Familia tunahisi kijana ametuongopea kuwa amehitimu udsm 2026,

Familia tunahisi kijana ametuongopea kuwa amehitimu udsm 2026,

Ukute alidisco.

Dogo alidisco chuo na hakutoa taarifa, tukawa tunalipia ada vizuri mpaka mwisho na hakuwa na mkopo hivyo gharama ilikuwa kubwa. Kamaliza naye akatwambia haina haja ya sie kwenda kwenye graduation.

Akaazima joho la mwenzake akapigia picha kisha akatutumia. Kimbembe kikaja kwenye kutafutiwa kazi, kila mchongo tunaopanga haendi interview kumbe vyeti hana. Kakazana yeye kuajiriwa hataki anataka kujiajiri. Basi atueleze anataka kujiajiri kwenye nini kila siku ana business plan mpya. Tukagundua hapa hamna wa kujiajiri tukomae tu aajiriwe. Ndio rafiki yake kuja kutueleza ukweli baada ya kuona tunahangaika sana.

Now yupo yupo tu haeleweki na umri unazidi kusonga na hana mishe ya maana. Kabakia kulaumu tu kila mtu.
 
habari ya wakat huu wadau? kama tittle inavyojieleza nina mjomba wangu ambae alikuwa akisoma udsm na mwaka huu ndio alitakiwa kuhitimu lakin kama familia tunashindwa kuelewa kama kweli kahitimu au anaidanganya familia, sababu aligoma kuonesha matokeo yake ya mwisho pia aligoma ndugu yoyote asiende kwenye mahafari hayo yaliyo fanyika october 15!

Wadau nilikuwa naomba mdau yoyote humu mwenye kitabu cha wahitimu udsm 2026 anisaidie kwenye website udsm sijafanikiwa kuona, ili niweze kutazama jina lake kama kweli ni miongoni mwa wahitimu!
Mna uhakika alikuwa anasoma UDSM? Au alikuwa anakaa UDSM?
 
Hiyo imemkuta mdogo wa rafiki yangu,alidanganya anasoma bcom makarere university, mzee wake akawa anatuma ada na matumizi mengine..kumbe dogo starehe za Kampala zilimchanganya aka disco chuo siku nyingi.
Saivi yupo tu huku bongo anakula vumbi.
 
Wakati nipo Chuo nilikutana na mwana kutoka Kijijini kaja kusoma ila kozi tofauti,tuna undugu fulani kwenye ukoo jamaa akawapa taarifa wazazi wake kuwa amekutana na mimi,wazazi wakafurahi. Baadae nikaona jamaa ana tabia tofauti akajiingiza kwenye mambo ya umaarufu chuoni nikawa nampotezea sababu sio pigo zangu.

Imefika mwaka wa tatu kuna msala walifanya hizi issue za mademu na lecturers, wakampiga Disco kwao hakutoa taarifa,mimi nikapotezea nikasema hayanihusu. Graduu imefika kuna mtu kule kijijini akawa anajua akamwambia Dingi yake kuwa Ijumaa anaenda kwenye Graduu yangu,Dingi akapaniki mbona fulani hajatupa taarifa,kumtafuta akawaambia msiwaze kila kitu kipo fresh.

Dingi yake akaanza kufuatilia akawa anapata taarifa mkanganyiko ikabidi anitafute na kuniomba sana nimmwambia ukweli. Nikamchana kuwa jamaa kadisco ongea nae vizuri au nenda chuoni,Dingi akaenda Chuo akakuta jamaa kadisco tangu Semister ya kwanza mwaka wa tatu.
 
habari ya wakat huu wadau? kama tittle inavyojieleza nina mjomba wangu ambae alikuwa akisoma udsm na mwaka huu ndio alitakiwa kuhitimu lakin kama familia tunashindwa kuelewa kama kweli kahitimu au anaidanganya familia, sababu aligoma kuonesha matokeo yake ya mwisho pia aligoma ndugu yoyote asiende kwenye mahafari hayo yaliyo fanyika october 15!

Wadau nilikuwa naomba mdau yoyote humu mwenye kitabu cha wahitimu udsm 2026 anisaidie kwenye website udsm sijafanikiwa kuona, ili niweze kutazama jina lake kama kweli ni miongoni mwa wahitimu!
Ulikuwa ukimlipia Ada au ni umbea tu kutaka kufuatilia mambo ya watu
 
Back
Top Bottom