio uli trigger vitu vilivyokua nyuma ya pazia na maelewano kati ya hawa wawili lazma kuna untold story ila ukimhoji aliyeua anaweza akakuambia nn kilipelekea yeye kufanya ivoo
 
Haya yanaweza kutokea popote,haijalishi asili ya mtu.
Billionaire Msuya na wengine kadhaa ikiwa ni pamoja na yule mwanamke aliyemuua mama yake akishirikiana na majambazi yote hayo ni ukanda huo
 
Nimekuzidi mara mbili. Mie nusuti
Untitled.jpg

huyo siyo ?
 
Back
Top Bottom