Bahati mbaya ni kutokuwa na viongozi wenye maono ya kutuondoa katika hali hiyo; badala yake wanazidi kutuhimiza tudidimie zaidi hata kuliko tulivyokwishapiga hatua chache mbele. Tunaambiwa tukasali, tutumie 'nyungu' na dawa ambazo hakuna ushahidi wowote wa kuonyesha zinafanya kazi kwenye ugonjwa huu mpya..
Ni kama tunarudi kinyumenyume, badala ya kwenda mbele kwa kasi; kwa sababu sisi tunatakiwa kuigiza tu, jinsi ya kutumia yaliyokwishavumbuliwa na wenzetu ili yatuletee maendeleo haraka.
Hatuna haja tena ya kufanya uvumbuzi mpya wa haya mambo.
Kama ni laana, laana yetu ipo hapo: kushindwa kutumia njia zilizopo tayari ili twende haraka mbele.