mgen
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 23,169
- 9,054
Tumesha kuelewa ww ni kipenzi wa Mbowe na chadema kindaki ndaki!Ligaidi halichomoki hata mseme nini.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tumesha kuelewa ww ni kipenzi wa Mbowe na chadema kindaki ndaki!Ligaidi halichomoki hata mseme nini.
Bado tu hujapeleka swala hili zito na kubwa namna hii TAKUKURU? Wahitaji kufuatiliwa.Mbowe lazima afungwe, naona mwanaharakati wa kichagga anamtetea mchagga mwenzake aliyeanzisha chama chakuwatetea wachagga Tanzania, mashahidi na mawakili wengi kwenye kesi ya Sabaya ndio nyie nyie, inatia mashaka.
Muangalie huyo wakili anamsimamia Sabaya koa mpaka dactari aliyekuja kutoa ushahidi mahakamani. Duh! Laana ya ukabila mbaya sana
Mpumbavu isije ikawa ni wewe. Look, Jaji mahiri atajiuliza sana laki sita zitafanya ugaidi wa vipi, ataanzia hapo kuangaliwa ushahidi kwa umakini Sana.Hoja ya 600K ni ya kipumbavu.
Nadhani nimeeleweka.
Na likichomoka utajajinyea na kutembea uchi wa manyama mtaani na kinyesi chako???,acha kujitoa ufahamu wewe,utateseka sanaaa.Ligaidi halichomoki hata mseme nini.
Kabisa, tena ni ufipa haswa.Tumesha kuelewa ww ni kipenzi wa Mbowe na chadema kindaki ndaki!
Hasira za nini sasa?Na likichomoka utajajinyea na kutembea uchi wa manyama mtaani na kinyesi chako???,acha kujitoa ufahamu wewe,utateseka sanaaa.
Huyu bibi anapelekwa tu na akina SirroMpumbavu isije ikawa ni wewe. Look, Jaji mahiri atajiuliza sana laki sita zitafanya ugaidi wa vipi, ataanzia hapo kuangaliwa ushahidi kwa umakini Sana.
Nakubali hata shilingi Moja inaweza kufanya ugaidi, but inamsitua mtu mwenye akili kujiuliza maswali mengi na hivyo scrutiny ya ushahidi itakuwa Kali. It is an eye catching figure with the intended act.
Ni uonevu wa kijinga tupuNa likichomoka utajajinyea na kutembea uchi wa manyama mtaani na kinyesi chako???,acha kujitoa ufahamu wewe,utateseka sanaaa.
"Mtu mwenye akili, akikuambia jambo la kijinga na wewe ukamkubalia, atakudharau".Washauri wa mama wanamdanganya hapo
Basi kama hata shilling moja inaweza kufanya ugaidi ni upumbavu kukataa nguvu ya laki 6.Mpumbavu isije ikawa ni wewe. Look, Jaji mahiri atajiuliza sana laki sita zitafanya ugaidi wa vipi, ataanzia hapo kuangaliwa ushahidi kwa umakini Sana.
Nakubali hata shilingi Moja inaweza kufanya ugaidi, but inamsitua mtu mwenye akili kujiuliza maswali mengi na hivyo scrutiny ya ushahidi itakuwa Kali. It is an eye catching figure with the intended act.
Ndio mnajipanga pa kutokeaUtani utani anaishia jela kama babu seya
Hujamwelewa mkuu Retired rudi ukasome tena tena utulie.Basi kama hata shilling moja inaweza kufanya ugaidi ni upumbavu kukataa nguvu ya laki 6.
Yes Hana self judgements, tumepata hasara Sana. Huyu bure kabisa kabisaHuyu bibi anapelekwa tu na akina Sirro
Anachoweza ni kusafiri pekeeYes Hana self judgements, tumepata hasara Sana. Huyu bure kabisa kabisa
Acha upumbavu wewe. Anajua mengi juu ya bimkubwa wako amma nn?Huyu Malisa aunganishwe kwenye tuhuma za Mbowe haraka anaonekana anajua mengi
USSR
Umeandika gazeti refuuu lakini limejaa utopolo mtupu! Kwani kufadhiri ugaidi lazima utoe pesa kiasi gani? Unaweza kuwasaidia magaidi hata usafiri tu wakuwatoa point A kwenda point B na ukawa na hatia ya kufadhiri ugaidi. Tumia akili kidogo acha kuwa na akili za kinyumbu mkuu!Kabla ya Mbowe kusomewa mashtaka, watu waliipa Jamhuri "benefit of doubt" kwamba huenda ina ushahidi wa maana. Watu wakahisi labda Mbowe ana uhusiano na makundi ya kigaidi kama Al Shabab, Al Queda, Boko Haram etc na pengine anapeleka vijana huko kwa ajili ya mafunzo.
Hayo ndio yalikua matarajio ya wengi. Hata Kigogo alisema subirini asomewe mashtaka mtashangaa. Dada yetu wa Marekani nae akasema ameelezwa mambo mazito kuhusu tuhuma za Mbowe na ugaidi.
Lakini kilichotokea leo ni tofauti na matarajio ya wengi. Eti Mbowe alitoa laki 6 kufadhili ugaidi. Seriously? Huu ndio ule ushahidi mzito tuliokua tunaungojea? Hiki ndio kile ambacho Mama aliiambia dunia kwamba Mbowe alifadhili ugaidi halafu akatoroka nchi? Yani alifadhili ugaidi kwa laki 6 halafu akakimbia?🤣.
Kama ugaidi unaweza kufadhiliwa kwa laki 6, basi nchi yetu ingekua na vikundi mengi sana ya kigaidi. Kwa mujibu wa ripoti ya BBC ya December mwaka jana, Kundi la Al Shabab linakusanya zaidi ya $180M kama kodi kutoka kwa raia wa Somalia. Hizo ni sawa na TZS Bilioni 400. Pia wanapata ufadhili kutoka taasisi mbalimbali unaokadiriwa kufikia $900M kwa mwaka sawa na TZS 2.2 Trilioni.
Kwahiyo bajeti ya Al Shabab kwa mwaka ni zaidi ya TZS Trilioni 3. Hicho ni kikundi cha kigaidi ambacho kiko hapo Somalia. Lakini Tanzania tuna kikundi cha kigaidi cha Mbowe chenye bajeti ya laki 6 kwa mwaka. Funny but not funny.
Mashtaka ya leo yameonesha huenda serikali haikujipanga na kesi hii, na yamezidisha mashaka ya wale waliokua wakisema Mbowe amekamatwa kwa sababu za kisiasa ikiwemo kudai katiba mpya. Watu walitegemea hati ya mashtaka iliyosheheni "serious offence" za ugaidi, sio hiki kilichopelekwa mahakamani leo. Hata CCM wenyewe wamepigwa butwaa kusikia hizi tuhuma za Mbowe kufadhili ugaidi kwa laki 6.
Pia tuhuma za kutaka kuchoma vituo vya mafuta ni kituko kingine. Kama Mbowe alikua na "roho mbaya" kiasi hicho basi angepanga kuchoma vituo vya mafuta baada ya matokeo ya uchaguzi 2015, kwa sababu wananchi walikua tayari kwa lolote. Lakini akatumia hekima kuwatuliza. Akaonekana muoga lakini hekima ikamuongoza, kuhakikisha hakuna hata mtu mmoja anajeruhiwa kwa sababu ya uchaguzi.
Sasa kama aliweza kutiza watu waliokua kwenye "tention" kubwa kiasi kile akafanikiwa, angewezaje kupanga kuchoma moto vituo vya mafuta kwa sababu ya Sabaya? Halafu akishachoma yeye ndio anakuwa Mkuu mpya wa wilaya ya Hai? What a crap?
Pia tuhuma za kupanga kumuua Sabaya nazo zina ombwe. Askofu mmoja leo amesema Mbowe hawezi kupanga kumuua Sabaya, lakini Sabaya anaweza kupanga kumuua Mbowe. Ushahidi wa kimazingira unaonesha hivyo.
Sabaya amewahi kuvamia hotel moja ya kitalii akiwa na bunduki, akataka kuoneshwa chumba alicholala mwanamuziki mmoja wa bongoflava ili aende kumbaka. Walinzi wakakataa kumuonesha. Akiwa na mabaunsa wake wakawapiga wale walizi na kuwalaza rumande. Tukio hilo lilirekodiwa kwa CCTV camera za hoteli hiyo lakini wala hakujali.
Sabaya amewahi kutumia magari binafsi akayapachika namba za umoja wa mataifa kisha akaenda kufanya nayo uhalifu, bila kujali kwamba anaharibu diplomasia yetu kimataifa. Sabaya amewahi kumvamia diwani mmoja huko Machame na kutembeza kipigo kwa familia nzima, kisha akamkata sikio mtoto wa diwani huyo.
Sasa jiulize kati ya Sabaya mwenye rekodi za ukatili kiasi hiki, na Mbowe mwenye rekodi za kutumia hekima kutuliza "tention" za watu, nani anaweza kupanga kumuua mwenzie? Kusema Mbowe alipanga kumuua Sabaya ni sawa na kusema Papa Francis anapanga kumteka kiongozi wa Boko Haram. Future imposible tense.
Halafu kumbuka Sabaya ndiye aliyetoa tuhuma hizi za kutaka kuuawa. Watu wanauliza je kuna uhusiano gani kati ya Sabaya na Jamhuri kwenye kesi ya Mbowe?
Kwanini kesi ya Sabaya inaendeshwa kwa kasi sana? Mwanzoni ilikua inasikilizwa baada ya wiki mbili, lakini kwa sasa inasikilizwa kila siku? Kuna watuhumiwa wangapi ambao ushahidi umekamilika lakini kesi zao hazipelekwi kwa kasi kama ya Sabaya? Kwanini Hakimu alibadilishwa? Kwanini tuhuma za Sabaya kwa Mbowe zinapewa uzito sana kwa sasa?
Halafu kwa mujibu wa sheria ya ugaidi no.21 ya mwaka 2002, kifungu cha 4 ugaidi unahusisha halaiki ya watu sio mtu mmoja. Yani ukiua mtu mmoja hayo ni mauaji na utashtakiwa kwa maujai (murder), lakini ukiua halaiki ya watu huo ni ugaidi na utashtakiwa kwa ugaidi (terrorism). Sasa imekuaje tuhuma za kupanga kumuua Sabaya (mtu mmoja) ziitwe ugaidi?
Mimi nadhani Rais Samia amshauri DPP kuiondoa hii kesi mahakamani. Wala haitakua kuingilia uhuru wa mahakama. Rais Samia aliwahi kumshauri DPP kaziondoa mahakamani kesi za "kubambikia" na wala hakuonekana anaingilia uhuru wa mahakama. So anaweza kushauri kwa hii ya Mbowe pia.
Hii ni kwa sababu kesi hii inachafua sana serikali ya Samia, kitaifa na kimataifa. Kesi hii imemuondolea heshima yote aliyoijenga kwa siku 100 za kwanza. Hata wawekezaji watapungua kwa sababu hakuna mtu atakayekua tayari kurisk mtaji wake kuwekeza nchi yenye ugaidi. Hata wafadhili watapunguza misaada kwa sababu hakuna mtu anataka kufadhili nchi yenye ugaidi.
Kwahiyo Rais Samia anaweza kumshauri DPP kuifuta hii kesi kwa maslahi mapana ya serikali yake, maslahi mapana ya nchi yetu, na maslahi mapana ya demokrasia nchini.
Na hatakua wa kwanza kufanya hivyo. Mwaka 1970 Bibi Titi Mohamed na wenzake walifungwa gerezani kifungo cha maisha kwa tuhuma za uhaini. Kumbuka Bibi Titi ni mmoja wa watu waliopigania uhuru wa nchi hii, na ni Waziri wa kwanza mwanamke.
Watu wenye hekima wakamfuata Mwalimu Nyerere na kumwambia, athari za kumfunga bibi Titi ni kubwa kuliko za kumuachia huru. Kumuweka jela kunaiharibia zaidi serikali yako. Ukimuachia huru atakayefaidika zaidi ni wewe na serikali yako sio yeye. Nyerere akaelewa na mwaka 1971 akamuachia huru.
The same applies kwa kesi ya Mbowe. Ikiwa DPP ataamua kuifuta hii kesi, atakayenufaika zaidi ni Samia na serikali yake, si Mbowe wala Chadema.
Hata hivyo Samia ana uhuru wa kusuka au kunyoa. Kesi iendelee kusikilizwa na yeye aendelee kuchafuka na kujifungia fursa za wawekezaji (hata kama Mbowe atashinda) au amshauri DPP kuifuta kesi, apate heshima ya kufanya maridhiano ya kisiasa, na historia imkumbuke kama mama shujaa wa demokrasia. Kupanga ni kuchagua.!