Facts kadhaa zinazoufanya Mkataba wa Tanzania na Dubai juu ya Bandari kuwa batili. Tuwe nazo Makini

Mkuu, kuhusu 'mapungufu' na 'madoa' ya kisheria kwenye hii IGA ambayo wataalam na wabobevu mbali mbali wamekuwa wakiyapazia sauti, nini maoni yako kama mwananchi?

-Kaveli-
Kila kifungu cha mkataba huo mi nakiangalia kwa namna 4 hadi 5.
1. Kazi ya IGA hii ni nini?
2. Maana ya kilichoandikwa
3. Dhahania ya kwanini kimeandikwa hivyo
4. Natumizi yake kwa ujumla wake
5. Kilichoandikwa ni matokeo ya majadiliano ya pande mbili zenye sifa ya kuvutia upande wake kwa kila mmoja.

Katika hali kama hiyo, hamuwezi kuwa na mkataba au makubaliano ambayo upande mmoja utakuwa umepata kila kitu. Ukisoma maoni mengi, wamejikita kwenye maana ya kilichoandikwa bila ku foresee kwanini au ilikuwaje hadi kikaandikwa hivyo.

Mpaka sasa, kwa vifungu vinavyopigiwa kelele mimi binafsi naona havina shida za hivyo. Na naamini, kuna upotoshaji wa kimaslahi kutoka kwa watu wachache halafu wengi wameunga tela kwa kufuata mkumbo.

Kuna viashiria vingi sana vinaonyesha kuwa kuna upotoshaji. Mfano, IGA inataja kiambatisho chenye maeneo ya kipaumbele katika utekelezaji kama phase I, lakini cha kushangaza opponents hawayataji hayo maeneo ila zaidi wanatuambia kuwa bandari imeuzwa mazima. Unajiuliza, sasa kama Tanzania ishatoa Bandari (yote), logic ya maeneo ya utekelezaji ya phase I yanakujaje?

Kuna hoja ya kwanini Bandari ya Zanzibar haipo. Huhitaji kuwa mfanyabiashara mkubwa kujua kuwa bandari ya Zanzibar sio economically viable kwa investor yoyote yule. Hivi Bandari ya Zanzibar utaifanya hub kwa ajili ya mzigo wa kwenda kuuza wapi? Au mtu anakwenda Lindi na kuwaambia hii Bandari yenu itachukuliwa na DP World! Hivi kwa akili za kawaida tu, DP ajenge au aendeleze Bandari Lindi kwa interest gani? Will it be economically viable?

Lakini pia, kwanini akili zetu zimejijenga kwenye kuvunja??

Kwenye hoja ya ukomo. Unamuuliza mtu, IGA imesema ukomo wake ni subject ya mikataba ya utekelezaji ambayo imetajwa, then unamuuliza je nini itakuwa maoni yako kama hiyo mikataba itakuwa imesema miaka 10, je baada ya miaka 10, IGA itaendelea kuwa hai? Hupati majibu. Au unamuuliza wewe ulitaka hicho kifungu cha ukomo kiwe vipi? Anakwambia kitaje miaka kama 10, 20, 30 etc, unamuuliza basis ya kuandika 10, au 20 au 30 ni nini? Hana majibu.

In short, mambo ni mengi.
 
Nakuuliza umepigwaje? Achana na maneno ya kijiweni.
Tuje kwenye ahadi zilizotolewa, gas ikifika dar itasaidia kwenye usalishaji wa umeme na umeme ungeshuka bei na ingeondoa kabisa kukatakata kwa umeme. Hilo la kwanza, ilitekelezeka?
 
Mambo yasiyo na mwelekeo pia ambayo ni fitinishi kama unayopenda kiposti mara kwa marq.
Hii ni definition yako au umeitoa wapi? Na kiwango cha mantiki ya post zangu unapima wewe? Wewe na nani?
 
Hii ndo ilikua suluhisho tupigane na polis wao adi kieleweke sema tumekua waoga sana
Hizi ni kauli za kuambiana kwa sasa. Kavu kavu kama alivyosema nshalla. Uzuri hata wao wana roho moja.
...WHEN THE SOFT WAY FAILS, THE HARD WAY IS INEVITABLE..
 
haya umeyatoa unakojua mwenyewe
 
Hii ni definition yako au umeitoa wapi? Na kiwango cha mantiki ya post zangu unapima wewe? Wewe na nani?
CHADEMA mna matatizo vichwani. Mnadhani nchi ni Kaskazini tu. Ndo maana hamtakuja kuupata uraisbwa hii nchi mpaka kiama. Hamfai kabisa.
 
Kwamba HGA zote ni Non-disclosure?

-Kaveli-
Ndio, utaona tu kampuni sehemu inapiga kazi. Au watu mnahamishwa, basi.

Kule ngorongoro si wamasai walihamishwa! Uliuona huo mkataba? Tuanzie hapo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…