Faida na hasara za kujenga nyumba yenye flat roof

ni mtazamo wako
 
Tusaidie basi jibu la kitaalam.
Binafsi huwa nashauri Pitched roof, flat roof ina madhara makubwa kwa nyumba kuliko pitched, posibility ni kubwa ya kuwa na penetration ya rain water kwenye kuta hivyo inasababisha fungus katika kuta, matumizi ya waterproofing membrane yanaweza kuongeza gharama pia, mfano huwezi kuchoma bitumen membrane juu ya bati ya gauge 30 au 32 na hata gauge 28 haishauriwi sana.
 
Hapo kwenye maintenance naomba ufafanue zaidi kwasababu zinatumika mbao na mabati kama nyumba nyingine sema hii roof inakuwa imefichwa na matofali.
Maintenance kwa maana ya kuvuja kunakoweza kujitokeza mara kwa mara kunakotokana na either kuachia mwanya kidogo kwa bati toka kwenye ukuta au kuziba kwa gutter kutokana na majani yaliyoletwa na upepo au wanyama kama ndege, au mawe yaliyorushwa na watoto watukutu
 
Kaka tafadhali mjibu muuliza swali naona umeishia kumtolea mifano ya life spans tu. Tafadhali nakuomba elezea kinachopelekea tuwe na design yenye life span ya mida tofauti. G+ 1 roof na nyumba ya kawaida zina tofauti Gani????
 
Nashukuru sana kwa huu uzi, nina kakibanda kangu kapo hatua ya kupaua nitafikiria kutumia hii design kwa ajili ya kupunguza gharama
 
ondoa shaka boss wangu ni kama mshkaji wangu na ameshajenga nyumba nyingi ndio maana nikaona niombe ushauri kwa mzoefu wa hizi mambo
 
fafanua tafadhali, baada ya miaka 15 natakiwa kuweka paa jipya au?
 
Flat roof siku hizi hutii slab. Unatumia bati za kawaida tu
Hilo sikujua kwamba kuna flatroof za bath,na nilikuwa naumiza kichwa kwa mahesabu ya nondo na zege wakati kumbe kuna alternative.
Napenda sana flatroof,maana nyumba inakuwa unique
 
Hizo shida zote mnazosema kabla ya kuweka hii roof zimezingatiwa. Nikuulize hizi pitched roof hakuna ambazo huwa zinavuja? Sababu ni nini? Obvious ni makosa ya fundi. Kwahio hata hizi fundi anakuwa makini na anajua changamoto yake.

Gutter inayokwa humu sio kama hizo mnazoweka kukinga maji ya mvua. Inawekwa gutter kubwa na bomba kubwa sasa hilo bomba kuziba labda uweke kipande cha tofali.
 
Napata faida kubwa sana hapa na popote pale hii ningetakiwa niilipie!asanteni sana JamiiiForums pia wakuu mnaotiririka hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…