EX wako unamuombea maombi gani na kwanini?

Unasema hufanyi nini??labda pengine umri bado.aise..
Umejeruhika mno Chief.muda ni mponyaji mzuri sana utakuja kuoa bhana usifanye hivyo na wewe.

Mwanamke atakaekuwa na wewe atateseka kwa kipindi fulani maana unamajeraha mno.

Pole sana mwamba aiseh 😌😌😌
Hata simtesi mi sina desturi za niumizwe na grace halafu nikalipize kwa Careen big no nitamtafta grace nimpe hata nusu ya maumivu aliyonipa Niko kwenye mahusiano tena yana mwezi tu navyomtreat huyu mtoto mpaka haamini anasema ameuona ufalme wa Mungu
 
Abou pleeeeaase...😌

Achana na huyo mtu nawala usifikirie kulipa kisasi.please

Please Abou🥺🥺🥺
Labda watu waache kumtaja taja najuta hata kwanini nilimtambulisha kwa kila mtu maana washkaji wakikupigia wanaanza "baba fulani" wakati ww hata humkumbuki.
 
Hata simtesi mi sina desturi za niumizwe na grace halafu nikalipize kwa Careen big no nitamtafta grace nimpe hata nusu ya maumivu aliyonipa Niko kwenye mahusiano tena yana mwezi tu navyomtreat huyu mtoto mpaka haamini anasema ameuona ufalme wa Mungu
Ohooo Amen..

Najua taratibu kabisa hata na roho ya kisasi itapungua.😊😊nakuombea masta
 
Labda watu waache kumtaja taja najuta hata kwanini nilimtambulisha kwa kila mtu maana washkaji wakikupigia wanaanza "baba fulani" wakati ww hata humkumbuki.
Waambie ukweli.waambie kuwa hauko nae.waambie hupendi wala hufurahishwi na wanavyomtaja kila siku.waambie wasikukoseshe Amani.Waambie
 
Yule mtu bana alikuwa na dharau flan baada ya kutusua kwenye haya maisha.Akawa na dharua za hapa na pale na anajua wadada wengi wanamng'ania.baada ya mim kumaliza chuo nkaondoka Dsm tukawa tunawasiliana ila kwa kusua sua..hapo mim sina kazi basi hata nkimtafuta mara niko bz unajua kazi za watu.miyeyusho mingi had mawasiliano yakaanza kulegalega hadi yakaisha.amezunguka sana tu muda wa kuoa ulipofika akaona mimi ndo nafaa kuwa mkewe.anakuja kunitafuta tayari mim nshakuwa na familia.Aliniomba na kunisihi niachane na mume wangu..nadhani hakuamini ni mim niliyempa yale majibu hadi leo.Basi analia lia ooh mim ndo nlistahili kuwa mumeo sijui nilikuwa na malengo nawe.Mimi namzoom tu jamani..alinichosha zaidi alipokuwa ananiambia kuwa anakuja mkoa nilipo tukutane tuspend siku mim na yeye.nkamwambia haitawezekana wala sihitaji hayo mambo.hakunitafuta tena na mim wala sina story nae
Duh pole sana,alichezea shilingi chooni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha mema
Ya baraka
Apate furaha , Amani, ustawi zaidi, na yote yaliyo mema.
 
Unamlaani?kwanini!

Unambariki?kwanini!

Ninambariki mno mno..nitafarijika niko endelea kumuona anafanikiwa na kuishi na ndoa yake kwa upendo na amani.

Mungu azidi kumkinga na hatari katika maisha yake alikuwepo wakati ninauhitaji na kila mtu aliniacha(nalithamini hilo kuliko kawaida) Mungu azidi kumtunza mtu huyu.

Twende kazi.

🧚‍♀️🧚‍♀️🧚‍♀️🧚‍♀️🤸‍♀️🤸‍♀️🤸‍♀️
Mm sina lakusema na muachia mungu tu maana ali niumiza sana,mpaka nika ondoka kijijini nikaja mjini kuanza maisha mapya, ila sjui ni mshukuru tu,asinge niacha bado ngekua kijijini aise,mungu ambariki kwa kuniacha.
 
Yule mtu bana alikuwa na dharau flan baada ya kutusua kwenye haya maisha.Akawa na dharua za hapa na pale na anajua wadada wengi wanamng'ania.baada ya mim kumaliza chuo nkaondoka Dsm tukawa tunawasiliana ila kwa kusua sua..hapo mim sina kazi basi hata nkimtafuta mara niko bz unajua kazi za watu.miyeyusho mingi had mawasiliano yakaanza kulegalega hadi yakaisha.amezunguka sana tu muda wa kuoa ulipofika akaona mimi ndo nafaa kuwa mkewe.anakuja kunitafuta tayari mim nshakuwa na familia.Aliniomba na kunisihi niachane na mume wangu..nadhani hakuamini ni mim niliyempa yale majibu hadi leo.Basi analia lia ooh mim ndo nlistahili kuwa mumeo sijui nilikuwa na malengo nawe.Mimi namzoom tu jamani..alinichosha zaidi alipokuwa ananiambia kuwa anakuja mkoa nilipo tukutane tuspend siku mim na yeye.nkamwambia haitawezekana wala sihitaji hayo mambo.hakunitafuta tena na mim wala sina story nae
Ni suala la mda tu.
 
Mm sina lakusema na muachia mungu tu maana ali niumiza sana,mpaka nika ondoka kijijini nikaja mjini kuanza maisha mapya, ila sjui ni mshukuru tu,asinge niacha bado ngekua kijijini aise,mungu ambariki kwa kuniacha.
Mshukuru sana..unajua kuna mambo mengine huwa yanatokea ili kujifunza.wengi hatuangalii hilo
 
Back
Top Bottom