3 Angels message
JF-Expert Member
- Aug 3, 2017
- 5,350
- 15,426
Unaposema ibada za kikristo maana yake nini?Ibada zipo toka enzi na enzi! Mada hapa ni ibada za kikristo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unaposema ibada za kikristo maana yake nini?Ibada zipo toka enzi na enzi! Mada hapa ni ibada za kikristo.
Kwa hiyo ukiweka akiba tayari imekuwa siku ya ibada?1 Kor 16:2
Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja
Siku ya kwanza na siku ya saba zote ni takatifu..Salam, Shalom!!
Ni Kweli, Yesu alituagiza kuwa "Tusiache kukusanyika" wapi alisema tukusanyike Jumapili?
Ibada na kutafakari neno la Mungu ni muda wote, mchana na usiku,
Na Ibada Takatifu ni Ile ifanyikayo katika Roho na Kweli.
Na Mungu hufanya KAZI muda wote, hata sasa afanya KAZI.
Mungu anakuuliza Ewe Mkristo kupitia thread hii, ni nani aliyekwambia kukusanyika Jumapili Kwa ibada takatifu?
Ukiulizwa andiko utalitoa wapi?
Ni nani aliyekuagiza kusherehekea sikukuu ya Christmas tarehe 25 December?
Unalo andiko? Ni maagizo ya Roho mtakatifu kufanya mambo hayo?
NB: Mkristo aulizwaye swali hili ni yule aliyeokoka, aliyebatizwa Kwa maji mengi na Kwa Moto wa Roho Mtakatifu, yule aaminiye juu ya karama Tano, unabii ukiwemo, aaminiye juu ya kunena Kwa lugha, aliyefunguliwa macho ya Rohoni na kuisikia sauti ya Roho mtakatifu wazi WAZI.
ANGALIZO; Hii Si mada kuhusu Ukristo kama DINI, Bali Ukristo kama IMANI juu ya Yesu Kristo na maisha matakatifu.
Karibuni.🙏
Sabato ya siku ya kwanza ya Juma, maana yake ni Pumziko.(Mambo ya walawi 23:7) Si siku ya kwanza ya juma, ni siku ya kwanza ya mwezi wa pasaka.
Hivyo siku kuu ya kukusanyika wakristo Bado ni siku ya Saba ya juma hata sasa yaani Jumamosi.
Ibada na kuabudu ni Imani ya Mtu. Wewe Baki na Imani yako na Fanya unachaomini. Hata wakikusanyika Kila siku wewe inakuhusu Nini? Fanya Yako kivyako.Salam, Shalom!!
Ni Kweli, Yesu alituagiza kuwa "Tusiache kukusanyika" wapi alisema tukusanyike Jumapili?
Ibada na kutafakari neno la Mungu ni muda wote, mchana na usiku,
Na Ibada Takatifu ni Ile ifanyikayo katika Roho na Kweli.
Na Mungu hufanya KAZI muda wote, hata sasa afanya KAZI.
Mungu anakuuliza Ewe Mkristo kupitia thread hii, ni nani aliyekwambia kukusanyika Jumapili Kwa ibada takatifu?
Ukiulizwa andiko utalitoa wapi?
Ni nani aliyekuagiza kusherehekea sikukuu ya Christmas tarehe 25 December?
Unalo andiko? Ni maagizo ya Roho mtakatifu kufanya mambo hayo?
NB: Mkristo aulizwaye swali hili ni yule aliyeokoka, aliyebatizwa Kwa maji mengi na Kwa Moto wa Roho Mtakatifu, yule aaminiye juu ya karama Tano, unabii ukiwemo, aaminiye juu ya kunena Kwa lugha, aliyefunguliwa macho ya Rohoni na kuisikia sauti ya Roho mtakatifu wazi WAZI.
ANGALIZO; Hii Si mada kuhusu Ukristo kama DINI, Bali Ukristo kama IMANI juu ya Yesu Kristo na maisha matakatifu.
Karibuni.🙏
Weka Andiko Brother.Kumbuka siku ya 7 na kuitakasa,kuitakasa means kuitenga + msiache kukusanyika+ plus akawafanya wengine kuwa wachungaji,wainjilisti,maskofu nk[ikumbuke siku ya Saba na kuitakasa ,tangu Wana wa Israel walipopewa Iyo amri kule jangwa ilianza kufanya kazi ,walikuwa wanaita hema ya kukutania,walipofika kanaan ikaitwa hekalu na wahudumu wake walikuwa wanaitwa makuhani, lakin yesu akawabadili vyeo wakaitwa wengine wachungaji,wengine wainjilisti ,na maaskofu ,yesu akajua watakuja watu wenye Sera kama yakwako akasema msiache kukutanika } zile amri 10 zinasimama mpaka Leo maanake kama kipindi kile walikuwa wanakutanika siku ya Saba kwenye hema ya kukutania, hekaluni, kwa nini Leo ibadilike alijua technolojia itakuja na shetani atakuja na Sera zake kwamba watu wabaki nyumbani waangalie kwenye TV,Ndo maana alisema msiache kukutanika na vile hakutaja mahali bhasi tujue Sera yeyote au mpango wowote wa kutaka tusikutanike popote tunapotakiwa kukutanika kwa mambo ya mungu tusikubaliane nacho.
Kumega mkate, ni Ibada za nyumba Kwa nyumba,Matendo 20:7 . Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana kumega mkate, Paulo akasema nao...
Kutokufungwa na SHERIA ndo kubadili siku kuu ya kukusanyika Kwa Ibada Kutoka Siku ya Saba ya juma (Jumamosi) kwenda siku ya Kwanza ya juma (jumapili)?Waroma10:4 "Kwamaana Kristo ndiyo mwisho wa Sheria ili Kila mtu aliye na Imani awe na uasilifu". Wakolosai2:16,17 "Kwa hiyo,msimruhusu mtu yeyote awahukumu kuhusu mnachokula na kunywa au kuhusu kushika sherehe au mwezi mpya au sabato,17 mambo hayo ni kivuli Cha mambo yanayokuja,bali uhalisia ni wa Kristo. Agano la zamani la Sheria ambalo Mungu aliwapa kupitia Musa lilifika mwisho wake wakati kifo Cha Yesu kilipotimiza agano Hilo.Waefeso2:15"Kupitia mwili wake alifuta uadui,ILE SHERIA ILIYOKUWA NA AMRI NA MAAGIZO ,ili afanye vile vikundi viwili katika muungano na yeye mwenyewe viwe mtu mmoja mpya na kufanya amani. Kwa kuongezea wakristo hawapo chini ya SHERIA ya MuSa tena Bali chini ya SHERIA ya Kristo,wagalatia6:2.
Amri ipi imeandikwa siku kuu ya kukusanyika Kwa Ibada takatifu ni Jumapili?S
Soma amri kumi za Mungu utaona Hilo agizo
Kwamba hujui siku ya kwanza ya juma ni Jumapili?Kwa calenda ipi Sasa,
Hii tunayotumia kwa Sasa Duniani ilianzishwa na Wakatoliki
boss kula ushibe hii mada imekaa Kirobot robotMungu hapumziki? Una hakika?
Umeongea sahihi, siku yoyote mnaweza kukusanyika,Siku zote ni za kumsifu na kumwabudu Mungu, Matendo2:46-47
Mungu anachotaka ni Kumwabudu katika Roho na Kweli, kwa maana Yeye ni Roho, Yohana4:23-24
Haijalishi Kanisa linakusanyika siku gani.
Nimalize kwa kukuliza sasa! Katika Agano Jipya ni Wapi ambapo Yesu aliliagiza Kanisa kukusanyika siku fulani?
Usisahau, Kusanyiko la kwanza la Kanisa, baada ya Yesu kupaa lilifanyika siku ya Jumapili, Matendo2:1-11.
Ni nani aliyebadili siku kuu ya kukusanyika Kwa Ibada takatifu Kutoka Siku ya Saba ya juma jumamosi kwenda siku ya kwanza ya juma (jumapili)?Mwisho wa Dunia umefika rasmi !
Ubarikiwe sana mkuu...yaani umetema point tupuSabato ya siku ya kwanza ya Juma, maana yake ni Pumziko.
Hivyo Waisraeli waliamriwa kupumzika tu siku hiyo. Na kustarehe kabisa wao na wageni wao.
Kumbukumbu la Torati 5
12 Ishike siku ya Sabato uitakase, kama Bwana, Mungu wako, alivyokuamuru.
13 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
14 lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako; siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala ng'ombe wako, wala punda wako, wala mnyama wako ye yote, wala mgeni aliye ndani ya malango yako, ili mtumwa wako na mjakazi wako wapumzike vile vile kama wewe.
15 Nawe utakumbuka ya kuwa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, na ya kuwa Bwana, Mungu wako, alikutoa huko kwa mkono wenye nguvu, na mkono ulionyoshwa; kwa sababu hiyo Bwana, Mungu wako, alikuamuru uishike sabato.
(Hakuna Neno Ibada hapo)
Kutoka 20
8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
10 lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
11 Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
(Hakuna Neno Ibada hapo)
Mambo ya Walawi 23
3 Mtafanya kazi siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, kusanyiko takatifu; msifanye kazi ya namna yo yote; ni Sabato kwa Bwana katika makao yenu yote.
( Hakuna Neno Ibada hapo)
Sabato maana yake ni kupumzika na kustarehe Kama maandiko yanavyosema.
Wewe kufanya Ibada siku ya Sabato ya mwanzo wa Juma umeambiwa wapi ?
Kama siku kuu za Makusanyiko Matakatifu za Bwana zipo nyingi na sio siku moja ya Sabato ya mwisho wa Juma pekee, kama unavyo sema.
Mambo ya Walawi 23
4 Sikukuu za Bwana ni hizi, ni makusanyiko matakatifu, ambayo mtayapigia mbiu kwa nyakati zake.
(endelea kuzisoma)
Nasubiri andiko linalosema ufanye Ibada siku moja tu, Siku ya saba ya Juma, Sabato)
Warumi 14:4-5Salam, Shalom!!
Ni Kweli, Yesu alituagiza kuwa "Tusiache kukusanyika" wapi alisema tukusanyike Jumapili kama siku kuu ya IBADA badala ya Jumamosi iliyovyokuwa awali?
Mtakufa na madini yenu ya kishetaniSalam, Shalom!!
Ni Kweli, Yesu alituagiza kuwa "Tusiache kukusanyika" wapi alisema tukusanyike Jumapili kama siku kuu ya IBADA badala ya Jumamosi iliyovyokuwa awali?
Ibada na kutafakari neno la Mungu ni muda wote, mchana na usiku,
Na Ibada Takatifu ni Ile ifanyikayo katika Roho na Kweli.
Na Mungu hufanya KAZI muda wote, hata sasa afanya KAZI.
Mungu anakuuliza Ewe Mkristo kupitia thread hii, ni nani aliyekwambia kukusanyika Jumapili kama siku kuu ya ibada takatifu badala ya Jumamosi?
Ukiulizwa andiko utalitoa wapi?
Ni nani aliyebadili siku kuu ya kukusanyika Kwa Ibada Kutoka Siku ya Saba ya juma, kwenda siku ya kwanza ya juma,jumapili?