Faida ya kuishi duniani ni ipi kama tulizaliwa ili tufe?

Faida si hiyo ya kufa.
 
Hivi kweli Mungu hakujua ya kwamba viumbe aliowaumba yeye watakuja kula tunda walilokatazwa?
Kama Mungu anajua future zetu iweje hakutambua hilo?
 
[emoji120]
 
Kwamba kuna vitu sivielewi then wewe unavielewa.....!?

Hv unaelewa nkikwambi kuwa bible ni kitabu cha hadithi!?
Tena ukiwa unaanza kusimulia inabidi uanze kwa kisema "hadith hadithi..."
Ili watu tuitikie
"hadithi njoo uongo njoo utamu kolea.."

Wewe unaleta hadithi za Ibrahimu hapa, hizo ni hadithi za kutungwa tu, unautafuta ukweli kwenye hadithi.

Na kukuonesha kwamba hujui kitu, ni kwamba wewe hujui hata hizo hadithi zimepitia mambo gani!? Zimeandikwa na akina nani...!?
Zimerekebishwa na kuongezewa content mara ngapi..!?
Na umeanza kuamini bila kujua hata chembe ya hiko kitabu.

Hayo maajabu mbona hayatokei siku hizi!?

Huyo Mungu wa waisrael aliyekuwa nao kuwaokoa kutoka Babylon na misri, alishindwa vipi kuwapaisha tena kipind kile cha mtaalam Adolf hittler akawaua mamillion (zaid ya 5 million waliuawa).
Unadhan isingekuwa kabla ya usasa wangeshindwa kuandika hadithi hapo ya Musa part 2!?

Huyo Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote hayupo.
Wala hata hawezekani kuwepo.
Mungu mwenye hizo sifa asingeweza kumjaribu Ibrahimu.
Kitendo cha kumjaribu Ibrahimu kinaonesha kuwa si mjuzi wa yote.
Unaelewa hilo!?
 
Sasa kama ilikuwa ni sex,
Nikisema kuwa huyu Mungu alikuwa hajitambui ntakuwa nakosea!?

Yani aliumba uume na uke halafu akawakataza wasisex??

Kwanini aliwaumba na hzo organs..!?

Mimi nimewaambia watu, hyo project ya eden haikuwa na specific objectives, naweza sema kuwa Mungu alikurupuka tu hakujiandaa.

Inakuwaje akaumba wanaume na magovi halafu baadae aje awaambie watahiri!?
 
Ye si mjua yote? We unaweza ukaweka bomb chumbani afu ukawaambia watoto wako chezeni huko ila msiguse bomb? Hizi ni story za mababu katika kujaribu kujua shida zimetokea wapi ndo maana wamemtunga Eva Kama mwenye kosa coz ni mwanamke
Mimi huwa sipend hata nkiskia mtu anarejelea mwanamke kama chanzo cha shida na mabaya yote anayopitia.

Huwa nateseka sana moyoni.

Maisha yakikupiga, mwanamke hahusiki.
Mungu mwenye upendo wote hawezi akahukumu kizazi chote kwa kosa la mtu mmoja.
Huyo Mungu wa design hyo anamatatizo makubwa sana kwa tafsiri ya chini kabisa ya kibinadamu.

Hiyo ni dhana ya zama za giza, mwanamke alikuwa hathaminiwi.
 
Sasa Mungu muweza wa yote na mwenue ujuzi wote angeshindwa kuumba ulimwengu ambao watu hawafi na idadi haiongezeki!?

Unataka kunambia Mungu muweza wa yote na mjuzi wa yote angeshindwa kuumba dunia ya watu immortal na ikatosha kusupport maisha ya watu wote??
 
Sasa Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote alishindwa kuumba ulimwengu ambao watu wasingewezekana kuja kufa!?

Yaani hakujua kuwa hao watu wa kwanza wanacharacter ya ukaidi na wangekuja kutokumtii maagizo yake?
 
🤣Story yenyewe imeibwa Gilgamesh
 
🤣Ni coz story zimeanzishwa na wanaume
 
Jehanamu ni Israel, ni sehemu walikuwa wanachomea maiti zamani.
Maarufu kama bonde la hinnom ama Gehenna.
Kwahyo Moto wa Jehanam ni kama metaphor kurejelea hapo.

Usiteswe na hadithi za watu wa israel 🇮🇱
 
🤣Story yenyewe imeibwa Gilgamesh
Watu hawaelewi haya,
Hawajui kuwa Miungu wa Babylon kule Mungu Enlil na Enki walikuwa wanapiga story wanaambizana "na tumuumbe mtu kwa mfano wetu"
Halafu mwandishi wa bible akasahau kurekebisha hapo ili awe Mungu mmoja. Huyo Muweza wa yote mjuzi wa yote.

Watu hawajui kuwa Mungu wa maji na hekima, Mungu Enki alimwambia Atrahasis ajenge safina ili aokoe kizazi kwani angeshusha gharika.

Haya yote hawajui kuwa ni hadithi.

Sasa wao wamesoma kwa mhusika Nuhu pekee,
Ilikuwa ngumu kwangu kukubali Penguin 🐧 alitoka America akaenda mashariki ya kati kutafuta safina.
 
excellent!!! iyo biblia unayo utume humu
 
mungu alitaka kujua je mtamuamini yeye? na je makatazo yake uliyazingatia ? na je unamuabudu yeye au una mungu wako uliyemshirikisha? baada ya kufa ndio utayakuta uliyoyatenda
1. Jibu la mtoa mada kuhusu kwanini mti uliokataliwa ulikuwepo bustanini lipo hapo. Yale yote yalifanyika ili tu kujua IMANI (msimamo) wa Adam na mkewe yaani lilikuwa ni JARIBU

Kwenye majaribu ndipo wengi wanapomsaliti Mungu. Na ukishinda kwenye jaribu hapo ndipo Mungu anakukubali. Unajifunza nini kutoka kwa...

-Abrahamu kumtoa sadaka mwanae wa pekee Isaka? je angekataa ingekuwaje na baada ya kukubali ilikuwaje?
-Meshack, shedraka na Abednego kama wangekataa kuchomwa moto ingekuwaje?

2. Jibu la mtoa mada kuhusu kufa lipo hapa, kwanza kabisa ndani ya mwili wa binadamu kuna Roho ambayo shauku yake ni kumwona Baba yake (MUNGU) na kuketi pamoja naye.
-Mungu hana mwili yaani ni Roho naye huketi katika ule ulimwengu wa Roho. Ukitaka kwenda kumwona Mungu sharti mwili uuache kwanza ndipo roho yako itaenda kumwona Mungu.
- Ni kama tu ilivyo kwa wanafunzi ukitaka kwenda shuleni lazima manguo yako uyaache kwanza nyumbani then unavaa sare na kwenda shuleni.

Nitakuja kuendelea...
 
Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote aliweza vipi kuweka machaguo mabaya kama hayo?

Wewe mwanao aliye mchanga na nidhaifu unaempenda utamfungia chumbani halafu uweke sumu peupe!?
Kulikuwa na ulazima gani wa kuweka option mbaya kama hiyo!?
Sasa mtu anakwambia huyo Mungu anaupendo wote?
 
Hapo tyari umesema Mungu si mjuzi wa yote.
Na wala hana upendo.

Ukitaka kwenda kumwona Mungu sharti mwili uuache kwanza ndipo roho yako itaenda kumwona Mungu.
Yale yale ya MacKenzie.

Mkuu usije tuondolea nguvu kazi ya taifa.
 
Sasa kama tunakufa idadi inayotakiwa itafikiwa kwa style gani?
 
Maisha mazuri na sio manzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…