Familia nyingine ni za ajabu sana

Familia nyingine ni za ajabu sana

Kuna familia zingine zinashangaza na zinakatisha tamaa sana.

Sisi kwenye familia yetu tumezaliwa watoto 9 wakiume tupo 6 na wakike wa 3 na uzao wetu umekaa hv kuna kaka zangu wakubwa wa 3 waliozaliwa miaka ya 70 then wanafuata dada 3 waliozaliwa miaka ya 80 halafu ndio sisi tena wakiume wa 3 wa mwisho tuliozaliwa miaka ya 90.

Kiukweli tulilelewa vzr sana na atukuwahi kushinda wala kulala njaa japo mzee alikuwa anafanya kazi ya kawaida sana ila alijitahidi kuhakikisha watoto wake tunalelewa vzr japo kwenye swala la kielimu atukufika mbali sana.

Mzee alijitahidi sana kuwekeza nguvu zake kwa hao kaka zetu wakubwa miaka ya 90 kipindi sisi wengine bado tupo wadogo sana ili wao ndio waje kuwa msaada kwetu.

Shida ni kuwa kaka zangu wawili walikuwa ni watu wa starehe na pombe mwisho wa wakafukuzwa kazi. Mmoja aliiba pesa kiac cha sh milioni 2 kazini kwake akakimbilia nchi jirani ya kenya hiyo ni milioni 2 miaka ya 90 haikuwa pesa ndogo, huko alikokwenda pia aliendekeza starehe kama kawaida mwisho pesa zote zilikwisha na mbaya zaidi aliugua sana ikabidi tena mzee aende kumfata huko alipokuwa,

na kaka yangu mwingine alienda mbali zaidi kufikia hatua ya kuingia chumbani kwa mzee na kuiba kiac kikubwa cha pesa na kukimbilia uganda,
Japo nilikuwa mtoto ila sikushindwa kujua maumivu aliokuwa nayo mzee, kwa mara ya kwanza nikamuona mzee akitokwa na machozi mbele yangu aisee niliumia sana.

Mwamba huko uganda akawa mtu wa starehe sana ni mwendo wa pombe na wanawake mwisho pesa zilikwisha akarudi tanzania akawa anakuja nyumbani kwa siri, Siku moja usiku muda wa saa 8 baba aliskia kama mchakacho akachukua panga akakutana na mtu anatoka koridoni mzee akataka kumkata panga akijua kuwa ni mwizi kwa bahati nzuri bro akawahi kutoa sauti ndio mshua akashusha panga.

Kama mjuavyo wazazi ni watu wenye huruma akamsamehe mambo yakaisha japo mshua akuwa na upendo nae tena.

Imepita miaka kadhaa wakaja na project kwa mzee hiyo ilikuwa 2008 mzee akaona sio mbaya akawapa tena mtaji wakiwa wawili rejea nyuma hao wote walishaiba pesa katika vipindi tofauti.

Ila cha kusikitisha hakuna cha maana walichofanya kumbuka hapo nguvu ya mzee katika kufanya kazi imeshaanza kupungua halafu akikumbuka watoto wake wakubwa ambao aliwekeza kwao amna cha maana walichofanya zaidi ya kumtia tu hasara ilifikia stage mpaka sisi wadogo mshua akawa anatuchukia kwa makosa ya kaka zetu wale wakubwa japo sisi bado ni watoto wadogo na tunasoma ila mara nyingi alikuwa anamwambia mama unaona watoto wako hawa wadogo pia wakikua watakuwa kama kaka zao aisee hilo jambo lilikuwa linaniumiza sana.

Ila nachoshukuru kati ya wale kaka zangu wakubwa watatu kuna mmoja yeye alipomaliza shule alienda dar miaka ya 2000 alihustle ila kiac alifanikiwa na ndio huyo akawa anampa mshua back up pale hali inapokuwa mbaya.

Kuna kipindi huyo bro aliyumba kiuchumi na mshua alikuwa mgonjwa na kama mjuavyo familia nyingi za kimaskini ni mpaka mzee atoke ndio familia ipate kula bac mshua baada ya kuwa katika mazingira yale alianza kupata stress akikumbuka nguvu aliyowekeza kwa vijana wake wakubwa ilivyopotea bure mpaka sasa familia aina chakula na yeye ambae ndio mtafutaji yupo chini bac mzee alianza kudhoofu sana hiyo ilikuwa 2011 kipindi hiko mi nipo form2 bac kuyumba kwa mzee vile ilipelekea tukakosa ada bac nikakaa home.

○Mzee maradhi na stress vilimuandama sana mwisho akalazwa hospitali kwa bahati mbaya akafariki. Bac tukaanza namna ya kutafuta mawasiliano ya wale kaka zangu wawili watukutu maana walikuwa wilaya nyingine kipindi hiko tuliwapata aisee jamaa wamekuja msibani hawana hata mia yani wamechakaa kinoma. Bac yule bro ambae yupo dar alijitahidi kwa nguvu zake mwenyewe akamiliza msiba fresh.

○Na ndio anaetoa msaada mkubwa kumlisha mama toka mzee amefariki yeye ndio tegemeo la familia maana dada zangu pia maisha yao ni tabu tu na wote hawajaolewa mpaka sasa.
○Wanaishi kwa kuunga unga tu aisee kuna baadhi ya familia ukizaliwa ni shida sana.

Cha kusikitisha kingine ni kwamba wale kaka zangu wawili mpaka leo hii mmoja ana miaka 50 mwingine ana miaka 45 bado wapo wapo tu wakipata pesa ni pombe na wanawake awana wake wala watoto na mbaya zaidi wao wote wamerudi home wanaishi na mama lakini awajishughulishi na chochote wamekaa tu wanakula kwa mgongo wa bi mkubwa kiukweli kuna familia nyingine zinakera sana.

Ebu fikiria vijana wakubwa wawili miaka 40+ wanashindwa kumlisha mama yao nao wamekaa wanalishwa, just imagine mpaka umeme wa elfu 2 unapigiwa simu dar wakati home kuna vijana wawili wakubwa wao wakipata pesa zao wanaenda kuishi guest mpaka wahakikshe hizo pesa zimeisha ndio wanarudi home halafu wanasubili sisi ndio tuwalishe kifupi tu ni kwamba hao ma bro washakula pesa za watu nyingi na hawajawahi kurudisha.
na kipindi nipo mkoa nilikuwa najaribu kuwashauri ila nilikuwa naishia kukabwa na kutaka kupigwa

Wengine ndio tumepata ajira jana tu hata kujipanga bado lakini simu za mzazi zimekuwa nyingi wakati pale home kuna vijana wakubwa hawataki kujishughulisha na mbaya zaidi mama hata kuwashauri wanae hawezi sometime wanakuja kukaa hapo na wanawake zao halafu bado pesa ya kula sisi ndio tunatafuta ukimtumia mama nae anakaa anakula na wanae, yani wanaenda kuzurura huko wakirudi wanakuta mama kawaachia msosi wanakula wanaondoka tena wanaenda kuzurura wakirudi usiku tena unakuta bi mkubwa kawaachia msosi wanakula wanaenda kulala kesho tena hivohivo jamani halafu fikirieni watu wanaofanya hivo ni watu wenye miaka 40+

Na pesa ya matumizi ikiisha bi mkubwa anawatafuta tena mnaangaika mkipata mnatuma bi mkubwa anaendelea kula na wanae halafu mbaya zaidi nayeye hata awashauri wanae ukimueleza awashauri watoto wake pia wajishughulishe anakwambia sasa kama hawa kaka zako hawana pesa wafanyeje utadhani sisi ndio tunahela wakati tunaangaika ili mama apate kula wengine hata mambo ya wanawake tulishasahau kutokana na majukumu ya kifamilia jinsi yanavyotubana.
Lakini unakuta hapo kuna baadhi ya ndugu zako tena wengine wangeweza hata kukuzaa wao wamekaa wanasubili wewe uhangaike uwatumie pesa wao wale.

Hapa toka jana mama ameshaanza kusumbua anahitaji pesa ya matumizi na sio muda mrefu nilimtumia laki moja na bro school bus yake pia iliangukiwa na mti ipo right off namimi na saiz bado mambo yangu ayajakaa sawa.
Halafu fikiria hapo home kuna wazee wazima ambao hata sio walemavu wamekaa wanasubili uhangaike utume pesa wale.

Aisee kuna familia nyingine zinakatisha tamaa sana kama ni laaana bac hii ya familia yangu imezidi mpaka najuta ni kwanini nilizaliwa na ndugu kama hawa, jamani nimechoka just imagine mpaka umeme wa elfu mbili mama anakupigia simu dar.
Pole, ndio maisha yetu haya.
 
Kama mngelelewa vizuri, hao Kaka zako wasingekuwa Wezi na walevi.

Tofautisha Kulea na kufugwa!
Kumlisha MTU sio kumlea kwani hata Mnyama unaweza kumpa chakula.
Kuishi na mtoto na kumfunza ndio kumlea.
Malezi ya Watoto kama yakifanyika vizuri mtoto hawezi kuwa mwizi wala chapombe.

Mengine, poleni Sana. Hayo ndio Maisha.
 
Nieleweshe mkuu

Unaweza kumzaa mtoto lakini usiwe na bond naye.
Au mzazi anaweza akakuzaa lakini usiwe na bond naye. Yaani humpendi(hakuna nguvu ya ndani inayokusukuma kuwa karibu naye).
Hicho ndio wengi wanakosa. Na hiyo Ipo hivyohivyo tuu. Huwezi ilazimisha.

Kulea mzazi sio lazima Pesa Bali inahitaji hiyo bond.
Ni kama bond ya Mama na mtoto, ambayo Ipo tofauti na bond ya Baba na Mtoto.

Uwe umebarikiwa sasa uzae Watoto watani alafu watatu au wanne wawe na bond na wewe Hii Dunia utaenjoy Mno. Hata wasipokuwa na Pesa. Upendo unanguvu kuliko Pesa.

Wazazi lazima wamwombe Mungu bahati ya kuwaunganisha(bonding) na watoto wao.
Vinginevyo ndio haya yanayotokea katika familia zetu nyingi.

Yaani unakuta mtoto mnamlazimisha kujihusisha na Mama yake utadhani hakumzaa, sio kama anafanya Makusudi nop! Ni kwamba hakuna muunganiko baina Yao. Huwezi lazimisha muunganiko Kwa nyoyo ambazo hazijaungana
 
Aya jidanganye uyakimbie na mama yao,uone mama yao atakavyokumaindi kuwa unamtesea wanawe

Tia sumu yafe
Hahahaa 😂😂we Jamaa nimekukubali,Dah! Mama ukute ni ngumu sana kuishii bila hao mafalaa....so ukimletea swagaa za kumtenganisha naoo ni vita hatakii.

In Short familia zetu ni mtihani sana hasa ukiwa na utu kama mleta madaa.Ukikaa vibaya hao wanakutoa rohooo au kukupiga tukio hata wew.
 
Kama bi mkubwa anawatetea hao jamaa usimtumie kumi mwambie hata wewe huna.
Kwa nini uumie kwa uungwana wako?
Nimegundua ukiwa muungwana sana kwenye familia zetu unafanywa mjinga kama hivi.
Achana nao mzee pambana na Maisha yako na hakuna wa kukulaani sababu mko wengi kwa nini uumie wewe?
Mwambie aombe kwa mzunguko Kila mmoja amtunze mwezi mmoja baada ya miezi nane ndio zamu yako itafuata.
Umenishauri jambo la msingi sana
 
Unaambiwa Bwana Mungu huwapatiliza Watoto wa Uzao Mwovu hadi kizazi cha Nne.

Kama wewe unapata pesa kwa kudhulum endelea kula bata ila kuna uzao wako utalipa hiyo gharama ikiwa na wewe uko hai ili uchungu ukurudie.
Hakika unachosema. Watu wengi huwa hawaamini,,lkn huo ndio ukweli. Kwa hiyo ni jukumu letu kutenda mema kwa ajili ya vizazi vyetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika unachosema. Watu wengi huwa hawaamini,,lkn huo ndio ukweli. Kwa hiyo ni jukumu letu kutenda mema kwa ajili ya vizazi vyetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabisa yaani nimeona ndugu na familia za Uongozi wa Juu ktk Taifa hili jinsi wanavyopitia mambo mazito na magumu.

Ukiwaona ni mawaziri na wakurugenzi kwenyw vyombo nyeti huku kwenye nyumba zao zinawaka moto.

I learned it must be karma.
 
Nilitaka nisicomment nisome tu huu Uzi Ila wewe ni mtu wa ajabu kweli kweli Yaani majitu ya 40+ yanaka tu na huyu Dogo anakqbwa na maisha ndo awalishe eti Ana Roho mbaya mbona usiwaseme hao wahuni malofa yasiyofanya kazi ndo yanatoho mbaya??Dogo katoa nyongo aheshimiwe
 
Pole mkuu, hauko peke Yako na jambo hilo sio unique to your family.

Familia nyingi za kibongo hayo ndo maisha wanayoishi. Kizazi chetu hiki we pishana na watu tu mtaani, ila ukipewa uishi nao utakimbia. Wengi tumevurugwa, hatujitambui, wabinafsi na hatuna value Kwa familia na jamii zetu.

Kuna anguko kubwa sana la maadili, yaani kukuta familia Ina watoto at least 3 afu ukute wanajitambua hiyo ni NEEMA kubwa sana. Wengi wetu hata personal management imetushinda.

Umasikini na utegemezi ndio main reason why most families remain poor for decades. Unazaliwa na mzazi masikini, hunakosa malezi bora ili uje ujitegemee, na wewe unaanzisha familia yenye changamoto kama za wazazi wako na mnyororo wa umasikini unaendelea.

Kuna ushauri umetolewa na wadau naomba uuzingatie. Maisha ni maamuzi. Ndg zako wameanua kuishi maisha yao na unaona hakuna aliekufa na maisha yao yanasonga na wala hawajali. Wewe ndo unajiona muungwana na kutaka kubadiri fate ya maisha ambayo hata wazazi wako wameshindwa.

Unalo jukumu moja kuu na la msingi. Pambana anzisha familia Yako, Jenga misingi Yako ili usije kupata familia kama ya wazazi wako. Achana na hao wengine, ni watu wazima wataishi tu hata usipotuma iyo laki moja Yako Kila mwezi.

Life is all about decisions you make
 
Back
Top Bottom