Eti Mbowe alitoa laki 6 kufadhili ugaidi. Seriously?

Eti Mbowe alitoa laki 6 kufadhili ugaidi. Seriously?

Gaidi alitaka kuchoma vituo vya mafuta tokea mwaka jana, wakamuacha tu azurure mwaka mzima. Leo tunaambiwa amefikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya uhujumu uchumi...

Tundu Lissu kasiliba yote. Kasema hiyo wala siyo kesi bali ni ujinga mtupu na ndiyo uwezo na picha halisi ya prosecution system ya Tanzania.

 
Kweli tutayaona mengi, kiasi cha dollar 250 kufadhili ugaidi? Hata hazifiki 10% ya zile mbunge wa zamani wa Muleba aliita hela ya mboga.
 
Hiyo laki sita mbona nyingi Kuna wale wanaojilipua wa imani Kali hupewa tu nauli ya daladala kuwafikisha eneo la kujilipua na mabomu

Kufadhili ugaidi si mamilioni ya hela waweza tu lipia tu shilingi Mia tatu ya nauli ya daladala ukadakwa kwa kufadhili ugaidi
 
Mbowe's Dog... naona mmeanza kubweka. Wapi imeelezwa kwamba Bajeti ya mbowe kufadhili ugaidi ni laki 6 kwa mwaka? Mbona Sabaya alivyoambiwa ameiba simu ya techno mliona inawezekana?...
Mahakama ipi?

Kwa mashaidi hao unajiaminisha kwa hao waliotajwa?

hata kama wangekuwepo mashaidi 1000 subiri uone hapo kwenye maswali ndipo tutarudi kule

Wakili kibatala swali: Tuambie elimu ya yako Criminal investigation & terrorist attack?

Shaihidi: Nilisoma Secondary ya Uchama Nzega, baada ya kumaliza nilienda........
 
20210824_084848.jpg
 
Kabla ya Mbowe kusomewa mashtaka, watu waliipa Jamhuri "benefit of doubt" kwamba huenda ina ushahidi wa maana. Watu wakahisi labda Mbowe ana uhusiano na makundi ya kigaidi kama Al Shabab, Al Queda, Boko Haram etc na pengine anapeleka vijana huko kwa ajili ya mafunzo...

Tuache kunanga kiasi hicho cha fedha kinachoelezwa kutumiwa na Mbowe kufadhili ugaidi. Eti ni kidogo kwa ugaidi. Jambo la ajabu sana. Kuna mahali nililazimika kumuuliza mshabiki mmoja wa Mbowe kuwa nyumba anayokaa inahitaji dumu la petroli na kiberiti cha shilingi ngapi ili kuungua na kumteketeza na familia yake?

Filling stations zinahitaji mafuta na viberiti vya shilingi ngapi ili kulipuliwa? Yaani inashangaza mtu mzima tena wengine wasomi kabisa wanahoji impact ya laki sita kwenye ugaidi! Hawajui kuwa tendo la ugaidi liko zaidi katika ushawishi kwa nafsi ya mtu kuliko hata pesa.

Kuna vijana wanashawishiwa kufanya ugaidi ikiwemo kujilipua na mabomu bila hata kupewa senti tano. Wakati mwingine hata hayo mabomu wanajitengenezea wenyewe bila kupewa fedha. Hivyo hoja ya kupima ugaidi wa Mbowe kwa ulinganifu wa pesa ni hoja ya kitoto sana. Ni hoja ya isiyoweza kumwepusha Mbowe na hukumu ya miaka 20 jela ikiwa mahakama itamkuta na hatia.

Mbowe angeweza kushtakiwa kwa kosa la ku- facilitate ugaidi bila hata kutoa pesa yoyote. Brain wash tu inatosha. Nawasihi watanzania tujiepushe na matendo yoyote ya kigaidi kama aliyofanya Mbowe.
 
UPUUZI MTUPU hakuna kesi hapa zaidi ya kesi FAKE.
Tuache kunanga kiasi hicho cha fedha kinachoelezwa kutumiwa na Mbowe kufadhili ugaidi. Eti ni kidogo kwa ugaidi. Jambo la ajabu sana. Kuna mahali nililazimika kumuuliza mshabiki mmoja wa Mbowe kuwa nyumba anayokaa inahitaji dumu la petroli na kiberiti cha shilingi ngapi ili kuungua na kumteketeza na familia yake?..
 
UPUUZI MTUPU hakuna kesi hapa zaidi ya kesi FAKE.
Ndiyo mnachokosea Chadema. Badala ya kujibu hoja za msingi, mnaishiaga tu kutukana. Mvua 30 zinamhusu gaidi Mbowe. Endeleeni tu kusema ni kesi fake.
 
Kabla ya Mbowe kusomewa mashtaka, watu waliipa Jamhuri "benefit of doubt" kwamba huenda ina ushahidi wa maana. Watu wakahisi labda Mbowe ana uhusiano na makundi ya kigaidi kama Al Shabab, Al Queda, Boko Haram etc na pengine anapeleka vijana huko kwa ajili ya mafunzo...
NIsaidieni. Alitoa laki sita kufadhiri ugaidi upi? Hao magaidi aliokuwa anayafadhiri ni akina nani? Kesi yao ya ugaidi iliendeshwa lini? Ni ugaidi upi hasa? hapo bado niko nje, naomba mnijumuishe ili niweze kuchangia.
 
Hakuna hoja ya msingi kuhusu hii Serikali iliyopo madarakani kiharamu.

Ndiyo mnachokosea Chadema. Badala ya kujibu hoja za msingi, mnaishiaga tu kutukana. Mvua 30 zinamhusu gaidi Mbowe. Endeleeni tu kusema ni kesi fake.
 
Nacheka kama mazuri vileeeee... Kwahiyo mfadhili wa ugaidi aliweka mpunga wa 600,000 ili magaidi kutekeleza mauaji ya viongozi , sababu walisema viongozi hivyo ni zaidi ya mmoja... Katika hiyohiyo kuna na uchomaji wa vituo vya mafuta.... Hivi waligawana shilingi ngapi??

Mimi nafikiri kuna typing error... Badala ya 600,000,000 mchapaji kaweka 600,000= sababu kwa 600,000 hata kwa mmoja bado haifikiriki....
 
Duh! 600,000/= u home kituo cha mafuta and risk your livelihood,duh! Haijaingia kichwani bado
 
Mkuu fanyeni upuuzi woooooooooooooote lakini hili la ukabila achaneni nalo kwani kila mtu atakuwa mhanga maana kila mtu ana kabila lake. Hii ni sawa na kuchoma nyumba ambayo uko ndani yake.
Weye una akili Sana naunga mkono hoja yako
 
Mbowe lazima afungwe, naona mwanaharakati wa kichagga anamtetea mchagga mwenzake aliyeanzisha chama chakuwatetea wachagga Tanzania, mashahidi na mawakili wengi kwenye kesi ya Sabaya ndio nyie nyie, inatia mashaka.

Muangalie huyo wakili anamsimamia Sabaya koa mpaka dactari aliyekuja kutoa ushahidi mahakamani. Duh! Laana ya ukabila mbaya sana
sidhani kama hii issue ni kuhusu kabila. sioni relation ya kabila hapa zaidi ya interest za kisiasa.

Mwanachama yoyote wa chadema tegardless kabila lake .. ukiongea nae atakuambia mbowe si gaid.. wao wanamtetea kama mwenyekiti wao.. si mkuu wa kabila.
 
Hiyo laki sita mbona nyingi Kuna wale wanaojilipua wa imani Kali hupewa tu nauli ya daladala kuwafikisha eneo la kujilipua na mabomu

Kufadhili ugaidi si mamilioni ya hela waweza tu lipia tu shilingi Mia tatu ya nauli ya daladala ukadakwa kwa kufadhili ugaidi
Acha bangi mkuu
 
Huyu Malisa aunganishwe kwenye tuhuma za Mbowe haraka anaonekana anajua mengi

USSR

Sema hivi Malisa ana uwezo mkubwa wa kutumia ubongo wake aliopewa na Mungu....Hebu fikiria kijana kama huyu angepewa nafasi ya kuongoza taifa hili jamii ingefaidika kwa kiasi gani na uwezo wake mkubwa?

Huko Facebook anavyojitoa na kuchangisha michango kusaidia wenye shida na mambo mengi tuu sijui ni kwa nini hatuna mfumo wa kuwapa nishani au tuzo raia wema kama hawa.

Tunasubiri marais wa nchi zingine wamteue awe mshauri wa rais kama ilivyokuwa kwa Mo (huku kwetu tulimteka nyara Haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa Daaaaah).
 
Back
Top Bottom