Ewe jobless usijione mnyonge au kukosa furaha, ndugu zako tuko hapa

je chama kina faa na kina umuhimu??

  • Total voters
    139
KAULI YA SEMAJI LA CHAMAAAA CHA MAJOBLESS PROMAX.

Ndugu watanzania napenda kuwa hints chache juu ya chama hiki!

Rai yetu na sera yetu ni hii; Upendo, Ushirikiano na Umoja!

Chama hiki Hakina michango na chama hiki si kikundi Cha waasi Bali vijana ambao ni jobless wenye maumivu na hasira yenye mateso yalitokana na ukosefu wa kazi, ajira na fursa!

Hiki ni chama ambacho wanachama wake hawana wajomba, kaka au dada na wazazi matajiri ... Bali hiki ni chama ambacho wanachama mmoja mmoja ndio nguzo na tegemeo la familia zao!

Katika chama hiki wapo waliopata depression kutokana na u jobless wa muda mrefu! Ndio maana sera yetu ni kutiana moyo, kuombeana na ikiwezekana kupeana fursa!

Katika chama hiki wapo waliopoteza wapenzi na watu wao wa karibu kisa tu walionekana hawana mwelekeo wa maisha kwa sababu tu ni majobless!

Hiki si Chama Cha mazwazwa ni chama kilicho na wanachama wenye vipawa, Elimu, ndoto kubwa ambao hawana tu nafasi ya kuvionyesha na kutumia vipawa, karama, Elimu na ndoto walizo nazo!

Mimi kama semaji wa CHAMA hili chini ya uwongozi thabiti wa Rais wa majobless promax Intelligent businessman pamoja na Makamu wake Bolotoba na katibu mkuu wa CHAMA ndugu min -me

Tunawakaribisha sana!

Kumbekeni hatutarudi nyuma! Wala kuacha chama hiki kife kwa sababu Cha kundi dogo la watu wenye fikra finyu na wenye mtazamo hasi na wenye Giza!

Tutavumilia matusi na Spana zetu kwani sisi katika chama hiki tunatambua kuwa

HAKUNA MWANADAMU MKAMILIFU ILA TU WANATOFAUTINA UWAFADHALI

Kidumu chama

Semaji .. samaleko
 
Nakubaliana na wewe Kwa kiasi flan, lakini mtu ulipe Kodi, msosi, bills ya maji, umeme, usafi etc afu useme huyo mtu ni jobless?
Mkuuu watu wengi ni jobless ... Mimi msemaji wa CHAMA hiki ni jobless hakika

Samaleko
 
Nadhani hiki chama ndio chenye sera nzuri kuliko vyama vyote vilivyopo humu ndani... Kina mlengo chanya.
 
Nakubaliana na wewe Kwa kiasi flan, lakini mtu ulipe Kodi, msosi, bills ya maji, umeme, usafi etc afu useme huyo mtu ni jobless?
mkuu hapo ni surviving mode, Leo hii tuki kurupushwa.

wenye akiba ya elfu 50 ndani, I swear una weza cheka au shangaa.
 
Nadhani hiki chama ndio chenye sera nzuri kuliko vyama vyote vilivyopo humu ndani... Kina mlengo chanya.
Hakika Mkuu! Ni chama sahihi sana.
Sisi viongozi wandaamizi tumeitoa mioyo yetu kwa ajili ya wengine!

Hatuna utajiri wa kuwapa majobless wengine ila tunaweza kutiana moyo, kubebana katika yenye uwezekano!

Kuna furaha kiasi Gani kuona Kijana wenzako anateseka na kuumia hata kufikia hatua ya kuiba au kujiua? Ungali unaweza kumtia moyo na akasonga mbele!

Tunaamini katika Uwepo wa Mungu, semaji la chama ataanza kufunga na kuwaombea majobless ambao ni wanachama kila ijumaa!

Samaleko
 
Tanzania ina ardhi ya kutosha,mvua zinanyesha rasilimali chungu mzima unawezaje kuwa jobless? Tuache utani bwanaaa
Ujobless uko na maana Pana mkuu, kwa jinsi ulivyouliza nadhani unahisi watu wakisema majobless ni kwamba hawana kazi za kufanya... Kuchulia jobless ni mtu ambae Hana mshahara, chukulia jobless ni mtu ambae mshahara haukidhi mahitaji, chukulia jobless ni kijana anaejitafuta kwenye biashara lakini haina muendelezo wa kudumu (watu wa Dar waliambiwa waache kuuza uduvi na mkuu wa mkoa wao)

Ndugu Katibu min -me aliniambia hapo juu kwamba hata mkulima ambae anawekeza nguvu zake shamba lakini Hana uhakika na mavuno, kwasababu kilimo ni probability so mvua isiponyesha kwa namna ile inavyotakiwa nguvu zinaweza kwenda bure, huyu nae ni jobless. Na kadhalika na kadhalika.
 
Hakika Mkuu! Ni chama sahihi sana.
Sisi viongozi wandaamizi tumeitoa mioyo yetu kwa ajili ya wengine!

Hatuna utajiri wa kuwapa majobless wengine ila tunaweza kutiana moyo, kubebana katika yenye uwezekano!

Kuna furaha kiasi Gani kuona Kijana wenzako anateseka na kuumia hata kufikia hatua ya kuiba au kujiua? Ungali unaweza kumtia moyo na akasonga mbele!

Tunaamini katika Uwepo wa Mungu, semaji la chama ataanza kufunga na kuwaombea majobless ambao ni wanachama kila ijumaa!

Samaleko
Hii imekaa vizuri, ila msemaji naomba useme neno kwa mtu ambae alikua jobless jana akajiunga na chama halafu kesho yake akapata kazi ambayo kwa tathmin yake na kwa vigezo vyake inaonekana si kazi ya kijobless, vipi atatimuliwa kwenye chama au 😂😂😂😂
 
Jambo Moja katika chama hiki tunachojivunia ni Uwepo wa Katiba.

Katina ya chama inasemaje? Sheria namba kumi ibara ya 8

Nanukuu

"Endapo mwanachama wa CHAMA hiki atapata kazi yenye kumpa uhuru wa kiuchumi na maendeleo Binafsi, chama hakitamtambua kama ni jobless Bali Bado atakuwa na nafasi katika chama ex-jobless person huku akiwa na Haki za kutoa ushauri, kushiriki shughuli zote za chama kwani mtu huyu anaweza kuwainua wengine kwa connection, fursa hata pengine kuelezea experience yake ambayo itawatia moyo wanachama wapya"
 
Hii imekaa vizuri sana... Kumbe na katiba ipo bhana.
 
TUANZIE HAPA
Ili mtu kuwa jobless inabidi asimiliki nini?
Chama chetu kina sera na Katiba!

Chama Cha Majobless hakikumbatii u jobless kama vazi la kuringia!

Chama Cha hiki ni chama chenye muono chanya ambacho kinaamini kuwa u jobless unaweza kuwa ni hatua Moja kabla ya kufikia mafanikio au uhuru wa kiuchumi!

Hivyo Katiba ya Chama hili, Sheria ya 4 ibara ya Tisa inasema;

Nanukuu

"Ili mtu aweze kuwa mwanachama Cha Cha hiki, sharti awe ni mtu asiyekuwa na kazi, ajira, au shughuli yoyote ramsi ya kumuingizia kipatao.

Kwa sababu hili litatusaidia kujua status ya mwanachama na endapo kutatokea fursa yoyote aweze kunufaika nayo"

Hivyo kikubwa uwe una miliki roho na mwili maana yake uwe kiumbe hai!

Kanuni ndogo ya chama inapinga vikali mtu mwenye uwezo na fursa au uhuru wa kiuchumi kuingia katika chama hiki ili kunufaika na chama!

Japo Katiba inaruhusu mtu kujiunga na chama hata kama si jobless kulingana na masharti na matakwa ya Katiba ya Chama!

Samaleko
 
Back
Top Bottom