EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta kuanza kutumika 04/05/2022. Petroli na Dizeli bei juu zaidi

EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta kuanza kutumika 04/05/2022. Petroli na Dizeli bei juu zaidi

Tunalipia madhara ya vita!!...

Halafu kuna watu wanasifia Urusi kuvamia nchi nyingine....
Sio sababu kubwa sana,, ilaumu serikali yetu kuweka tozo Kibao kwenye mafuta haya ndo madhara yake!!

122F40D9-580D-4A7D-B77A-FFB85A0A412F.jpeg
 
Hata mapenzi yatapanda bei....!!!

Kuanzia ya kununua hadi ya halali kwa mke/mume.
 
Sio sababu kubwa sana,, ilaumu serikali yetu kuweka tozo Kibao kwenye mafuta haya ndo madhara yake!!

View attachment 2210544
Ni sahihi tozo ni kubwa. Ila zilikuwepo hata raisi aliepita..kumlaumu huyo sio sahihi. Ni muda wa kuangalia jinsi ya kufanya adjustment...Njia nzuri kwa nchi yetu kuleta nafuu ni Serikali kupunguza matumizi yake ili kupunguza pia baadhi ya kodi..Serikali ikiwa na matumizi makubwa hupelekea kila wakati kuongeza tozo na tozo za kujirudia.

Numbisa njoo uchangie jirani yangu.
 
Mafuta yamepanda tena Bei, Dar Lita ya petrol kuanzia kesho ni 3148, dizeli 3258

View attachment 2210381

Bei za mafuta kuanzia April 4, 2022

Bei ya petrol kwa Dar itakuwa ni Tsh 3,148 kwa lita. Kwa watu wa Tanga watanunua kwa Tsh 3,161 na kwa watu wa Mtwara kwa 3,177 kwa lita.

Dizeli itauzwa Tsh. 3,258 kwa lita kwa Dar, na kwa Tanga watanunua kwa Tsh. 3,264. Mtwara watauziwa kwa Tsh. 3,309 kwa lita.

Mafuta ya taa hayako nyuma ambapo bei ya lita kwa Dar itakuwa Tsh 3,112. Mikoa mingine itakuwa na bei kutokana na hesabu zitakvyofanyika.

EWURA wamesema mabadiliko ya bei katika soko la dunia yamesababisha 93% ya mabadiliko ya bei

Bei za Jumla
Port Petrol
(TZS/Litre)
Diesel
(TZS/Litre)
Kerosene
(TZS/Litre)
DAR ES SALAAM 3,015.88 3,125.18 2,980.56
TANGA 3,028.72 3,131.39 --
MTWARA 3,044.88 3,176.87 --

View attachment 2210436

View attachment 2210437

View attachment 2210438

View attachment 2210439

View attachment 2210440
Yapande tu. Mbona tunanunulia mademu Savanna moja@5,000/=? Hapo bado lodge, kondomu na UKIMWI unaweza kupata vile vile
 
Back
Top Bottom