Na si kuumwa tu chembe ya moyo na tumbo unaweza hata kujifikiria una ukimwi maana dalili zake ni nyingi vidonda mdomoni maumivu ya mwili hata unaweza kufikiri ni typhoid au malaria mgongo na kiuno kuuma miguu uchomvu mwilini kichwa kuuma miguu kuwanga nk
Kweli kabisa!
Hapa tatizo hasa huwa ni lipi?
Maana ukienda hospitali ukiwaelezea dalili ya unavyosumbuliwa na tumbo suspect yao ya kwanza huwa ni vidonda vya tumbo!
Nilishawahi kupimwa hispitalini wakaniambia nina vidonda vya tumbo wakanipa dawa za kutuliza vidonda vya tumbo na wakaniambia nisile baadhi ya vyakula lakini dawa hiyo haikunisaidia sana.
Ikabidi nibadilishe hospitali nikaenda kukutana na specialist wa masuala ya tumbo yeye baada ya vipimo akaniambia sina vidonda vya tumbo ila nina fungus tumboni hivyo nile vyakula vyote nilivyokuwa nimezuiliwa mara ya kwanza akanipa dawa ya kutibu fungus. Nimetumia dawa hiyo ikanipunguzia maumivu kwa kiasi kikubwa sana na nikaona ahueni.
Tumbo kuuma kwa dalili zilizokuwepo mwanzoni ziliisha yaani kuuma pale unapohisi njaa badala yake lilianza kuuma kivingine likawa linauma juu kwenye ubavu au chini ya kitovu yaani maumivu yanakuwa yanahama! Nikaenda tena hospitali nyingine nikapima wakaniambia bandama ina shida sikuwaelewa ikabidi niende sehemu nyingine wakanipima wakaniambia sina tatizo hilo lakini wakasema kuna dalili za vidonda vya tumbo tu kuna mikwaruzo kwa mbaaaali! Wakanipa dawa nikatumia nikapata ahueni tena mpaka sasa ni afadhali kwa upande wa tumbo.
Kuna shida zingine kama uchovu wa mwili, kukosa appetite ya chakula, kutokuongezeka uzito(nimekuwa na uzito ule ule zaidi ya miaka minne pamoja na kuwa nimeimprove kidogo level ya maisha na sina majukumu makubwa yanayonikabili kwa wakati huu) nk bado hizi zinakuwa zinajirudia.
Dawa ambazo nimekwishatumia ninazokumbuka ni Rabeprazole, Esomeprazole. Kwa jinsi majibu ya hospitalini yanavyokuwa yanakinzana huwa nashindwa kujua tatizo linalonisumbua hasa ni lipi ninachoweza kuelezea tu ni jinsi ninavyoumwa ila tatizo lenyewe sijui hasa ni lipi!
Sijawahi kuumwa seriously kuweza kuacha kutekeleza majukumu yangu ya kila siku!
Hebu naomba kwa experience ambavyo mnafahamu mnisaidie. Tatizo hasa ni nini?
Dawa yake ni ipi?