Familia zina siri kubwa, mwanasheria msibani: Mwanasheria kazua gunzo msibani akisoma mirathi, watu tulishangaa sana

Watanzania tunapenda umbea.

Wewe kama nani kwenye hiyo familia mpaka ualikwe inapofunguliwa mirathi yao?

Nijuavyo hayo ni mambo private
 
Kuna jamaa mtoto wao wa kwanza alikuwa sio wake lakini waliitunza siri hiyo hata ndugu ni wachache tu ndio walijua na mtoto hakujua kabisa na jamaa hakumbagua hata kidogo na kwa bahati nzuri wakati jamaa anaumwa yule mtoto ndiye aliyekuwa akijitoa sana akiamini anamuhudumia baba yake lakini alipofariki katika wosia wa marehemu uliosomwa ndio ulibainisha kwamba yule mtoto sio wa marehemu,kwakweli mtoto aligalagala kwa kilio kikali na kumlaumu sana mama yake kwanini hakumwambia ukweli huo miaka yote.
Mwishoni mwa uhai wake jamaa baada ya kuona huyo mtoto ambaye sio mwanawe anamsaidia kuliko hao wanawe alijaribu kutaka kumjumuisha kwenye mirathi lakini ilishindikana kwa sababu ule wosia wa mahakamani ulibaki kama ulivyo hivyo kumaanisha wenyewe ndio wosia halisi na maelezo yaliotolewa kienyeji nyumbani hayakuzingatiwa.
 
Kikulacho kinguoni mwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…