Fahamu kuhusu vibali vya ujenzi, umuhimu wake na namna ya kuvipata


Huuu ushauri mzuri sana ikiwezekana twende kuubandika kwenye ofisi zao na hapo kwenye maneno ya mwisho tuweke bold..

Kwanini gari la kuja kufanya survey huwa halina mafuta ila ukisha jenga bila kibali gari hilo linapata mafuta
 
Kuwa makini kuna utapeli ukihusisha baadhi ya maafisa wasio waaminifu. Wangapi wamejenga bila hivyo vibali nchi hii, ukiamsha hili si unataka balaa?

Hao wametengeneza mfumo wa kupiga wageni wanaohamia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
dmkali,

Nikweli. Hawa mbuzi ukienda kuwachukua wanasema gari yao haina mafuta. Ukishajenga wakitaka rushwa, mafuta wanayo.
 
Ukifanya mchezo watapiga X, Nenda mkaelewane vizuri ulipe hizo penati na gharama watakazokutajia.Hakikisha unalipa reasonable cost siyo wakupige mikwala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amesema mwenyewe hakuwa na kibali cha ujenzi.

Kwa kumsaidia tu hao serikali za mtaa sijui kata wao hawahusiki na vibali vya ujenzi. Wahusika ni Manispaa (kwa case yako ni Manispaa Temeke nafikiri).

Na hakuna muda ambao manispaa zilisitisha kutoa vibali vya ujenzi kwani ni kitu muhimu sana kabla hujaanza shughuli yoyote ya ujenzi.

Je, kwanini kibali cha ujenzi ni muhimu?
Unapoenda kuomba kibali cha ujenzi lazima uambatishe na nyaraka halali za umiliki wa kiwanja na ramani ya nyumba(floor plan, elevations, soakaway pit etc) tarajiwa. Kupitia nyaraka hizo especially ramani ya nyumba utashauriwa na kurekebishwa sehemu zenye makosa na kukuepushia gharama na usumbufu zisizo za ulazima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukifanya mchezo watapiga X,Nenda mkaelewane vizuri ulipe hizo penati na gharama watakazokutajia.Hakikisha unalipa reasonable cost siyo wakupige mikwala

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani barua haina nembo ya manispaa, nenda hii tabia ya kudharau wito ni hatari sana hujafanya kosa la jinai nenda kajieleze utapigwa faini yataisha mm kijenga tu uzio wa ploto zilinitoka zakutosha
 
Ukifanya mchezo watapiga X,Nenda mkaelewane vizuri ulipe hizo penati na gharama watakazokutajia.Hakikisha unalipa reasonable cost siyo wakupige mikwala

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao mbuzi wapiga X kujifurahisha tu. Hawavunji nyumba ya mtu. Muulize Lukuvi au kama una mtu ikulu mwambie akuulizie kwa.
 
Inatakiwa uwafuate sio wakufuate. Idea ni nzuri ila utekelezaji, rushwa na uzembe wao unaleta kero, theoretically inabidi uende kabla wakushauri usije jenga kumbe unatumia njia za kuleta maafa au kero kwa eneo husika, kwahio wanategea uanze wakuombe rushwa, ushauri aulize majirani zake kama wana permit na walitoa ngapi kupata idea.
 

Nimekuelewa na najua utaratibu unavyotakiwa kwenda mkuu. Lakini kama ulivyosisitiza, unaweza kufuatilia kibali cha ujenzi lakini utakavyozungushwa unaweza kujikuta umekula pesa ya ujenzi. Hapo kuna uzembe wa pande zote mbili, kwa muktadha huo ilibidi waje kudai faini ya kutokuwa na kibali cha ujenzi maana wanajua fika hawakukitoa. mazingira ya rushwa yametamalaki.

Afadhali kidogo siku hizi upatikanaji wa hati kidogo umerahishishwa na unawezapata kwa gharama ndogo.
 
Mtafute mjumbe na mwenyekiti wa CCM hapo unapoishi watakusaidia pa kuanzia
 

Mkuu umeandika kila kitu sawa ila ushauri wako sio mzuri. Jamaa kapewa notice according to regulations za ujenzi hapo ni kama mtego tu wana msikilizia tu afanye kama unavyomshauri steps zingine zitafata.

Kujenga bila kibali cha ujenzi kinaweza kukusababishia nyumba yako kubomolewa kwendana na building regulations.
Kushindana na authority sio jambo jema.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kuwa makini kuna utapeli ukihusisha baadhi ya maafisa wasio waaminifu. Wangapi wamejenga bila hivyo vibali nchi hii, ukiamsha hili si unataka balaa?

Hao wametengeneza mfumo wa kupiga wageni wanaohamia.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu kusema kuwa watu wengi wanafanya kosa haikupi sababu ya wewe kufanya ilo kosa. Sheria inakataza kuanza ujenzi pasipo kuwa na building permit kutoka kwa authority. Hao wakiamua kuisimamia sheria atakae umia ni mtoa mada.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Amesema amejenga kwenye skwata! Regulations?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yale makazi holela yaliyorasimishwa pia wanafuata hivyo vibali.
 
Hii kitu huenda inachangia kupungua kwa kiwango cha ujenzi cha mtu mmoja mmoja kwenye jamii ukiachilia mbali swala la changamoto ya kiuchumi!

Yani vibali vya ujenzi ni shida! Though nia ilikuwa ni njema lakini imeleta kukwama kwa ujenzi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo zoezi la kua na Building Permit ndio limeanza sasa, hapa majirani zangu hakuna mwenye hiyo permit ila naona wameziangalia nyumba mpya tu kama ni ya zamani hawatoi hiyo notice, nitakwenda nijue.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…