Familia tunahisi kijana ametuongopea kuwa amehitimu udsm 2026,

Familia tunahisi kijana ametuongopea kuwa amehitimu udsm 2026,

habari ya wakat huu wadau? kama tittle inavyojieleza nina mjomba wangu ambae alikuwa akisoma udsm na mwaka huu ndio alitakiwa kuhitimu lakin kama familia tunashindwa kuelewa kama kweli kahitimu au anaidanganya familia, sababu aligoma kuonesha matokeo yake ya mwisho pia aligoma ndugu yoyote asiende kwenye mahafari hayo yaliyo fanyika october 15!

Wadau nilikuwa naomba mdau yoyote humu mwenye kitabu cha wahitimu udsm 2026 anisaidie kwenye website udsm sijafanikiwa kuona, ili niweze kutazama jina lake kama kweli ni miongoni mwa wahitimu!
Mjomba ktk ubora wako!
 
Matokeo hutapewa believe me...
Kama hujui. Basi jua kuwa hata mwanachuo akiumwa malaria. Dean of students anatakiwa kujua.

Unaumwa, umefiwa , unahairisha mwaka au unachangamoto yoyote nje ya masomo .unatakiwa kureport kwa dean.
Sio lecturer au principal.

Yaan uwepo wako chuoni ni lazima dean aujue.
Na usipokuwepo lazima ajue kuwa nilianza na wanafunzi 100. Ila sasa nina 99 kwa sababu mmoja hayuko kwa sababu hii.

kwahiyo reason ambayo kama dogo hajagraduate basi dean anayo kwa records zake.
 
Mtu anayehitimu Chuo Kikuu nimtu mzima, na hawajibiki kwa mtu yoyote ila yeye na maisha yake tu! Ndio maana matokeo hayatumwi kwa wazazi au walezi bali kwake.

Watanzania tuache kulea watu wazima! Hii ya mtu mzima na bado mnahitaji kujua kama amehitimu au la ndio inazaa watu tegemezi! Kama mlikopesha mdaini Fullstop!
 
habari ya wakat huu wadau? kama tittle inavyojieleza nina mjomba wangu ambae alikuwa akisoma udsm na mwaka huu ndio alitakiwa kuhitimu lakin kama familia tunashindwa kuelewa kama kweli kahitimu au anaidanganya familia, sababu aligoma kuonesha matokeo yake ya mwisho pia aligoma ndugu yoyote asiende kwenye mahafari hayo yaliyo fanyika october 15!

Wadau nilikuwa naomba mdau yoyote humu mwenye kitabu cha wahitimu udsm 2026 anisaidie kwenye website udsm sijafanikiwa kuona, ili niweze kutazama jina lake kama kweli ni miongoni mwa wahitimu!
Amin amin nakuambia hao ma dropout wanafanyaga vizuri sana mtaani!
 
Back
Top Bottom