Erick Kabendera: Mwendazake aliendesha genge la wahuni na alikusudia kumkamata Rais Mstaafu Kikwete

Erick Kabendera: Mwendazake aliendesha genge la wahuni na alikusudia kumkamata Rais Mstaafu Kikwete

View attachment 2386088
Legacy inazidi kuzamishwa chini zaidi. Mwendazake alikuwa wa hovyo sana

====
Aliyoandika Kabendera

Wale mliouza mali zenu kupata pesa za kuhonga kusaidia plea bargain zenu zikubaliwe mjitokeze kutoa ushahidi. Wafanyabiashara mliopelekwa ofisi maarufu ya serikali, mkatishwa kwa mitutu ya bunduki wakati Mwendazake akiangalia kupitia CCTV, mkalazimishwa kutoa pesa mjitokeze.

Kuna mfanyabiashara maarufu alipitia mateso makali kwa kipindi cha miaka minne, ikiwemo kubinywa korodani, akilazimishwa aseme uongo kuwa alitoa dola milioni 100 kwa Rais Kikwete. Mwendazake alitaka kutumia ushahidi huo kumkamata Kikwete. Ni lazima atendewe haki.

Tuhuma dhidi ya Mwendazake kuanzisha na kuendesha genge la kihalifu nje ya mfumo wa serikali na kutoa maelekezo kwa genge hili kuwaua viongozi wa vyama vya upinzani, CCM na viongozi wakuu wastaafu ambao wangekuwa kikwazo kwake kutawala milele zichunguzwe pia.

Si mara ya kwanza zoezi kama hili kufanyika; Rais Mwinyi aliunda tume ya kupitia upya kesi zote ya uhujumu uchumi alizoziendesha Sokoine baada ya kuingia madarakani na kuna watu walirudishiwa mali zao.

Binafsi nimeombwa kuwasilisha maelezo ya maandishi kwa mamlaka husika kuhusu vitisho alivyovitoa Ndugu Biswalo dhidi yangu mara kwa mara baada kuachiwa huru na nimefanya hivyo.
Tarehe 17 03 2021 itabaki kuwa siku ya ukombozi wetu Watanzania. Nchi ilikuwa inaenda kuzimu kabisa,asante Mungu kutuamulia huu ugomvi.
 
NI kweli marehemu alikuwa na michezo ya kihuni.
Ila kwa Sasa haya unayofanya bwana kabendera hayana maana.
Yupo zake chato anajigeuza geuza.
Na kule alipo Hana smartphone
Lazima yasemwe ili Kama Kuna waliobakia wawajibishwe walioshirikiana nae Kama kina biswalo mganga
 
Nadhan ulikuwa mtoto ww,vp vile viroba vya maiti baharin?
Vip wale wasiojulikana waliokuwa wakilindwa????
Acha kujitia upofu
Yaani ni bidii na juhudi za kuondoa legacy iliyopo. Hata siku moja haitafanikiwa. Legacy utaiondoaje? Na Mungu anakasirika kwa juhudi za kishetani kama hizo. Ona mauaji ya kiajabu yanayofanana na yale ya albino albino yamerudi. Ona ajali zinazoua makumi ya watu zimerudi na tulishasahau yote hayo. JPM aliingia mauaji ya albino STOP. Vifo vya ajabu ajabu stop. Sasa wamefanya walichofanya JPM hayupo yamerudi hayo mauaji. Bila toba kwa Mungu hii nchi ni finished. Ona ukame wenzetu majirani mvua kuliko wastani. Jamani TUTUBU kwa ajili ya waTZ waliomfa nyia mabaya na wanaoendeleza kujaribu kufuta legacy japo KAMWE hawatafanikiwa
 
Duh!

Ndio maana alisema kuna wastaafu wanawashwawashwa.

Huyu Bwana alikuwa ni mtu hatari sana!

Ukiangalia ile picha aliyokuwa amepiga magoti akiomba kura kwenye kampeni za 2020, unaweza hata kumuonea huruma na ukapata picha kuwa ni mtu mpole na humble, kumbe ni kinyume chake kabisa!

Niliwahi sema humu na leo narudia: Mwendazake alikuwa na kipaji kikubwa sana cha uigizaji, sema tu hakuingia kwenye hiyo sanaa ange-fit zaidi huko.
Alikua ni professor wa unafki
 
View attachment 2386088
Legacy inazidi kuzamishwa chini zaidi. Mwendazake alikuwa wa hovyo sana

====
Aliyoandika Kabendera

Wale mliouza mali zenu kupata pesa za kuhonga kusaidia plea bargain zenu zikubaliwe mjitokeze kutoa ushahidi. Wafanyabiashara mliopelekwa ofisi maarufu ya serikali, mkatishwa kwa mitutu ya bunduki wakati Mwendazake akiangalia kupitia CCTV, mkalazimishwa kutoa pesa mjitokeze.

Kuna mfanyabiashara maarufu alipitia mateso makali kwa kipindi cha miaka minne, ikiwemo kubinywa korodani, akilazimishwa aseme uongo kuwa alitoa dola milioni 100 kwa Rais Kikwete. Mwendazake alitaka kutumia ushahidi huo kumkamata Kikwete. Ni lazima atendewe haki.

Tuhuma dhidi ya Mwendazake kuanzisha na kuendesha genge la kihalifu nje ya mfumo wa serikali na kutoa maelekezo kwa genge hili kuwaua viongozi wa vyama vya upinzani, CCM na viongozi wakuu wastaafu ambao wangekuwa kikwazo kwake kutawala milele zichunguzwe pia.

Si mara ya kwanza zoezi kama hili kufanyika; Rais Mwinyi aliunda tume ya kupitia upya kesi zote ya uhujumu uchumi alizoziendesha Sokoine baada ya kuingia madarakani na kuna watu walirudishiwa mali zao.

Binafsi nimeombwa kuwasilisha maelezo ya maandishi kwa mamlaka husika kuhusu vitisho alivyovitoa Ndugu Biswalo dhidi yangu mara kwa mara baada kuachiwa huru na nimefanya hivyo.
Hivi huyu Erick hua akomi sema huyu maza mpole sana
 
Kwani ile haki ya kikatiba ya kufanya mikutano mbna yule kubwa la maadui alipiga marufuku???
Kwa katiba ya nchi hii Rais akiamua kufanya lolote anaweza bila kutishwa na yoyote.

Kama unataka kujua nguvu ya Rais kikatiba ktk nchi hii muulize yule andunje wa kongwa atakupa ushuhuda murwa kabisa
Kabendera kaandika uongo

Katiba ya nchi inamlinda Raisi akiondoka madarakani hairuhusiwi kumkata wala kumshtaki kwa lolote alilotenda akiwa Raisi

Analindwa na katiba

Kabendera yuko sifuri kichwani kuhusu katiba
 
Vyeti feki acha chuki,Magufuli amefariki sukari ilikua 2,200/=
Wewe acha uwongo, labda ulikuwa Burundi ndiyo maana unapinga tu.

Halafu nashangaa kila anayepinga udhalimu wa Magufuli anaitwa Cheti Feki au Fisadi. Hiyo siyo sawa, kuwa na Cheti Feki hakuchukui haki ya mtu kutoa maoni. Isitoshe hata Magufuli mwenyewe alikuwa na PhD Feki. Leta hoja nyingine
 
Kabendera umeanza Tena naona hujakoma. Achana na system
System ya nioko ,Huu upumbav,unafiki, uchawa na uoga WA kijinga ndio ulisababisha maafa awamu iliyopita ,watu wakafilisiwa ,wakauawa , kutekwa ,kuteswa ,kubambikizia kesi za uongo ,kutishwa na kuchafuliwa Kwa kashfa mbovu za uongo
 
Back
Top Bottom