Familia nyingine ni za ajabu sana

Mimi sina roho ya namna hiyo ndugu kusema niue mtoto mlemavu. Mtoto mlemavu hiyo ni scenario tofauti na ya hawa majamaa.
Wewe una uhakika gani kwamba sio walemavu wa akili wewe ndio uliewazaa? Wewe ndie mama yao? Wewe ndie unaewafahamu tangu wanazaliwa walikuaje wakaishi mazingira gani?

Hizo ni assumption zako Ila mimi ninakaa upande wa huyo mama ukitaka kujua uchungu wa mtoto/watoto nenda kamuulize mama Msuya anajisikiaje sasa hivi bora ufuge hata chizi ndani Ila ni mwanao
 
Hapa ninavyosoma hii thread yako, inaita simu ya baba mdogo. Yuko kwenye 50s hapo. Ila kila week lazima atapiga kuomba elfu kumi/ishirini.

Bado ana nguvu kabisa za kufanya kazi, lakini naamini akili yake ameshaielekeza kwenye kuomba pesa ya kula. Niliwahi kumshauri walau aseme ni biashara gani ndogo anaweza kufanya imuingizie kipato sisi kama watoto wa kaka yake tumchangie, lakini anapiga chenga.

Somo: Kuna vitu vingine tunavilea lakini ndo vinaturudisha nyuma. Kumhurumia mtu ambaye hajihurumii ni kupoteza muda. Tusaidiane pale inapobidi na sio kila wakati.
 
Hakuna mtu anachagua familia ya kuzaliwa, muhimu mshukuru Mungu kwa familia yako....alafu usiache kusaidia pale unapoona unaweza hasa kwa mzazi wako aliyebaki.....Mungu atakulipa.

Hao ndugu zako inawezekana wamefungwa ufahamu (akili) kichawi au walijifunga wenyewe bila kujua, usiache kuombea familia yenu tena kwa mzigo sana....ili watoto wako wasije kurithi tabia za baba zake wakubwa.
 
usichoke kusaidia ndugu zako hasa mzazi wako maisha ni duara na pia maisha ni fumbo.. nakuambia usichoko usichoke huijui kesho yako
You nailed it boss...👊👊👊

..kijana asiache kabisa kumsaidia mzazi wake, tena awe makini sana kwenye eneo hilo.
 
Mwisho wa siku huyo mama yetu ana shida kidogo kwenye malezi ya wanawe.
Tatizo liko hapa nashangaa watu hawasemi. Chanzo cha matatizo yote ni mama, tumeambiwa mzee wake alikuwa mpambanaji hivyo muda mwingi aliutumia kutafuta familia yake iishi vizuri.
Sasa hawa walevi na wazinzi ni zao la mapungufu ya mama yao ambaye bado anawaendekeza.
Baba hakuwa na asili ya uvivu, umalaya na ulevi ni tabia za mama hizo ambaye anaziona za kawaida anachukulia poa. Ndio hao mama akiwepo watoto shule ya msingi wanarudi usiku kutoka disko vumbi, baba akiwepo jioni wanarudi ndani wamejikunyata hawana raha wanaona baba mkorofi.

Kwenye familia bora mama awe mkali kuliko baba, sijawahi ona familia ya mama mkali inapoteana.
 
Hakika mkuu, mimi nilisummarise tu ila wewe umemaliza kila kitu.
 
Wewe ndio mpuuzi, nilijua utatoa ushauri wa maana. Kwa hiyo asimtumie mama yake hela? Unawajua akina mama wewe? Hata akituma elfu tano bado atakula na hao watoto wake wavivu na mwisho wa siku atapata presha afe kwa kukosa chakula cha kulisha wake
Nimesema atume hela zilizo ndani ya uwezoo wake. Uwe unasoma msg yangu kabla hujanywa mataputapu kilabuni.
 
Sanaa. Kuna ndugu yangu watoto watatu wote sio wake. Mhaya wa kwetu alijichanganya kwa mzaramu. Huyo mwanamke ni mshenzi, mshenzi na sasa ndugu mwenyewe karogwa akarogeka ni pimbi mbele ya mkewe. Ndugu tumeshaacha.

Mhaya wa wapi huyo?? Kweli wazaramo wawazidi akili nyie mbona kwenye malimbwata ndio wenyewe!!!! Hebu shirikisheni mabibi zenu mnamchomoa faster kwenye iko kifungo
 
Mhaya wa wapi huyo?? Kweli wazaramo wawazidi akili nyie mbona kwenye malimbwata ndio wenyewe!!!! Hebu shirikisheni mabibi zenu mnamchomoa faster kwenye iko kifungo
Ana miaka 48. Tatizo tunaweza kumpoteza akapata mshtuko akafariki hasa akielezwa ukweli analea watoto wa wanaume wenzake. Maana ni mpole na muungwa kupitiliza. Ndiyo maana tumeona tuache tu. Ingekua kuua sio dhambi yule mwanamke mimi ningemuua.
 
Ana miaka 48. Tatizo tunaweza kumpoteza akapata mshtuko akafariki hasa akielezwa ukweli analea watoto wa wanaume wenzake. Maana ni mpole na muungwa kupitiliza. Ndiyo maana tumeona tuache tu. Ingekua kuua sio dhambi yule mwanamke mimi ningemuua.

Nyie mlijuaje km sio wake mliwapima DNA au vipimo vya macho mmetumia??
 
Nyie mlijuaje km sio wake mliwapima DNA au vipimo vya macho mmetumia??
Wabibi wa Kanyengereko wanajua wanachokizungumza omwana. Na zaidi kuna siku huyo wa pili almanusura aropoke stori kamili. Alishaanza baba leo tumeenda kwa baba yake na...mama mtu akamuwahi kwa karipio kali na kuipotezea stori.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…