Iko hivi. Baada ya bro kumaliza chuo, akawa amerudi kitaa kuendelea na deal zake,, kama unavyojua vibez za akina bimkubwa Waka mfosi bro aoe, by the way bro at that time alikua Hana mpango huo wa Kuoa alifanya kumridhisha bimkubwa.. Aisee bna bro akaona isiwe kes akaoa (hapo ndipo shida ilipo anzia)
Bna bna baada ya kuoa yule mke, kesi zikawa haziishi kila siku ugomvi kuja ku solve pale hom.. Ukitrace back ugomvi wao vitu vya kijinga
Ikafika mahala bro akawa hapikiwi chakula kisa kaacha hela ndogo akati humo ndani kwao kuna vyakula vyote na kila kitu.. Yaan hela ya ku nunua mboga 5000 et ndogo!! (usawa wa magufuli Enzi hizo si mlikua mnaujua wazee😇)
Mamaqee bna bna bro akaanza kusanda haeleweki , alikua ana ndinga akapiga bei, sometimes akija home anaongea maneno hayaekeweki , kiujumla akawa nusu kichaa hopeless😢..mother ni mtu wa dini (mwaposa akasome 😂😂 jokes tu wapakwa mafuta mnisamehee🙏🙏) , so akawa ameingia kwenye Maombi ndio automatically yule mwanamke akawa anasema mambo mengi, kuna siku bro anasimulia anasema wamekaa ndani , yule mwanamke akawa anamuogesha mtoto miez7 maji ya baridii (barid la mbeya mnalijua) so ile bro KWENDA kumgombeza yule mwanamke, ghafla yule mwanamke akapatwa hasira, sura ikabadilika na nguvu za ajabu mithili ya bondia , akamnyanyua bro, yaan akamkunja shati na kumbamiza ukutani then akatamka maneno '' nyie na Familia yenu hamnijua vizuri mim ni nan!!''
To cut off story matukio mengi nimeruka hapo. Yule mwanamke ni mchawii since alimtamkia bro kwa maneno yake mwenyewe, ku trace back ile Familia, kumbe baba yao alimkimbia mama wa huyo mwanamke kwa ishu za kichawii na by the way alimpigia simu bro akamwambia '' huyo mke wako ni mwanangu wa kumzaa ko kama unataka kufa we endelea kua naye''
Ili kua ngumu Sana kuvunja Ndoa ile maana yule mwanamke alikua mchawii haswaa mpaka na andika hivi now bro wangu bado hajarudi katika default settings mda wote analia akimkumbuka huyo mwanamke. Dunia Ina mengi sana nlikuaga siamini UCHAWI Lakin n kwa sasa huwez ukanishauri kitu kuhusu uchawii.. Uchawi upo!!!