Acha ujinga; kama umeshahamia usiwaze, hiyo barua ichane endelea na shughuli zako, vinginevyo labda kama kuna ujenzi unaendelea, lakini kama umeshahamia, na hakuna ujenzi wewe chana hiyo barua endelea na shughuli zako! Utaratibu Wa kibari cha ujenzi maeneo ya skwata ulikuwa na lengo zuri sana; ambalo lilikuwa ni kupunguza migogoro ya ardhi, lakini utekelezaji wake umekuwa kinyume na imegeuka kero!
1. Unatakiwa kuaandaa ramani architectural drawing inayoonesha view zote ikiwemo site plan zilizogongwa mihuri ya architect, hii gharama hufikia hadi 400000~600000/= kwa nyumba za kawaida
2. Utatakiwa kuwa na nakala tatu, ukiambatanisha na hati ya kiwanja na barua kutoka see/ mtaa
3. Gharama za kuwapeleka site hao jamaa bila kuwatoa hawaji, na kama wakija lazima watafte kasoro mfano; uwepo Wa njia,ushahidi wawakute majilani site yaani waache kwenda job kwa ajili yako.
4. Utapaswa ulipie kibali wanachaji kwa square meta makadirio nyumba nyingi 88000~150000/=
HIYO MILOLONGO UKICHUMLISHA INAKATISHA TAMAA! Ilitakiwa mwanachi achangie malipo yasiyozidi 20000/=
CHA AJABU KULIKO VYOTE, Gari la kuja kufanya savei wanakujibu halina mafuta, lakini ukijenga bila kibali huwa wanakuja fasta sijui huwa wanapata wapi mafuta!
USHAURI WANGU CHANA HIYO BARUA ACHANA NAO HAWANA CHA KUKUFANYA USHAJENGA IMETOKA HIYO