Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Kwa hiyo hizi aya zina maana gani?
Q9:5 Q47:4
 
Kwa hiyo hizi aya zina maana gani?
Q9:5 Q47:4
Hizo aya au namba tu?

Hiyo 9.5 anza kuisoma kuanzia 9.1 mpaka 9.15 na kuendelea utaielewa tu. Haihitaji ufafanuzi, ipo wazi. Labda kushereheshwa tu.

Hiyo ipo kwenye sura Tawba (toba).

Hata hiyo 47.4 ukianzia 47.1 ipo wazi kabisa.

Ukiisoma Qur'an bila kuikata kata inakujibu yenyewe, haina shaka.
 
Vipi msimamo wako kuhusu maulid? Maana kuna watu wanatoka povu hadi kuandaa munaqasha. Mimi sio muisilamu ila huko mitandaoni huwa nashuhudia malumbano si ya kitoto kuhusu maulidi, wengine wakisema ni ushirikina
Wanaofanya wafanye wasiofanya wasifanye. Sioni sababu kwanini wanabishana.

Mie nikikuta pilau naipiga tu, siasa zao watajuwana wenyewe.
 
Jinsi hii Mungu aliupenda Ulimwengu,Hata akamtuma Mwanae wa pekee,ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele(Yohane 3:16-18)
Safi sana, hapo ume hakikisha imani ya Kiislam kutokea ndani ya Biblia, kuwa Yesu alitumwa. Siyo Mungu mwingine aliyetumwa bali ni mtoto wa Mungu.

Wana na watoto wa Mungu kwenye biblia wako wengi sana. Haimaanishi kuwa kazaliwa na Mungu, ni kama wewe na mimi, sote ni watoto wa Mungu. Tumeumbwa nae.

Akitaka kitu husesema "kuwa" kinakuwa.

Ahsante sana.

Hata sisi Waislam tunaamini Yesu alitumwa.
 

Punguza hasira, jisome tena halafu ulipokosea jirekebishe.

Wakati unajirekebisha soma hii:

wataingia Peponi ikiwa watafanya wema.

Ingieni Peponi nyinyi na wake zenu kwa furaha. (43:70)
Na anaye fanya mema, na akaamini, akiwa mwanamume au mwanamke, tutamhuisha maisha ya furaha. (16:97)
Qur'an inawausia wale wanaume wanaowadhulumu au kuwadhulumu wanawake:


Soma zaidi Chanzo: Women in the Quran and the Sunnah
 
Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh Da Faiza.
Swali langu nilisikia kuwa kuna dua ukiomba wakati unachimba kisima basi maji hutoka ya baridi yasiyo na chumvi je unaifahamu dua hiyo?
Naomba kuifahamu pia. Natanguliza shukran
 
Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh Da Faiza.
Swali langu nilisikia kuwa kuna dua ukiomba wakati unachimba kisima basi maji hutoka ya baridi yasiyo na chumvi je unaifahamu dua hiyo?
Naomba kuifahamu pia. Natanguliza shukran
Wa Alaikum salaam. sijawahi kusikia hilo, sina ujuzi huo. Nami ntaendelea kuulizia, In shaa Allah nikipata jibu ntarudi kukufahamisha.
 

Nimeambiwa nikujibu swali hilo, nimekuleta huku kwenye uzi wangu.


Ningefurahi sana kulijibu hili swali ingekuwa huyo binti yupo kwenye ndoa na mumewe.

Ni mambo madogo sana hayo lakini yanaweza kuwa chachu ya ndoa.

Nawashauri waache uasherati, waowane kwanza, halafu kama bado tatizo linaendelea tutajitahidi liwaondokee. Wanasema "it takes two to tango".
 
Asante sana kwa kujali Faiza.

Ushauri wako nitampatia ausome mwenyewe ili nisiongeze wala kupunguza neno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…