Bora wewe umeongea ukweli wa moyo wako, hakuna mwanamke ambaye anaweza kuachwa na akakufikiria kwa wema, huwa wanatamani hata ufe
Wangu nilimuombea mabaya mno,sikutamani kumuona akifanikiwa wala akiwa na furaha kabisa,ilinichukua zaidi ya miaka mitatu au minne na zaidi.Nilianza kusali,lakini sala zangu zilikuwa ni za uchungu na laana juu yake nilikuwa nalia mnoπ₯Ίπ₯Ίnilikuwa najiona nasali kumbe kiuhalisia nilikuwa nanungβunika(kwa tafsiri nyingine ni kwamba nilikuwa namwambia Mungu amwangamize)
Nilikuwa nakwenda kwenye maombi sana kanisa la KKKT Korogwe,au Kwenye mikutano ya Mwalimu Mwakasege kipindi hicho ilikuwa ni viwanja vya mlimani kabla hajaamia Tanganyika Packers.kupindi chote nilikuwa nasali kwa kunungβunika tu.
Siku ya mwisho wa mkutano Tanganyika packers wa mwakasege ndo siku ambayo nilifunguliwa ufahamu kwa yale maombi ya miaka yote niliyokuwa nayaomba.sikuwa sahihi hata kidogo.nilijipa muda wa kumtafakari Mwamba kwa kina sana nikagundua kuwa ninadhambi ya kutubu ya kumuombea masta mabaya.mwamba alikuwa baba,mama,kaka,dada,mshkaji wangu,mwalimu wangu alikuwa kila kitu kwa kipindi hicho.
Ilinibidi nianze upya kusali kuomba toba iliyothabiti.nakumbuka nilifunga siku 80 kama sio 100 kwa ajili ya kuomba msamaha kwa Mungu kwa maombi ya laana niliyokuwa nikumuombea.niliahidi kufunga hata siku elfu moja mpka pale nitakaposhusha mzigo niliokuwa nimemuwekea mwamba siku nitakayopata Amani na nikawa sina kinyongo tena basi ndipo siku nitakayoacha kufunga(wachache mno watanielewa nikisema kushusha mzigo na kuitafuta amani ya moyo)
Moyo wangu ni mweupe kwake kama theluji.ninauhakika alitumwa na Mungu kwenye maisha yangu kwa asilimia π―.yapo mengi sana ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya huyu kiumbe.
Na nikisikiaga mke wake anamsumbua natamani nikamzibue huyo mwanamke vibao 20 mfululizo astuke usingizini.
Mpka sasa sijapata mtu siriazi mwenye tabia kama zake. alinifundisha usela flani Hivi.imagine tulikuwa tukitaka kupelekeana moto utamsikia βmwanangu tukapige basi gameβorβtwende tukakulane basiβtulikuwa tukipika pamoja..huku vitunguu vinaungua jikoni sisi tu napiga gameππjamani..yani tulikuwa kama watoto vile.
Mjinga yule alijua kunifundisha maisha namshukuru mno. Sijui nisingekutana nae kwenye maisha haya ningekuwa na maisha gani.nazidi kumtukuza Mungu kwa ajili yake aiseh.
Niliahidi kumchukua yatima mmoja awe mtoto wangu niwe mzazi wake hii yote ni kusema asante kwa Mungu na Mwamba kwa waliponitoa.hili ni lazima nilitekeleze hatotokea wa kuubadilisha huu msimamo.
Mungu wa majeshi azidi kumtunza huyu baba.amuepusha na kila hila ya muovu shetani.Amen