Waislam tunaamini katika Taurati, Zaburi, Injili na Qur'an.
Tunasema kama kuna Old testament na new testament basi Qur'an ni final testament.
Unajuwa Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vingi na kuna madhehebu mengine ya Wakristo kuna vitabu vingine vya biblia hawaviamini kabisa.
Pia hakuna ubishi kuwa kuna watu wanakaa na kuamua hiki kiongezwe, hiki kiondolewe, hiki kibadilishwe. Ndiyo sababu kubwa ya kuwa na versions nyingi sana za Biblia. Kumbuka versions, siyo translations.
Sisi tunaamini kuwa humo humo kwenye mkusanyiko wa hivyo vitabu kuna maneno machahe sana yamebaki kuwa ni kweli mafundisho ya Mwenyeezi Mungu. Na yale ambayo si ya Mwenyeezi Mungu na ni mikono ya watu tu ndiyo mengi zaidi.
On the other hand, Qur'an toka imetujia miaka zaidi ya 1,400 iliyopita haijabadilishwa na haitoweza kubadilishwa kwa sababu Allah ameahidi kuilinda, cha ajabu ni kuwa katupa uwezo sisi wenyewe wa kuilinda. Hakuna kitabu leo hii duniani kilichohifadhiwa kwenye mioyo ya watu kama Qur'an. Kama kipo nijulishe. Jee, kwanini?