Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwangu Samsung kazidi tu sababu infinix ni Go edition,hii inashusha sana simuAndroid 10 ambao ni Go Edition.
Hilo toleo Go edition kama limefungwa yan,huchukui kitu nje ya play store (baaz ya simu)kweli kabisa
Mkuu kumbe umeligundua hilo na wewe? Afu kwenye minimize pia wanatoka mapema sana,unakuta simu ram 2 lakini ukifungua app 1 kurudi juu ya sec 10 unakuta app ishajifunga,kero kwa wengiHapo ndipo walipojichanganya
Mkuu me kwa sasa simu za android nanunua kuanzia ram gb3 kuendelea maana zinakuaka za ovyo sana basi tuMkuu kumbe umeligundua hilo na wewe? Afu kwenye minimize pia wanatoka mapema sana,unakuta simu ram 2 lakini ukifungua app 1 kurudi juu ya sec 10 unakuta app ishajifunga,kero kwa wengi
Huu uchambuzi sijsuelewa kabisa.Habari nimeona ni share na nyinyi hii,
Katika ushindani wa soko la simu kampuni nyingi za simu zimejikuta zikitoa simu zenye kushabihiana sifa. Kwa leo tuliangalizie kwa ndani simu aina ya Infnix Hot 10 Play na Samsung Galaxy A02s.na mwisho wa makali hii nadhani tutakuwa tumepata kufahamu ipi ni simu sahihi.
kwako kotokana na matumizi yako.
![]()
Sifa za Ndani (CPU, Chipset, RAM na ROM)
Kwa upande wa sifa za ndani, Infinix Hot 10 Play inakuja na CPU yenye uwezo zaidi hadi Octa- core (2×2.0 GHz Cortex-A75 & 6×1.8 GHz Cortex-A55), huku Galaxy A02s ikiwa nyuma yake kwa kuwa na CPU yenye uwezo wa hadi Octa-core 1.8 GHz Cortex-A53.
Mbali na hayo, Infinix Hot 10 Play inakuja na Chipset ya MediaTek Helio G35, wakati Galaxy A02s inakuja na Chipset ya Qualcomm Snapdragon 450. Chipset zote zinakuja na uwezo tofautin ani rafiki hata katika uchezaji games kupitia simu hizo.
Kwa upande mwingine wa RAM, Infinix Hot 10 Play inakuja na RAM ya GB 4, huku Galaxy A02s yenyewe ikiwa inakuja na RAM kati ya GB 3. Tukiangalia uhifadhi wa ndani, Galaxy A02s inakuja na ROM ya GB 32, huku pia Infinix Hot 10 Play nayo inakuja na ROM ya hadi GB64.
Uwezo wa Battery
Infinix Hote 10 Play ni moja kati ya simu ambayo ipo kwenye list ya simu zinazodumu na chaji zaidi mwaka 2021, hii ni kwa sababu simu hii inakuja na battery kubwa yenye uwezo wa hadi 6000 mAh, huku ikiwezeshwa na teknolojia ya kufanya ijae na chaji kwa haraka yaani Fast charging yenye uwezo wa 10 Wh. Galaxy A02s yenyewe inakuja na battery ya 5000 mAh, huku nayo ikiwa na Fast charging ya hadi 18 Wh.
Muundo
Kwa kuanza, tuakiangalia muundo wa simu zote mbili, zote zimetengenezwa kwa plastiki, hii ikiwa na maana muundo wa nyuma wa simu hizi ni plastiki, na hata fremu yake pia ni plastiki. Kwa nyuma Infinix Hot 10 Play inakuja na sehemu ya ulinzi ya fingerprint, huku Galaxy A02s yenyewe ikiwa haina sehemu hiyo kabisa.
Kioo
Kwa upande wa kioo Infinix hot 10 play inakuja na kioo kikubwa wa inch 6.82, huku Galaxy A02s ikiwa inakuja na kioo cha inch 6.5. Mbali na hayo, kioo cha Infinix Hot 10 Playkimetengezwa kwa teknolojia ya IPS LCD, wakati kioo cha Galaxy A02s kikiwa kimetengezwa kwa TFT/PLS IPS. Kwa upande wa resolution simu zote mbili zinakuja na uwezo wa 720p.
Kamera
Kwa upande wa kamera Samsung Galaxy A02s na Infinix Hot 10 Play zote zinakuja na kamera kuu za nyuma za Megapixel 13, huku Galaxy A02s ikiwa na kamera mbili zaidi zenye Megapixel 2 kila moja. Hii inafanya simu ya Galaxy A02s kuwa na Kamera tatu, huku Inifnix Hot 10 Play ikiwa na kamera mbili kwa nyuma.
Kwa upande wa kamera za mbele, Infinix Hot 10 Play inakuja na kamera ya Megapixel 8, huku Galaxy A02s ikiwa inakuja na kamera ya mbele ya Megapixel 5. Pia kamera hiyo ya Infinix Hot10 Play inakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p@30fps. Vilevile Infinix Hot 10 Play inakuja na LED flash kwenye kamera ya mbele, wakati Galaxy A02s yenyewe haina sehemu hiyo.
Mfumo wa Undeshaji
Kwa upande wa mfumo wa uendeshaji, Galaxy A02s inakuja na mfumo wa uendeshaji wa Android 10, huku Inifnix Hot 10 Play nayo pia ikija na mfumo wa Android 10 ambao ni Go Edition. Simu ya infinix inakuja na mfumo mpya wa XOS 7, wakati Galaxy A02s ikiwa inakuja na mfumo wa One UI.
Uwezo wa Battery
Infinix Hote 10 Play ni moja kati ya simu ambayo ipo kwenye list ya simu zinazodumu na chaji zaidi mwaka 2021, hii ni kwa sababu simu hii inakuja na battery kubwa yenye uwezo wa hadi 6000 mAh, huku ikiwezeshwa na teknolojia ya kufanya ijae na chaji kwa haraka yaani Fast charging yenye uwezo wa 10 Wh. Galaxy A02s yenyewe inakuja na battery ya 5000 mAh, huku nayo ikiwa na Fast charging ya hadi 18 Wh.
Bei za Makadirio
Kwa upande wa Bei, Inifnix Hot 10 Play inapatikana kwa bei ya makadirio kuanzia TZS 350,000 wakati Galaxy A02s inapatikana kwa bei ya makadirio kuanzia TZS 450,000. Kumbuka bei hizi ni makadirio na zinaweza kubadilika kulingana na eneo unalo nunua simu hizi.
Upatikanaji
Kwa sasa simu zote zinapatikana hapa Tanzania, huku Infinix Hot 10 Play ikiwa inapatikana kupitia kwenye maduka ya kampuni ya kutoa huduma za simu ya Tigo Tanzania, pamoja na maduka ya simu ya Infinix kote Tanzania ikiwa na ofa ya GB 18.
Maji unywe wewe unaefananisha infinix na Samsung. Hujui simu wewe....Kaa kwanza unywe maji
😂 😂 Sawa mkuuMaji unywe wewe unaefananisha infinix na Samsung. Hujui simu wewe....
Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
We umewahi kutumia phantom 6 plus ya tecno?? Ni noma haima tofauti ni Samsung na wengine sema nyie mnatumia za laki 1 na 20 nunua laki4 kuendelea ujione mpaka laki 6 hukoInfinix Hot 10 Play haijawahi kuwa high End .
High end ni kina Sam S21 &Co.. (Flagship)
Mimi nimeshatumia hizo Infnix, Tecno vizuri kabisa lakini amini amini nakwambia hizo ni upupu tu ndio mana nikahama na sina mpango wa kurudi huko
Za makumbusho???
Huwa naziona zina manyonyo na wowowo,za kike sana hizo
Hapana basi tuZina sheria nyingi sana
Kuipenda simu haiji hivi hivi tu.Kweli ujue kila mtu ana mzuka na type za simu , hata mimi iphone sizipendi lakini haimaanishi kwamba ni mbaya au sina hela ya kununua hapana sizipendi tu.
🙏 🙏 🙏 ❣️Daaaah na utaka tuamnin kupitia specs ulzo copy na kupaste n sahihi kabsa
Aya bana ila infix tofaut na zero na zile zenye g80 processors hamna simu apo
Na kibaya zaid zina limited time life ( mafund wa software hope mnalijua hili tatzoo)
So busy with my blackberry q20