Ewe Mkristo, nani alikwambia kukusanyika kila Jumapili kwa ajili ya Ibada?

Ubarikiwe sana mkuu...yaani umetema point tupu
Huyo ni Msabato, maana yake ni mtu wa kupumzika na kustarehe siku ya Saba ya Juma.

Hili andiko anawalenga Kanisa Katoriki.

Nabii wao Allen G. White, alianzisha kanisa la Sabato kwa lengo la kuwakosoa Wakatoriki kuhusu kufanya Ibada siku ya Jumapili.

Mwisho wake Wasabato wanaendeleza mafundisho ya chuki dhidi ya Wakatoriki badala ya kuhubiri msamaha wa dhambi na wokovu kwa jina la Kristo.

Ukikutana na Msabato kitu cha kwanza kukuuliza ni "je unaabudu Jumamosi?

Ukimjibu ndio naabudu Jumamosi, kwake wewe ni Mtakatifu hata kama ni mchawi mlozi.

Matokeo yake wamejikuta wanaiabudu siku ya Jumamosi, badala ya kuitumia kupumzika na kustarehe kama walivyo amriwa katika Amri Kumi za Musa.

Siku Jumamosi imekuwa ni Sanamu kwao.
Ellen White amewapoteza Mwelekeo
 
Yoh4:23 "waabuduo halisi watamwabudu Bwana kwa Roho na kweli".Waabuduo halisi sio wale wanao abudu kanisa fulani ,siku fulani ,Je unaabudu katika Roho na kweli alhamisi,Jumanne,jumamosi nk ,kama ndio wewe ni mwabudu halisi.wakolosai 2:16-17 "Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo".AGANO LA KALE NI KIVULI sasa tunaishi kwenye uhalisia tunaabudu siku yoyote,popote katika Roho
 
Unakosea sana, Mimi Si msabato,

Wasabato Si wakristo.

Soma NB: hapo juu, wasabato hawana sifa hizo hapo juu, maana hawaamini karama ya unabii,miujiza na kunena Kwa lugha.
 
Kama kuabudu Kwa Roho ni siku yoyote,

Kwanini dini na madhehebu yanakusanyika Jumapili kama siku kuu ya IBADA?

Ingekuwa Wengine Wanakusanyika Jumatatu, Jumanne, J5, Alhamis,Ijumaa nknk.

Why Jumapili madhehebu karibia yote?
 
Unakosea sana, Mimi Si msabato,

Wasabato Si wakristo.

Soma NB: hapo juu, wasabato hawana sifa hizo hapo juu, maana hawaamini karama ya unabii,miujiza na kunena Kwa lugha.
Warumi (Rom) 10:17
Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.

So then faith cometh by hearing, and hearing by the word of God.

(Msikilize Kristo
Wacha kumsikiliza Ellen G. White
Atakupoteza Mazima.)

Kristo anasema hivi

Ufunuo wa Yohana (Rev) 22:13
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.

I am Alpha and Omega, the beginning and the end, the first and the last.
 
Kama kuabudu Kwa Roho ni siku yoyote,

Kwanini dini na madhehebu yanakusanyika Jumapili kama siku kuu ya IBADA?

Ingekuwa Wengine Wanakusanyika Jumatatu, Jumanne, J5, Alhamis,Ijumaa nknk.

Why Jumapili madhehebu karibia yote?
Kukusanyika ni muhimu imeandikwa "msiache kukusanyika pamoja kama ilivyo desturi Ebrania 10:25" aijaandikwa tukusanyike jumapili tu ,jumamosi tu,ndio maana kuna madhehebu yamefunguka akili waamini wanasali kila siku asubuhi,wengine wanaibada za katikati ya week jumatano au alhamisi ,tuko kwenye uhalisia kuabudu ni swala la Rohoni jiwekee utaratibu heshimu na Mungu atauheshimu ,siku zote ni za Mungu ,yupo popote ,anajua yote.
 
Wasabato Si wakristo, hawaamini karama ya miujiza, kunena Kwa lugha, unabii nk nk.

So mm Si msabato, ni mkristo, na nimekuwa nikiabudu J2 kama siku kuu tangu mdogo,

Nw nikiwa na utimamu wangu, baada ya kuokoka muda mrefu sasa, ndipo Swali hili limekuja nikuulize mkristo mwenzangu!!

Ni nani aliyewaagiza kubadili siku kuu ya kukusanyika Kwa Ibada takatifu Kutoka Siku ya Saba ya juma yaani Jumamosi kwenda siku ya kwanza ya juma yaani Jumapili?
 
Nimekustahi kwakuwa umeanza na "shalom" amani!

Wewe ni mpuuzi ila ni mpumbavu ambaye unaweza kuelimishwa.

Hakuna mkristo anayesali/abudu jumapili peke yake labda [wakatoliki ] ila watu wanaomkiri Yesu kuwa bwana na mwokozi wao, watu wanao mwabudu Mungu baba bila kupitia watu ambao wanadamu wanawaita watakatifu kila siku wanasali, kila siku wanakutana kanisani for morning glory, mchana kuna ibada ya lunch hour, jioni kuna ibada ya jumatano, kuna ibada za ijumaa, kuna mikesha ya ijumaa na pia jumapili wanakutana.
 
Swali hili waliulizwa wananaombi walipokuwa mkesha Kanisani,

Mungu aliwashukia na kusikiwa sauti ikiwauliza, mmoja mmoja kuwa,

Ni nani aliwaagiza kuabudu Jumapili?

Tembelea UNYAKUO TV, Kuna huo ushuhuda.

Hivyo, Mungu anatutaka tuliookoka kurudi kuabudu Siku ya Saba ya juma kama siku kuu ya kukusanyika Badala ya Siku ya kwanza ya juma.

Amen
 
Nani kabadili mbona sisi tunakusanyika na kufanya Ibada siku zote ikiwepo Jumamosi ?

Wewe waulize Wakatoriki kama unavyo taka.

Sisi tunakusanyika siku zote za Juma na kufanya Ibada kwakuwa hayo makusanyiko ya Jumamosi tu hayakumpendeza Mungu.

Yeremia 31
31 Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.

32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana.

33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

34 Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wamriwa ao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.

Waulize Wakatori ni kwanini wanakusanyika Jumapili tu.

Na wewe kawaukulize Wasabato wenzako.
Nani aliwaambia mkusanyike siku ya mwisho ya Juma tu. Na kudharau makusanyiko mengine yaliyo amriwa katika Agano la Kale ?
 
Ni Lini Yesu Kristo alikuagiza mkristo kukusanyika jumapili Kwa ajili ya IBADA Takatifu?
Kama vipi wale watakaopenda kukusanyika jumatano kuanzia saa 3 asubuhi tukutane tufanye jambo[emoji23]
 
Sibishani nawe,

Swali hili alishuka Mungu na kuwauliza wananaombi wakristo usiku,

Tembelea UNYAKUO TV -Video inaenda Kwa Jina OLE.. MNAOTETEA JOKA LA JUMAPILI.

NI onyo Kwa waliookoka kulifanya jumapili kama siku kuu ya kukusanyika Kwa Ibada takatifu mbali na Ibada za katikati.

Pitia na isikize video hiyo Kisha rudi kucoment.
 
Shida ni Jumapili au shida ni nn?
Aliyebadili Kutoka Siku ya Saba ya juma yaani Jumamosi kwenda siku ya kwanza ya juma yaani Jumapili alikuwa na agenda Gani?

Na alipata idhini Kutoka Kwa MUNGU kupitia Roho MTAKATIFU au alijiamulia mwenyewe?
 
Shida ni Jumapili au shida ni nn?
Jumapili inawauma baadhi ya waarabu wa Tanzania kwakuwa ni mapumziko kutokwenda Kazini!

Katiba mpya itamke ijumaa ni mapumziko.

Katiba mpya pia itamke jumamosi ni mapumziko kwa wote maana ni sabato.

Katiba mpya itamke jumanne ni mpumziko ni siku ya wa Siloamu.

Tufanye kazi siku 3, zinatosha!
 
OLE..MNAOTETEA JOKA KUABUDU JUMAPILI-UNYAKUO TV.

Pitia video hiyo, Mungu mwenyewe alishuka, na kuuliza swali Hilo,

Hivyo waliookoka,Kanisa la kwanza kinatakiwa kurudi katika msingi wake na kuachana na maelekezo ya Constantine.

Amen
 
Umeeleza kwa usahihi kabisa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…