Salam, Shalom!!
Ni Kweli, Yesu alituagiza kuwa "Tusiache kukusanyika" wapi alisema tukusanyike Jumapili?
Ibada na kutafakari neno la Mungu ni muda wote, mchana na usiku,
Na Ibada Takatifu ni Ile ifanyikayo katika Roho na Kweli.
Na Mungu hufanya KAZI muda wote, hata sasa afanya KAZI.
Mungu anakuuliza Ewe Mkristo kupitia thread hii, ni nani aliyekwambia kukusanyika Jumapili Kwa ibada takatifu?
Ukiulizwa andiko utalitoa wapi?
Ni nani aliyekuagiza kusherehekea sikukuu ya Christmas tarehe 25 December?
Unalo andiko? Ni maagizo ya Roho mtakatifu kufanya mambo hayo?
NB: Mkristo aulizwaye swali hili ni yule aliyeokoka, aliyebatizwa Kwa maji mengi na Kwa Moto wa Roho Mtakatifu, yule aaminiye juu ya karama Tano, unabii ukiwemo, aaminiye juu ya kunena Kwa lugha, aliyefunguliwa macho ya Rohoni na kuisikia sauti ya Roho mtakatifu wazi WAZI.
ANGALIZO; Hii Si mada kuhusu Ukristo kama DINI, Bali Ukristo kama IMANI juu ya Yesu Kristo na maisha matakatifu.
Karibuni.[emoji120]