Fanya haya endapo basi ulilomo ghafla linaanza kupinduka…

Ajali haina kinga.
Kuna jamaa, sijui kama ndio alikuwa macho zaidi ya wengine au la, maana basi lilipoanza kupata mushkeli, yeye pekee ndiye aliyechoropoka dirishani, bahati mbaya akaishia kulaliwa na basi na kupoteza maisha, hakuna mwingine yeyote aliyefariki.
 
Sijui kama umeishawahi kupata ajali kama hujawahi nikwambie TU kuwa walioko nje ndio hujua Nini kimetokea
Wewe akili itakurudia gari ikiwa imeshamaliza swala lake la kupinduka.

Muhimu funga mkanda Kisha muombe Mungu mfike salama
Katika comments za maana ni pamoja na hii kuliko hata ushauri wa mtoa mada!

Kwenye msukosuko wa kupinduka hauwezi kukumbuka kufunga ama kufungua mkanda ili kujihami eti sijui kulala chini!

Ukubwa wowote wa ajali huchukua muda mfupi sana kiasi ambacho binadamu hauwezi kujiweka sawa kifikira!

Nilishapata ajali za hovyo kabisa, gari kuacha njia na kwenda kuparamia mti live pamoja na ajali zinginezo za aina hiyo, hivyo nina uzoefu.

Pamoja na kudra za Mwenyezi Mungu, "Mkanda" ni kinga madhubuti sana mtu asije akaudharau, kifupi ni ngao mahsusi ya ajali, mimi umeniponya na kunikinga mara zote.

Na ajali ya mwisho ilikuwa ni mwaka jana, gari kugeuka chapati, lakini mimi na dereva wangu tulitoka tukijikunguta vumbi tu na wala hosipitali hatukukanyaga.
 
Hivi unajua jinsi uvungu wa basi ulivyo kweli ama unaongea nadharia tu.

Labda nikwambia ule uvungu hata mtoto wa miaka minne hawezi kutosha sasa wewe sijui unaongelea uvungu gani hebu iweke sawa tukuelewe
 
"Unachotakiwa kufanya ni kuinama haraka sana na kuingia ndani ya uvungu wa siti,na kuhakikisha unakificha kichwa ndani ya siti", ushauri wako ni mzuri ila ni kwa mabasi ya zamani. Mabasi ya siku hizi hayana hiyo nafasi ya kuingia chini ya siti kwani kuna kikanyagio cha kuweka miguu na pi siti ziko chini sana kiasi hata begi hauwezi kuliingiza. Ushauri wangu ni funga mkanda wakati wote pia usinyooshe miguu chini ya siti iliyo mbele yako ili isivunjike pia usiweke mikono dirishani na inamisha kichwa kuelekea katikati ya basi na usithubutu kuinuka kutoka kwenye kiti ili uruke kama askari wa mwamvuli, wakati wote huo kaa kimya mtangulize Mungu wako; tutakutana aliko jiwe.
 
Nakupongeza sana umejitahidi kuongea jambo zuri sana.

Lakini bahati mbaya ajali nyingi zaidi 95% ni sudden occasion ambapo huwez pata huo muda wa kurespond kwaajili ya kujikinga.
Usafiripo anza na kufikiria jinsi ya kujiokoa endapo ajali itatokea, hii inahusu moto au kupinduka. Uwapo ndani ya basi usipende kulala labda tu kama kondakta amekupa shuka, mto na mswaki, pia usikubali kukalia kigoda utakachopewa na kondakta, mwambie ampe dereva wake nawe akuletee kiti cha dereva. Kelele huleta vurumai ndani ya chombo na kuchochea kujeruhiana mkigombea dirisha.
 
Asante kwa elimu... ila mimi kwakweli kwenye basi ni usingizi mwanzo mwisho tena huwa usiku kabla ya safari najinyima usingizi ili nikaulipe nikiwa kwenye basi. Haya mambo ya usafiri kufa, kuumia au kutoka salama ni bahati tu. Ninewahi pata ajari automatically bila jitihada zozote za kujinusuru nilitoka salama kabisa ila kiatu changu kilichanika na chuma au kitu chenye ncha kali na akikufikia ngozi yangu.
Nilikuwa na simu tu sikuwa na begi simu ilipotea lakin chaajabu niliikujakuipata hospital kwa moja ya majeruhi yeye alidhani ni yake ambayo ilifanana na yangu.
 
Katika yote tumtegemee Mungu tu.
 
Hii post itafanya kazi tu pale unapojua kiwa nni kitakwenda kutokea maana kuna wajuba huwa wana oteshwa kitakacho kwenda kutokea tofauti na hapo ajali haiepukiki cha msingi ni kuchukua tahadhari kwa kufunga mkanda

Mostly ukiwa ndani ya gari nivigumu kujua nni kinakwenda kutokea maana huwa ni kitendo cha gafla fumba na kufumbua umesha oga vumbi , umesha buruzwa, kama ni kumia kwa haraka haraka utahisi ganzi full kupigwa bumbuazi huelewi chochote ,... mmi na sisitiza ivi katika kila jambo tumtangulize MUNGU 🙏
 
Njoon chukuen uzoefu kwa mm ambae nimenusurika ajari 12 za mabasi 2 malor 2 pikipk 4 baiskel 2 hapa kwenye baisker nilikuwa spid mteremkon brek zika kata mbele kona ile nakunja kona roli hy hapa.... sasa mniulize nn kilifanyika baada ya kuingia vunguni mwa roli
 
Kama hujafunga mkanda kumbatia kiti mwanawane nasema tena kumbatia kiti kwa mikono yote usiachie kama unavokumbatia baby wako utakuja kunishukuru baadae. Wazee wakukesha safarini tunalijua hilo na limewaokoa wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…