EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta kuanza kutumika 04/05/2022. Petroli na Dizeli bei juu zaidi

EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta kuanza kutumika 04/05/2022. Petroli na Dizeli bei juu zaidi

Ni sahihi tozo ni kubwa. Ila zilikuwepo hata raisi aliepita..kumlaumu huyo sio sahihi. Ni muda wa kuangalia jinsi ya kufanya adjustment...Njia nzuri kwa nchi yetu kuleta nafuu ni Serikali kupunguza matumizi yake ili kupunguza pia baadhi ya kodi..Serikali ikiwa na matumizi makubwa hupelekea kila wakati kuongeza tozo na tozo za kujirudia.

Numbisa njoo uchangie jirani yangu.
Binafsi sizungumzii siasa hapa za uteam hapa nazungumzia hali halisi kama wanavyosema adui wa rafiki yako si adui wako hivyo hivyo hizi tozo kama ni za raisi aliyepita kama huzitaki kwann usiziondoe??
 
Mafuta bei juu, huku TARURA wakichanja parking fee hadi mtaani. Gari si asset tena

Cap-prices-wef-4-May-2022-English-2.jpg
 
Huyu Putin Mungu amlaani afe kifo cha kama babu yake Stalin. Katuletea dhiki sana duniani kwa ubabe wa kitoto na kishamba.
 
Chini ya Jiwe kivipi wote wale wale tu kwani huo mfumo wa ununiaji mafuta kwa bulk purchase si aliuleta yeye Magufuli,alitaka kila kitu ifanye Serikali.
Tena huyo Magufuli wenu ndio yangepaa mpaka 10,000.
Usimzungumzie Magufuli ujinga wa huyo bibi yenu! Magufuli alikuwa anapambania sana masrahi wa watu wa kawaida.Wewe na chuki zako za kipumbavu unataka kutuaminisha ujinga wa Samia ni sawa!
 
Ninamlaani Biden na wazungu kwa kuipatia Ukraine silaha. Hii vita ilipaswa kwisha ndani ya wiki moja.
Kwamba ukraine walitakiwa wapigwe tu huku wametulia? Yaani wasiji defend wala nini?
 
Huyu Putin Mungu amlaani afe kifo cha kama babu yake Stalin. Katuletea dhiki sana duniani kwa ubabe wa kitoto na kishamba.
Upande wa pili kuna faida kubwa iwapo tutajifunza katika hii shida. Kwanza, hatuna sababu ya kuagiza mafuta ya kula wakati tunaweza kuamua kuzalisha mafuta ya kula na ndani ya miaka 5 tukaacha kabisa kuagiza mafuta ya kula kutoka nje.

Serikali inaweza kuamua kwa makusudi kabisa kuuza miche ya chikichi kwa bei ndogo na hata kutoa bure. Kama iliweza kutoa mashamba ya kulima miwa ya sukari na ardhi ya kujenga kiwanda cha sukari kwa Bakhresa, inaweza kufanya hivyo kwa kampuni zinazozalisha mafuta ya kula. kwa makubaliano maalumu ili kuokoa bilioni mia kadhaa tunazotumia kuagiza mafuta ya kula.

Pia serikali inaweza kupunguza kodi ya kuingiza vifaa vinavyotumika kuweka mifumo ya gesi kwenye magari kwa Taasisi zake za DIT na VETA ili bei za kuweka hiyo mifumo zitelemke hata kwa 50% ili kuchochea matumizi ya gesi kwenye magari na kwa jinsi hiyo kulifanya shirika lake la TPDC kuchangia pakubwa katika kuongeza mapato ya serikali.

Vv
 
Kwamba ukraine walitakiwa wapigwe tu huku wametulia? Yaani wasiji defend wala nini?
Rais wa Ukraine ni fala tu, kutojiunga kwake na NATO kunampunguzia nini? Wasweden na Wafini wame-enjoy amani na Urusi kwa miaka mingi kwa sababu ya kutojiingiza kwenye mafungamani na NATO, leo wako roho juu kwa sababu ya kujiingiza kwenye mgogoro wa Russia vs Ukraine kwa kupeleka silaha Ukraine au kutaka kujiunga na NATO. Kupanga matumizi kwa kipato ambacho jirani ameahidi kukusaidia ni ujinga. Hao Marekani na wenzao wanachofanya ni kupeleka silaha tu kwa Ukraine ili vita iendelee wakati wao wako pembeni wanasubiri kuwapelekea ankara ya gharama za silaha mara vita vikiisha.

Ukraine wameingia gharama kubwa sana kwenye vita hii, kama wangechagua kubaki na msimamo wa awali hii vita isingekuwepo. Itawagharimu sana kuijenga upya miundimbinu yao na hakuna gharama ya kufidia uhai wa watu wao.

Vv
 
Alikuta sukari 1,500 kwa kilo
Kwa upuuzi wake akasababisha ikapanda hadi 3,500 over night
Hiyo sukari 3500 unaopata wali wewe fala? Walipopamdisha uliona Magufuli alichukua hatua gani? Ongelea huyo bibi yako! Vitu vyote vimepanda bei hata kabla ya vita ya Ukraine!
 
CDM mtanyooka safar hii, mlituchelewesha mnoo 😂😂😂😂😂NB: kazi iendeleeeee!!!
Mafuta yamepanda tena Bei, Dar Lita ya petrol kuanzia kesho ni 3148, dizeli 3258

Bei za mafuta kuanzia April 4, 2022

Bei ya petrol kwa Dar itakuwa ni Tsh 3,148 kwa lita. Kwa watu wa Tanga watanunua kwa Tsh 3,161 na kwa watu wa Mtwara kwa 3,177 kwa lita.

Dizeli itauzwa Tsh. 3,258 kwa lita kwa Dar, na kwa Tanga watanunua kwa Tsh. 3,264. Mtwara watauziwa kwa Tsh. 3,309 kwa lita.

Mafuta ya taa hayako nyuma ambapo bei ya lita kwa Dar itakuwa Tsh 3,112. Mikoa mingine itakuwa na bei kutokana na hesabu zitakvyofanyika.

EWURA wamesema mabadiliko ya bei katika soko la dunia yamesababisha 93% ya mabadiliko ya bei

Bei za Jumla
PortPetrol
(TZS/Litre)
Diesel
(TZS/Litre)
Kerosene
(TZS/Litre)
DAR ES SALAAM3,015.883,125.182,980.56
TANGA3,028.723,131.39--
MTWARA3,044.883,176.87--

View attachment 2210436

View attachment 2210437

View attachment 2210438

View attachment 2210439

View attachment 2210440
 
Binafsi sizungumzii siasa hapa za uteam hapa nazungumzia hali halisi kama wanavyosema adui wa rafiki yako si adui wako hivyo hivyo hizi tozo kama ni za raisi aliyepita kama huzitaki kwann usiziondoe??
Aina ya washauri wa uchumi tulionao hawashauri kwa maslahi ya wananchi bali maslahi ya serikali...wanatafuta tozo tu mpaka kuna bidhaa zina tozo za kujirudia.,Na ukubwa wa gharama za 'uendeshaji'.
 
Back
Top Bottom