Nimesikitishwa sana na kitendo cha binti mdogo Niffer kujiingiza kwenye mtego wa wanaharakati uchwara na kujikuta akikwaruzana na serikali. Niffer ni mfanyabiashara anayefanya vizuri kwenye biashara yake huku akiwa bado na umri mdogo. Kukamatwa kwake na jeshi la polisi kwa tuhuma zinazomkabili ni jambo la kusikitisha sana ila hakuna namna lazima sheria ifuatwe.
Huenda Niffer na vijana wengine wengi wa umri wake hawajui kuwa kina Mange na Maria wanalipwa mamilioni na mabeberu kwa kazi ovu wanayoifanya ya kuwachonganisha wananchi na serikali. Wao bila kufikiria mara mbili wakaingia kichwakichwa kusapoti ushenzi. Labda kama Niffer hana ndoto kubwa kuhusu biashara zake basi ni sahihi kufanya hizo harakati kama za kina Mange za kuhamasisha maandamano haramu.
Vijana wajue hakuna mtu aliyewahi kushindana na serikali akashinda. Majuzi tumeona Elon Musk akimvimbia Rais Trump lakini ghafla akabadili gia angani na kuomba msamaha. Serikali sio ya kuijaribu. Serikali ina namna nyingi sana ya kumwadhibu mwananchi mtukutu. Ninamwombea Niffer aweze kusamehewa na kurudi kuendelea na shughuli zake kwa adabu.