Fanya yote ila usimzalie mtoto huyo mwanaume!

Unawezaje kufikiri nwanaume atakufa kabla yako, kuachana "mawazo ya wakata tamaa
Kwamba wewe hautakufa au unataka kusemaje?
Ni nini mnakifuata kwenye ndoa/mahusiano ni pesa,njaa zinawapeleka huko ama tamaa?
Mimi huwa nafuata mapenzi, furaha na raha. Sijui wengine πŸ€·β€β™€οΈ
 
Ndio ugundue akili za huyu mtu zilivyo fupi. Ni ma emotions tu kayaweka hapa
 
Kwanini wanawake wanafikiri wanatuzalia watoto? Mtoto akizaliwa sio wa baba pakee, ni wa wote. Kwani kwenye maisha ndoa ni ya lazima? Cha muhimu mwanamme atoe matumizi ya mtoto na mama
Nakubaliana na wewe cha muhimu mwanaume ahudumie mtoto.
Ila pia ni vizuri kufahamu familia ya mtu unayezaa naye siyo kukutana vichochoroni tu bila kufahamiana vizuri.
 
Ukitaka kuzaa Anza kujipanga kiuchumi hata kama huyo mwanaume atageuza shingo yake wewe utakua umesimama vizur
Tatizo wanawake akili zetu ni za kuambiwa Kuna kale kausemi et nikimzalia atanioa au nikimzalia atakua ananipa hela aloooh zaa huyo mtoto utalia kilio zaid ya huyo mtoto
 
Kwani aliye kwambia akikuowa hawezi kukuacha na kukutelekeza na watoto wako ni nani ? Mimi nimeona ndowa zilizo dumi miaka mitatu na watoto watatu na mme akasepa. Mke akabaki analea. Ushauri mzuri ni kuwambia wanawake wajuwe suala la kulea watoto ni jukumu la wazazi wawili . Wahakikishe kabla ya kuolewa wanajenga uwezo wao wa kiuchumi kwanza. Ili waingie kwenye mahusiano kama equal partners. Hakuna wmanaume anaweza kumwacha mwanamke anaye saidia kuongeza kipato cha familia. Ukiona mwanaume anacha familia ujuwe amepinga mahesabu akaona kuna faida kuacha kuliko kuendela na majukumu.
 
Hivi,kuna mwanamke huwa anasaidia kulea mtoto (tukiacha kumnyonyesha)
Mwanamke hasaidii analea, tukiachana na kutoa hela, nyie wanaume mnafanya nini kwenye malezi.?
zaidi ya kulazimisha mwanaume awajibike kwa kila kitu?
Kwenye kuwajibika kiuchumi, mfano: ukiamriwa na ustawi ulipe 100,00 ya matumizi ni kweli unaamini malazi, mavazi na chakula kwa mwezi mtoto wako anatumia 100K au kiasi kilichobaki kinatoka kwa mama yake?
 
-Labda neno "KULEA" maana yake ni nini?
-Ni mtoto gani kwenye nchi yetu ambayo wastani kamili wa matumizi ya familia ni nusu dola(US)ieTsh.1300 kuna mtoto mdogo mmoja atumie zaidi ya familia yote?
 
Kwanza pole na changamoto za mahusiano.

Pili, wanawake si malaika, wapo wengi wa hovyo na wanaofanya mambo ya ajabu ambayo hayakubaliki na hatuwezi kuyatetea.
Huu uzi si wa generalization, bali ushauri kwa mabinti wadogo kutozaa hovyo hovyo.
Story ya mshikaji hapa namsikiliza!
Mwambie mshikaji, hata kama anavunga ujumbe tumeupata πŸ˜‚
 
Amempa kipochi Cha nini Sasa? Maadamu ametanua miguu mimba itapita hapohapo, washaur wasitoe kipochi Hadi waolewe na Wala sio mwanaume kuja nyumbani kuchumbia, Bali waolewe kabisa hapo watakuwa wamefanikiwa vinginevyo hamna kitu pia maisha yanawasumbua wengi anaona labda akimzalia mambo yatanoga zaid, kuweni na kampeni hii, Hakuna ndoa hakuna tendo la Ndoa, Kataa Zinaa. Imeisha hiyo.
 
Usizae mtoto kama huwezi kumhudumia mwenyewe.
Ndoa sio guarantee ya kuhudumiwa hakikisha unafanya kazi sana.
Ndoa inaweza kukupa guarantee ya kusikilizwa kuhusu mtoto japo sio 100%
Asante mamie, sina cha kuongezea, wazingatie πŸ‘†πŸ’―
 
Hii vita ya kijinsia inavyoenezwa ni kama kuna mfumo unaandaliwa, au maisha mapya yanaandaliwa. Sioni hata ni kwanini kuna hiyo vita. Ukishajua kwanini ulizaliwa uwe mwanamke au mwanaume, hutashabikia hii vita inavyopiganwa mitandaoni.
Kumbe kuna vita ya kijinsia na wengine hata hatujui, aiseeh πŸ€¦β€β™€οΈ!
 
Nyie wadada msikilizeni mwenzenu ana watoto 5 hapo alipo na ana.mimba changa.

Wewe kaa hapo usizae uje uzae uzeeni...

Mimi nawambia MA BINTI zaeni ila zaa ukijua nazaa kwa ajili yangu binafsi, nazaa kwasababu namuhitaji mtoto, nazaa kwasababu ni muda wangu umefika.

Huzai kwa ajili ya mwanaume
Humzaliii mwanaume
Huzaliii ndugu zake au ukoo wake

Kama ulivyopambana ukatafuta hela ukafungua biashara Yako, ukalipa kodi kwako,ukanunua vitu vya ndani,nk

Fahamu Ujauzito ni Jukumu kama hayo mengine na NI JUKUMU LAKO.

Jipange zako BINTI YANGU weka hela yako Binti angu, kisha Ukiona una ki Balance chako cha kukutunza kwa kipindi ulichojipangia.

BEBA MIMBA Yako, Mwanaume akikutunza hiyo ni BONUS ila usije zaaa kisa UMEAMBIWA kisa Mwanaume Kataka, Kisa unampenda unatamani umkamate kwa kumzalia.

Zaa Tu ikiwa ushajua MTOTO ni kitu unakihitaji.

Msimsikilize sana huyu mdada mtoa MADA mtazeeka Bila watoto na Sio SIFA una KIZAZI zaa ila TAMBUA kuzaaa/kulea ni JUKUMU LAKO.

Kadhalika na Wanaume hii iende vice versa pia.
 
Sina Watoto 5 ila ushauri wako ni mzuri sana πŸ’―πŸ“Œ, wazae kwa ajili yao na wawe na uwezo wa kuhudumia watoto wao bila kutegemea wanaume, maana wengi hawaeleweki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…