Mimi niliacha chuo alafu sikuiambia familia sababu kubwa nilikuwa nasumbuliwa na msongo wa mawazo kwahiyo miwili unataka kubaki chuo akili haitaki nyumbani wanajua Niko chuoni na napokea bumu langu kumbe mimi Niko mtaani Arusha Dunia inanifunza nilikonda mpaka nokawa kama msomali nilipitia maisha ambayo hata mdg zangu hawayajui mwisho wa siku walijua kama nimeacha chuo niliamua tu nirudi nyumbani nilisemwa,tengwa,fedheheshwa,tukanwa kila aina la lawama mpaka sasa hivi kaka yangu hatupatani maana alionesha chuki ya wazi wazi kwangu ila ukweli kipindi akili haikuwa sawa nahisi hata ningejiua Kosa nililofanya ni kuondoka chuoni bila kutoa taarifa yoyote japokuwa familia inajuaga nilidisco chuo