Faida na hasara za kujenga nyumba yenye flat roof

Binafsi najua flat inachukua bati chache na mbao chache ila ikiinuka inakula mbao nyingi na bati nyingi.
 
Mpaka hapa nilichokielewa mimi ni kwamba unaweza ukajenga nyumba kwa style ya flat roof ila still gharama zote utakazozikimbia huku kwenye pitched roof ukakutana nazo huko.

So mfano nyumba yako ambayo ulitamani kuezekwa kwa paa la kuinuka kwa cost ya 10mill ukaja kwenye flat ukafanyiwa 8.5/9mill hakuna ulichookoa mie naona na nadhani labda kama mtu umeamua tu kuchagua style fulani ila kusema unafanya kupunguza gharama hakuna kitu kama hiko.
 
Uko sahihi kabisa mkuu............. Ni mapenzi ya mtu tu, ila technically pitched roof ni best kuliko flat roof
 
Bati za gauge ngapi ndio zinafaa kwa flat roof?
Kwa nyumba zetu hizi za kawaida Gauge 28 mkuu,
Gauge 26 kwa majengo makubwa yale ya serikali,
Gauge 30 kwa vibanda labda cha mtaani maana bati inakua nyepesi
 
Waambie kuna gutter za Zege (concrete gutter)
 
Hii fasion inarud kwa kasi, ila ikiisha fasion hutaona mbaya. Kwa mfano vent za kwenye bati sasa zimeisha fasion
Sio ishu unaweza badili mtindo badae ukitaka. Kwenye ujenzi hakishindikani kitu.
 
Waambie kuna gutter za Zege (concrete gutter)
Concrete gutter huwa haiwezi kuziba mkuu?
Msingi wa hoja yangu kuhusu kufanya maintenance ya gutter ni endapo kama ndege au mijusi imepeleka takataka zinazoweza kuziba hiyo gutter
 
Flat roof ni nzuri changamoto ni kwamba inahitaji finishing ya uhakika, garden nzuri kuzunguka nyumba otherwise itaonekana kama jumba lililoachwa na waarabu.
Teh teh teh. Linakuwa kama kasri. Halafu hili lina gharama zake pia hawajui tu. Yani kwa mtu maskini hiii ni mbaya. Wala haipendezi. Wanaoweka hii naona wengi ni wale wanaojenga ghorafa angalau la flow moja ndo inapendeza lakini kwa nyumba ya kawaida walaa halifai.
 
Halafu matofali mzunguko mzima na gata za zege huoni kama mtu anakuwa hakuna anachokimbia. Gharama zinarudi pale pale tu.


Kama ishu ni design sawa lakini kwa swala la gharama sikubaliani nalo.
Wenzako wanasema inaokoa gharama wewe umekazana kupinga bila hoja za maana, wabongo ni shida aisee. Kama ni ujenzi unaopunguza material kama mbao huoni unasaidia pia kwenye uhifadhi wa mazingira
 
Concrete gutter huwa haiwezi kuziba mkuu?
Msingi wa hoja yangu kuhusu kufanya maintenance ya gutter ni endapo kama ndege au mijusi imepeleka takataka zinazoweza kuziba hiyo gutter
Concrete gutter yenye upana wa futi moja inaziba vipi? Bomba za kushusha maji chini ni 4'' linaziba vipi? Au kuna watu watakuwa wanatupia matofali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…