Hivyo ndivyo inavyotakiwa kuwa?Serikali ipo tayari kutoa ruzuku kwenye mafuta ya diesel/petrol lakini siyo mafuta ya taa,inaweza kupunguza pension kutoka 50% hadi 33% na siyo kuongeza kuwa 51-75% au 100% kwa kisingizio cha uhimilivu Wa mifuko badala ya kuipa mifuko hiyo ruzuku ili kuwaendeleza watumishi waliotumika hadi wakazeeka.
CCM hawawezi kumhurumia Mtanzania yeyote asiye mwanachama pendwa Wa chama chao.
Uongozi wa kiwanda cha mbolea ya Minjingu (Minjingu Mines and Fertilizer Ltd) Kinaendelea na Utoaji elimu kwa wakulima na umma wa watanzania juu ya ubora na umuhimu wa mbolea hiyo ya kupandia. Minjingu ni mbolea asilia ya kupandia. Mbolea hii inatokana na miamba inayochimbwa katika eneo la Minjingu mkoani Manyara ambayo husagwa na kufungashwa kwenye kiwanda kilichojengwa katika eneo hilo. Mbolea ya Minjingu ina kirutubisho cha mimea aina ya fosiforasi kati ya asilimia 12.3-13.2. Tofauti na mbolea nyingine za kupandia zenye madini ya fosiforasi kama vile TSP na DAP ambazo huagizwa nje ya nchi hivyo kugharimu fedha nyingi za kigeni, mbolea hii inayopatikana hapa nchini bei yake ni nafuu.