Nina Ma mdogo wangu aliingia mkenge huo huo kwa mtoto wa mjini muhuni, mwamba aliingia na gia kamaliza Mlimani halafu HB basi kapagawa, akaja kumkatalia Dr aliyesoma Muhimbili. Basi akawa anawaambia amemaliza anatafuta sehemu atleast ya kujishikiza akisubiria mchongo wa kudumu. Mwamba akawa anaishi mpaka kwa babu huku ma mdogo akawa anamtoa kidogo akiwa na changamoto, akampa mimba ma mdogo, baadae akamwacha akaenda kuoa mwanamke mwengine mwenye hela.Baada ya hapo akili zikamrudia ma mdogo kupeleleza kumbe mwamba ni muongo, mdananda na kingereza chake cha kuungaunga anawaaminisha kasoma Mlimani.Baadae akaachwa ,akawa anaungaunga, halafu si unajua ukizoea kulelewa na wanawake, fighting spirit ile ya kama mwanaume unaiangamiza, yupo kila siku anataka kurudi kwa Ma Mdogo.