Eti Mbowe alitoa laki 6 kufadhili ugaidi. Seriously?

Mbona hujashangaa eti Sabaya alitumia mtutu wa bunduki kupora elfu thelethini...!!!!!
 
 
Kwamba Mbowe peke yake,Bila kuwashirikisha viongozi waandamizi wenzake ndani ya chama,anatoa laki sita kuwapa makomandoo watatu walioachishwa kazi jeshini.

Pengine kila mmoja atumie laki mbili ili.
1.walipue vituo vya mafuta vya Mwanza,Arusha,Dsm,Mbeya,na kilimanjaro.
2.walipue masoko yenye mkusanyiko wa watu wengi, mfano kariakoo,soko la Mwanza na mengineyo.

Hivi kweli Mbowe huyu huyu tunaemjua ambae pale Mwanza kwenye sherehe za uhuru Mbele ya makamera na Mbele ya Magufuli aliomba maridhiano ya kitaifa anaweza kweli kupanga njama za kutaka kulipua masoko yenye watu wengi? Kulipua vituo vya mafuta nchi mzima?

Lakini ajabu kwa kuwatumia watu watatu tu na shilingi laki sita Mbowe aliwaelekeza wakate miti iliyoinamia Barabarani ili pengine kuzuia nagari yasipite kuanzia Morogoro kwenda iringa.

Mbowe huyu huyu?
Tanzania imebadilika Sana aisee.
 
Kawaida kwa mwenye hila hachelewi kumsingizua nwebye nia njema ndiye mwenye hila.
 
yani Mbowe alipe makomando kwa kulipua vituo vya mafuta🤣 kwani ufipa hakuna vijana wa kufanya hiyo kazi mpaka alipe makomando kama kweli alikuwa na nia hiyo
 
Moyo wa mtu msitu kijana. Kuna watu unakuta mchana mchamungu na mwema, usiku mchawi na katili.Mleta mada ungekuwa una undugu na familia ya Chacha Wangwe leo usingeandika ujinga huu.
 
Bavicha mna shida sana!

Huwa mnawekeza akili kwa wanasiasa alafu wakiwageuka mnabaki kama yatima!

Ilikuwa kwa Zitto
Ikaja kwa Slaa
Ikaja kwa Mdee
 
Usiniwekee maneno mdomoni mkuu.... ukifurahia wewe inatosha

Halafu tabia hii yako ya umbea na uzushi wa mambo sio nzuri kabisa haswa kwa forum inayoheshimika kama hii
futa hii na ujiheshimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…