Familia tunahisi kijana ametuongopea kuwa amehitimu udsm 2026,

Familia tunahisi kijana ametuongopea kuwa amehitimu udsm 2026,

Alikua mtaani tu, jamaa mmoja kampanga ndio anajifanya mwalimu..... anapiga simu kupitia huyo fake teacher, hela inatumwa kwa namba ya huyo fake teacher.

Kuna watu wana roho mbaya sana sijui angekua ndugu yake angefanya hivyo pia.
Kuna watu mbele ya pesa roho nzuri mkiwa nayo nyinyi inatosha aibu mtaona nyie
 
Ukute alidisco.

Dogo alidisco chuo na hakutoa taarifa, tukawa tunalipia ada vizuri mpaka mwisho na hakuwa na mkopo hivyo gharama ilikuwa kubwa. Kamaliza naye akatwambia haina haja ya sie kwenda kwenye graduation.

Akaazima joho la mwenzake akapigia picha kisha akatutumia. Kimbembe kikaja kwenye kutafutiwa kazi, kila mchongo tunaopanga haendi interview kumbe vyeti hana. Kakazana yeye kuajiriwa hataki anataka kujiajiri. Basi atueleze anataka kujiajiri kwenye nini kila siku ana business plan mpya. Tukagundua hapa hamna wa kujiajiri tukomae tu aajiriwe. Ndio rafiki yake kuja kutueleza ukweli baada ya kuona tunahangaika sana.

Now yupo yupo tu haeleweki na umri unazidi kusonga na hana mishe ya maana. Kabakia kulaumu tu kila mtu.
Sasa analaumu vipi kwa ujinga wake mwenyewe? Kuna jamaa nilisoma nae ilimkuta kama hiyo alidisco UDOM akatafuta nafasi chuo kingine kimya kimya bila kwao kujua na mwaka wa masomo ulivyoanza akawa analipa ada anazopewa na wazazi na aligraduate. Siku ya mahafali ndio wazazi wakajua alidisco UDOM baada ya kufanya mahafali chuo kingine na sio Udom.
 
Ushauri wangu kwa wazazi hasa wale mnaolipia kila kitu epukeni sana kutoa cash kwa vijana wengi. Umri wa ujana una vishawishi vingi sana nikikumbuka nilitoaga 100K kwenye ada ule mziki wa kuirudisha siji sahau milele.

Baadhi yao wakipewa pesa wanatumia kuhonga, kamari, starehe na mambo mengine ambayo sio ya msingi. Haya nayasema kwa shuhuda za wadau vyuoni.
 
Sasa analaumu vipi kwa ujinga wake mwenyewe?
Acha tu, anadai tulimnyima mtaji, wakati mama alimpa akaishia kula. Sasa acha afanye kazi atafute mtaji mwenyewe aone kama ni rahisi.
Kuna jamaa nilisoma nae ilimkuta kama hiyo alidisco UDOM akatafuta nafasi chuo kingine kimya kimya bila kwao kujua na mwaka wa masomo ulivyoanza akawa analipa ada anazopewa na wazazi na aligraduate. Siku ya mahafali ndio wazazi wakajua alidisco UDOM baada ya kufanya mahafali chuo kingine na sio Udom.
Bora huyu alijiongeza
 
Kama mlikuwa hamumlipii ada wala kufuatilia maisha yake ya chuo ikiwemo kumsaidia hapa na pale mnakosa uhalali wa kuhoji chochote kinachohusu elimu yake. Watoto wengi hasa wa kiume wakishamaliza form 6 ni kama wametelekezwa.
 
Dunia ina mambo mengi hasa watu wanaoishi ndani yake....
 
Kuna vitu huwa unabidi uwache hivyo vilivyo maana kwa upande huu tuluiokaa twaweza sema jambo ambalo tukaona mtu ana hatia, na kama tulikaa upande wake twaweza sema huyu mtu alikuwa shujaa katika maamuzi yake.

Maisha nikujifinza na kila siku tuko shuleni kujifunza kipitia sisi wenyewe au kupitia wenzetu.
 
Acha tu, anadai tulimnyima mtaji, wakati mama alimpa akaishia kula. Sasa acha afanye kazi atafute mtaji mwenyewe aone kama ni rahisi.

Bora huyu alijiongeza
Huyo anadeka anadhani maisha yatamdekeza awazi kuna leo na kesho na anaona kuwa msaada ni haki yake. Mmefanya vizuri kumuacha atafute mtaji mwenyewe ili akipata awe na nidhamu.
 
Huyo anadeka anadhani maisha yatamdekeza awazi kuna leo na kesho na anaona kuwa msaada ni haki yake. Mmefanya vizuri kumuacha atafute mtaji mwenyewe ili akipata awe na nidhamu.
Sio siri tulimdekeza, kalikuwa bright sana shule hivyo hata hatukuwa na wazo la kufuatilia maendeleo yake chuo kwakuwa tulimwamini. Na hatukutaka aje aanze kuteseka kulipia mkopo wa serikali akiajiriwa au kujiajiri. Kumbe akenda kuzuzuka chuo hata vipindi akawa hahudhurii
 
Mind your own business,mtu aliyemaliza chuo Ni mtu mzima
 
Mimi niliacha chuo alafu sikuiambia familia sababu kubwa nilikuwa nasumbuliwa na msongo wa mawazo kwahiyo miwili unataka kubaki chuo akili haitaki nyumbani wanajua Niko chuoni na napokea bumu langu kumbe mimi Niko mtaani Arusha Dunia inanifunza nilikonda mpaka nokawa kama msomali nilipitia maisha ambayo hata mdg zangu hawayajui mwisho wa siku walijua kama nimeacha chuo niliamua tu nirudi nyumbani nilisemwa,tengwa,fedheheshwa,tukanwa kila aina la lawama mpaka sasa hivi kaka yangu hatupatani maana alionesha chuki ya wazi wazi kwangu ila ukweli kipindi akili haikuwa sawa nahisi hata ningejiua Kosa nililofanya ni kuondoka chuoni bila kutoa taarifa yoyote japokuwa familia inajuaga nilidisco chuo
 
Sio siri tulimdekeza, kalikuwa bright sana shule hivyo hata hatukuwa na wazo la kufuatilia maendeleo yake chuo kwakuwa tulimwamini. Na hatukutaka aje aanze kuteseka kulipia mkopo wa serikali akiajiriwa au kujiajiri. Kumbe akenda kuzuzuka chuo hata vipindi akawa hahudhurii
Na mtu wa hivyo haaminiki tena kwenye familia hasa kwenye ishu ya hela
 
Back
Top Bottom