EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta kuanza kutumika 04/05/2022. Petroli na Dizeli bei juu zaidi

Tumeanza kumkuna bimkubwa, naona mambo yanazidi kuwa hovyo tu sasa. Yani ukiwa na 30k hupati lita kumi?

Ningekuwa na hela ningeweka mfumo wa gas wallah! This is absurd!
 
Tanzania inaenda kuwa Oligarchy state! Sahauni kuhusu demokrasia na utawala bora.
Namna pekee ya kujinasua ni kuanzisha strikes tu. Mabadiliko hayatakuja kwa kubembelezana na watawala.
 
Kimsingi mama katukabidhi buyu la asali 😅😅😅😅😅 yule kamanda waliemuita dikteta uchwara naona soon ataanza ki make sense!
 
Watakuita Sukuma Gang ila umepiga kwenye mshono 😅😅😅 JPM alikuwa raisi kwa wakati sahihi ambapo taifa lilimuhitaji!
Soon tutaongea lugha moja
 
Angekuwa Sio Samia bei isingepanda??!! Mafuta kupande bei hayana uhusiano na raisi wa sasa wala alieondoka...
Magufuli ange figure out cha kufanya ikibidi reserve zijengwe kama hamna. Hiki kilichotokea ni sabotage ya wafanyabiashara.

Tunaumizwa katika mtindo ule ule wa imposition of tozo.
 
UMEFUMUA MSHONO MKUU SASA MAUMIVU NI MAKALI SANA.
 
Watakuita Sukuma Gang ila umepiga kwenye mshono [emoji28][emoji28][emoji28] JPM alikuwa raisi kwa wakati sahihi ambapo taifa lilimuhitaji!
Soon tutaongea lugha moja
Hakika.

Kipindi cha JPM. Nlibahatika kukutana na Balozi wa nchi flani hapa Tz nyumbani kwake... Katikati ya maongezi Jamaa akasema; Rais mnaye sema tu hatokaa sana, Chuki ni Kubwa mno from outside.
 
Magufuli ange figure out cha kufanya ikibidi reserve zijengwe kama hamna. Hiki kilichotokea ni sabotage ya wafanyabiashara.

Tunaumizwa katika mtindo ule ule wa imposition of tozo.
Nakumbuka Muswada wa Tozo hata kabla ya kupelekwa kwake... Once when rumours has it, Mzee aliwaka kilimi akawaambia Wakunyonywa na Kukatwa hiyo Tozo sio Watanzania bali ni hawa Wezi wa Kizungu tutadeal nao mpaka wanyooke.

Zungu na wenzie wakaufyata. Mama alipoingia tu, wakapempelekea na Sasa tumeshazoea.

Hata Ushoga ulianzaga hivihivi huko nje mwisho wamezoea na kuona ni kawaida hata kufikia kudai haki zao mbalimbali.
 
Badala ya kutumia pesa kuagiza mafuta waweke reserve wajenge hata emergency reserve kwa dharula usiku na mchana wao hela wanatumia kufanya utalii angani..

Tutakukumbuka magufuli hakika ungekuwepo atleast bei ingekuwa himilivu.
Emergency reserve za serikali zipo. Ila wanahifadhia mafuta ambayo si ya serikali na hapo ndio utashangaa
 
Nafikiri suala la nchi kuwa na demokrasia halina relation na ishu ya bei.
Nchi inaweza ikawa ya kikomunist lakin kama viongozi wake ni vihiyo maisha yatakuwa gharama tu.

Sasa hapo ndio utash wa viongoz unatakiwa uonekane
 
Wengi mlishangilia uvamizi wa Putin Ukraine maana wabongo kila kitu wanafanya masihara sasa mnaanza kuonja athari za uvamizi. Na bei za mafuta zikipanda, bei za bidhaa na vyakula nazo zitapanda. Maana vyakula na bidhaa vinategemea mafuta kusafirishwa. Na bado msubiri bei za unga wa ngano na mikate zitapanda maana nazo zinaagizwa kutoka Ukraine na Urusi.
 
Sasa umetumia akili au umeona sources? Mimi kama ningeona source nisinge uliza lile swali sasa kutokea hapa baada ya kuona chanzo then naweza kutoa maoni yangu.
Thomaso una matatizo sana .... SI ufanye kwenda kituo Cha mafuta Cha jirani na ulipo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…