Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

WHO: Tunakabiliwa na uhaba wa vifaa vya kujikinga na virusi vya Corona

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus ameonya kuwa ulimwengu unakabiliwa na uhaba wa vifaa maalum vya kufunika uso pamoja na vifaa vingine vya kujikinga na virusi vya Corona.

Akizungumza leo katika kikao cha bodi ya wakurugenzi wa WHO mjini Geneva, Ghebreyesus amesema mapema wiki hii walianza kupeleka vifaa hivyo kwenye nchi zinazohitaji msaada.

Ghebreyesus amesema hadi sasa virusi vya Corona vimesababisha vifo vya watu 637 nchini China na wengine 31,211 wameambukizwa. Amesema katika siku mbili zilizopita pamekuwa na taarifa chache za watu walioambukizwa virusi hivyo nchini humo ambayo ni habari njema.

Hata hivyo, ametahadharisha kuhusu kuzitegemea zaidi takwimu hizo, kwani idadi ya waathirika inaweza kuongezeka tena. Mkurugenzi huyo wa WHO, amesema kuna baadhi ya nchi zimeshindwa kutoa takwimu kamili za kitabibu za watu waliothibitika kuambukizwa virusi vya Corona. [DW]
 
Hiyo idadi ya wagonjwa waliopata ahueni inatoa tafsiri gani mkuu FRANC THE GREAT ?
Ni aidha hawakuwa na ugonjwa au matibabu waliyopewa yamefanya kazi hivyo basi kuna tiba ya coronavirus?
Nieleweshe tafadhali
Mpaka sasa hakuna tiba ya Coronavirus.

Kinachofanyika ni kuwa, unatumika mchanganyiko wa dawa mbalimbali za maradhi mengine kwa mfano ya Ebola na HIV ili kutibu dalili za virusi vya Corona.

Kinachotibiwa ni dalili za virusi hivyo na si kukiangamiza kirusi chenyewe.

Baadhi ya dawa hizo ni dawa ya Ebola inayoitwa Remdesivir. Dawa hii imekwisha tumika kuwatibu watu wenye Coronavirus lakini bado iko katika majaribio na pia matibabu yanategemeana na hali ya kiafya ya mgonjwa na pia umri kwa baadhi ya watu.

Kwahiyo kinachofanyika sasa hivi ni matibabu ya dalili za virusi hivyo pamoja na uangalizi wa karibu kwa wagonjwa kwa Kiingereza tunaiita Supportive Care.
 
Mpaka sasa hakuna tiba ya Coronavirus.

Kinachofanyika ni kuwa, unatumika mchanganyiko wa dawa mbalimbali za maradhi mengine kwa mfano ya Ebola na HIV ili kutibu dalili za virusi vya Corona.

Kinachotibiwa ni dalili za virusi hivyo na si kukiangamiza kirusi chenyewe.

Baadhi ya dawa hizo ni dawa ya Ebola inayoitwa Remdesivir. Dawa hii imekwisha tumika kuwatibu watu wenye Coronavirus lakini bado iko katika majaribio na pia matibabu yanategemeana na hali ya kiafya ya mgonjwa na pia umri kwa baadhi ya watu.

Kwahiyo kinachofanyika sasa hivi ni matibabu ya dalili za virusi hivyo pamoja na uangalizi wa karibu kwa wagonjwa kwa Kiingereza tunaiita Supportive Care.
Asante kwa ufafanuzi huu mkuu.
 
UPDATE: Marekani imetoa kiasi cha Dola milioni 100 kwa China na mataifa mengine yaliyoathiriwa na virusi vya Corona ili kupambana na virusi hivyo vinavyoenea kwa kasi. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo amethibitisha.

====

Washington (AFP) - The United States on Friday offered up to $100 million to China and other impacted countries to combat the fast-spreading coronavirus.

"This commitment along with the hundreds of millions generously donated by the American private sector demonstrates strong US leadership in response to the outbreak," Secretary of State Mike Pompeo said in a statement.

"We encourage the rest of the world to match our commitment. Working together, we can have a profound impact to contain this growing threat," he said.

Pompeo, who has frequently criticized China on issues from human rights to its overseas infrastructure spending, said the United States would provide the assistance either directly or through multilateral organizations.

He said the spending would come out of unspecified funds that have already been allocated within the US government.

1581114128155.png
 
UPDATE: CORONAVIRUS
  • 34,375 confirmed cases worldwide
  • 26,359 suspected cases
  • 719 fatalities
  • 5,894 in serious/critical condition
  • 1,838 recovered
  • Most cases in China
  • 25 countries reporting cases

More updates to come!
 
wamefikia wapi ile hatua china watu walioomba kuwa uwa wenye hao virusi au ilikuwa ni fake news?
 
UPDATE: Umoja wa Falme za Kiarabu UAE imethibitisha visa vipya viwili (2) hivyo kufikisha jumla ya visa saba (7) nchini humo.
 
UPDATE: Idadi ya vifo vitano (5) imeongezeka tangu ripoti ya mwisho ilipotoka hivyo idadi ya vifo vyote imefikia 724 huku idadi ya visa vyote ikifikia 34,872 duniani kote.

Pia, wagonjwa takribani 1,568 wamepata nafuu.

1581122744503.png
 
UPDATE: CORONAVIRUS
  • 34,878 confirmed cases worldwide
  • 27,657 suspected cases
  • 724 fatalities
  • 6,107 in serious/critical condition
  • 2,050 recovered
  • Most cases in China
  • 25 countries reporting cases

More updates to come!
 
Back
Top Bottom