Madereva wengi wa kitanzania wanaamini kuwa pombe haiathiri uendeshaji wake. Wengine wanadai kuwa wakinywa ndio wanakuwa makini zaidi. Lakini sheria inazuia madereva wote kuendesha magari wakiwa wamekunywa kiasi fulani cha pombe hata wale wanaosema kuwa pombe inawafanya madereva bora zaidi. Kinachozuiwa hapa ni uwezekano wa dereva aliye kunywa kusababisha ajali ambayo itaathiri uhai wa watu wengine hata kama yeye atatoka mzima. Ingekuwa ukinywa pombe na kuendesha gari utaathirika peke yako, pengine serikali zingeona hamna haja ya kuingilia uhuru wako wa kunywa pombe.
Chanjo ni hivyo hivyo. Unaweza ukawa hauamini kuwa kuna corona au/na hauogopi kufa kwa corona kitu ambacho ni haki yako. Shida ni uwezekano wa wewe kuwaambukiza wengine na kuwasababisha ama wapoteze maisha yao au waathirike kwa namna nyingine( kiuchumi, kiafya n.k.) baada ya wewe kuwaambukiza. Na mbaya zaidi ni kuwa wengi wao hautawajua. Ndio maana ili kuwaokoa hao utakaowaambukiza, chanjo ni muhimu kuwa ya lazima. Tusipofanya hivyo hatutafikia herd immunity ambapo wote tutakuwa salama.
Amandla...
Unapolinganisha vitu, jaribu kutafuta vitu vinavyofanana.
Unalinganisha katazo la kutoingiza kitu mwilini (kunywa pombe) na katazo la uhuru wa kukataa kuingiza kitu mwilini (chanjo).
Hiyo hoja ya kuwaambukiza wengine haina mashiko, kwa sababu tushaona mfano wa Marekani zaidi ya 97% ya wagonjwa wanaopelekwa hospitali ni wale wasiochanjwa, na zaidi ya 99% ya wanaokufa kwa Covid ni wale wasiochanjwa.
Kwa hivyo, wanaotaka kuchanjwa wachanjwe, chanjo itawalinda, hawatapata symptomatic infections, na uwezekano wa kufa kwa Covid ni less than 1%, which is statistically negligible and within a margin of error.
Wasiotaka kuchanjwa, waachiwe uhuru wao, wasichanjwe, wana 97% or more ratio katika wanaopelekwa hospitali. Hawa na zaidi ya 99% ratio ya wanaokufa kwa Covid.
Kwa hiyo hapo utaona kwamba.
1. Wanaochanjwa chanjo inawalinda, tukiweza kumpa chanjo kila anayetaka chanjo, hakuna a realistic fear ya waliochanjwa kuambukizwa na kuwa symptomatic. Hospitalization comprises less than 3% of this group.Deaths comprises less than 1% of this group.
2. Wasiotaka kuchanjwa waelimishwe. Wakiona umuhimu wa chanjo watabadilika. Wale wabishi kabisa waachwe. Waachiwe uhuru wao. Kwa nini kumlazimisha mtu chanjo. Akifa kataka mwenyewe.Hawa ndio wanawapa Wamarekani kwa mfano zaidi ya 97% ya hospitalization na zaidi ya 99% ya vifo vya Covid.
3.Tatizo kubwa naona kuwa hata chanjo za kutosha hazipo. Wanaotaka chanjo hawapati. Which makes the entire discussion about mandatory vaccination for everybody ridiculous. Yani huna chanjo za kuchanja wanaotaka, unalazimisha wote wachanje. Wakija wote uwachanje utawachanja na nini? Kuna watu wanasubiri wengine waanze kuchanja wakiona wamechanja na wako salama watachanja, sasa kwa nini uanze na habari za kulazimisha chanjo hata kabla hujaelimisha watu na kuwaonesha chanjo hazina madhara?
3. Tatizo kubwa ninaloliona