Dan Zwangendaba
JF-Expert Member
- Apr 25, 2014
- 5,814
- 8,118
Kila kifungu cha mkataba huo mi nakiangalia kwa namna 4 hadi 5.Mkuu, kuhusu 'mapungufu' na 'madoa' ya kisheria kwenye hii IGA ambayo wataalam na wabobevu mbali mbali wamekuwa wakiyapazia sauti, nini maoni yako kama mwananchi?
-Kaveli-
1. Kazi ya IGA hii ni nini?
2. Maana ya kilichoandikwa
3. Dhahania ya kwanini kimeandikwa hivyo
4. Natumizi yake kwa ujumla wake
5. Kilichoandikwa ni matokeo ya majadiliano ya pande mbili zenye sifa ya kuvutia upande wake kwa kila mmoja.
Katika hali kama hiyo, hamuwezi kuwa na mkataba au makubaliano ambayo upande mmoja utakuwa umepata kila kitu. Ukisoma maoni mengi, wamejikita kwenye maana ya kilichoandikwa bila ku foresee kwanini au ilikuwaje hadi kikaandikwa hivyo.
Mpaka sasa, kwa vifungu vinavyopigiwa kelele mimi binafsi naona havina shida za hivyo. Na naamini, kuna upotoshaji wa kimaslahi kutoka kwa watu wachache halafu wengi wameunga tela kwa kufuata mkumbo.
Kuna viashiria vingi sana vinaonyesha kuwa kuna upotoshaji. Mfano, IGA inataja kiambatisho chenye maeneo ya kipaumbele katika utekelezaji kama phase I, lakini cha kushangaza opponents hawayataji hayo maeneo ila zaidi wanatuambia kuwa bandari imeuzwa mazima. Unajiuliza, sasa kama Tanzania ishatoa Bandari (yote), logic ya maeneo ya utekelezaji ya phase I yanakujaje?
Kuna hoja ya kwanini Bandari ya Zanzibar haipo. Huhitaji kuwa mfanyabiashara mkubwa kujua kuwa bandari ya Zanzibar sio economically viable kwa investor yoyote yule. Hivi Bandari ya Zanzibar utaifanya hub kwa ajili ya mzigo wa kwenda kuuza wapi? Au mtu anakwenda Lindi na kuwaambia hii Bandari yenu itachukuliwa na DP World! Hivi kwa akili za kawaida tu, DP ajenge au aendeleze Bandari Lindi kwa interest gani? Will it be economically viable?
Lakini pia, kwanini akili zetu zimejijenga kwenye kuvunja??
Kwenye hoja ya ukomo. Unamuuliza mtu, IGA imesema ukomo wake ni subject ya mikataba ya utekelezaji ambayo imetajwa, then unamuuliza je nini itakuwa maoni yako kama hiyo mikataba itakuwa imesema miaka 10, je baada ya miaka 10, IGA itaendelea kuwa hai? Hupati majibu. Au unamuuliza wewe ulitaka hicho kifungu cha ukomo kiwe vipi? Anakwambia kitaje miaka kama 10, 20, 30 etc, unamuuliza basis ya kuandika 10, au 20 au 30 ni nini? Hana majibu.
In short, mambo ni mengi.