#COVID19 Fatma Karume: Hakuna chanjo ya lazima. Haki za Binadamu zinataka faragha hususan wa mwili wako

Kwenye kutoa maoni hakuna right or wrong - kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake. Ni kama A kusema kuwa na baiskeli ni bora kuliko kuwa na radio kwa sababu kama una mgonjwa unaweza kumbeba na kumpeleka hospitali na B akasema ni bora kuwa na radio kwa sababu unapata habari ambazo zinaweza kukusaidia hata kujua baiskeli zinauzwa wapi na ni bei gani.

Lakini huwezi pia kumchagulia mtu atoe maoni namna gani - mmoja anaweza kusema chanjo iwe lazima (ni maoni yake) na mwingine akasema iwe hiari (ni maoni yake).
Unajua mbowe huwa hakosei na hua ni msimamo wa chama?
Sasa rukaruka aje akusikie unasema eti ni maoni yake.
 
Narudia, katika hili, Mbowe kakosea sana na sijui nani kamshauri.

Ni vema arekebishe kauli au aifute.

Hizi chanjo bado zina utata mwingi hivyo si busara kuja na hiyo kauli unless kuna ambazo zineshathibitishwa kuwa hazina madhara kwa walio wengi.
Aliropoka!
 
Mbowe yupo sahii sana.

Mapenzi ya Mbowe kwa Watanzania ni makubwa mno, ndio maana wazanzibari wakamfananisha na swahaba wa mtume, Abubakar.

Watanzania wote tupewe chanjo ili kudhibiti maambukizi.

M/Mungu akuweke Abubakar Mbowe.
Mmh! Abubakar utamfananisha na mbowe jiangalie vizur usizungumzie kitu ambacho hukielew
 
Narudia, katika hili, Mbowe kakosea sana na sijui nani kamshauri.

Ni vema arekebishe kauli au aifute.

Hizi chanjo bado zina utata mwingi hivyo si busara kuja na hiyo kauli unless kuna ambazo zineshathibitishwa kuwa hazina madhara kwa walio wengi.
Hajakosea Mkuu. Huo utata unasambazwa na wanaopinga aina yeyote ya chanjo. Hivi mnaamini kweli zingekuwa na madhara yeyote wamarekani, waingereza, watu wa jumuia ya ulaya, waisraeli, waaustralia, wa new zealand n.k wote hao wangeendelea kuchanja watu wao? Hatari ya kuwa na watu wasiochanjwa ni kuwa wanaambukizwa kirahisi sana huu ugonjwa na hivyo wanaweza kuwaambukiza wachache katika wale waliochanjwa. Aidha, kuendelea kuwako na wagonjwa wa huu ugonjwa kuna uuwezesha ku mutate katika umbo ambalo linaweza kuwaambukiza hata waliochanjwa. Marekani wameona hili. Maambukizo sasa yanaenea kwa kasi katika majimbo ambayo viongozi wake walipinga chanjo.

Ni lazima tutambue kuwa hii ni vita, na wewe kukataa kuchanja kunaweka maisha ya watu kibao hatarani. Nchi ikishambuliwa ina haki ya kuwaambia vijana wake kuwa wanatakiwa kwenda kumkabili adui hata kama baadhi hawataki kufanya hivyo. Katika nchi ambayo wengi walienda kunywa maji wasioyajua kwa imani kuwa yatatibu magonjwa yao, au wengine wengi tu wanaamini kuwa ukikanyaga mafuta fulani utapona yanayokusibu, au wale wanaokunywa juice ambazo hazijathibitishwa na yeyote kuwa ni dawa ya corona n.k. inabidi uamuzi mgumu ufanywe na serikali ili kutunusuru wengi wetu. Na chanjo ikiwa ya lazima itaondoa uwezekano wa taasisi kuzigeuza kitega uchumi kwa maana itatolewa bure.

Kwenye hili Mbowe yuko sahihi. Na anaongelea kutokana na experience ya familia yake kuugua na kupoteza watu wake wa karibu. Tusiamini mno hizo campaign za misinformation. Mpaka sasa tumechelewa mno.

Amandla...
 
Mbowe kamwagiwa pesa nyingi tu kuisemea corona vizuri, hata akifa mkewe lazima aoanishe ni corona, ingekuwa mwanae na kakake wamefariki kwa corona tungemuona kajifungia ndani kuonyesha yupo serious na anajali, ila sasa 🤕!.
 
Na MaCCM wanaozunguka nchi nzima wale waliocha ndio zao Mombasa katibu mkuu wake, na wale wa Mwenge kusambaza Corona na UKIMWI..?!

Mbowe yupo sahihi sana , njanjo kama ipo tuchanjwe tu wote ili tudhibiti maambukizi
na maisha yaendelee.
Mwambie Mbowe awachanje nyie bavicha na koo zenu wote ndio iwe kwa lazima lakini siyo kwa watz
 
Kwenye kutoa maoni hakuna right or wrong - kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake. Ni kama A kusema kuwa na baiskeli ni bora kuliko kuwa na radio kwa sababu kama una mgonjwa unaweza kumbeba na kumpeleka hospitali na B akasema ni bora kuwa na radio kwa sababu unapata habari ambazo zinaweza kukusaidia hata kujua baiskeli zinauzwa wapi na ni bei gani.
MBOWE NI KIONGOZI WA CHAMA KIKUBWA SANA CHA UPINZANI. KAULI YAKE HAIWEZI KUFANANISHWA NA MAONI YA KAWAIDA TU YA MTU MWINGINE. KWANZA YEYE HAJATOA MAONI ILA KAMTAKA RAIS AAGIZE KILA MWANANCHI ACHANJWE.
 
INTERESTING. Mbowe katoa maoni yake zimeanzishwa nyuzi kibao zilizoshiba kumshambulia. Wengine kwa point zinazoshawishi; wengine kwa kejeli za kisiasa tu kwani siku hizi hatuna bunge hivyo mpinzani mahiri kama Mbowe akiongea huko mitaani mahasimu wake wanamchangamkia kweli kweli! Inakuwa kama sherehe vile! Fursa adimu ya kumshushia Mbowe mipasho kama yote!

Pamoja na yote ya kisheria na yasiyo ya kisheria, MBOWE ANA HOJA MUHIMU. Ni juu yetu kuijadili kimipasho au kwa mantiki. Mbowe hana uwezo wa kulazimisha chanjo kwa kila mtu. Wala kauli yake haina uzito inaopewa. Muhimu, kauli ile ni kama USHAURI wa maana katika mapambano dhidi ya Covid-19.

Kwa wale wanaofuatilia kwa makini sana maendeleo ya mapambano dhidi ya Covid-19 duniani kuanzia data za maambukizi, kuugua na vifo, utendaji wa chanjo na hatua mbali mbali zinazochukuliwa na matokeo (impact) zake wataelewa. Kwa mfano, juzi UK wameamua kulegeza sana masharti ya kujikinga na Covid-19. Ni impact ya chanjo hiyo ndiyo iliyowapa kujiamini.

Marekani majimbo (States) yanapishana kwa hatua za kulegeza na kubana kutokana na hali halisi ya maambukizi, kuugua na vifo. Impact ya chanjo inavyoathiri data za matukio yote hayo na maamuzi inaonekana dhahiri. Wako wazi sana kwa data. Nafuu inayoletwa na chanjo ni kubwa sana. Haiwezi kupuuzwa. Marekani sasa wanahangaika kuhimiza kampeni ya watu kuchanja ili kuzuia variants zaidi zisiwaathiri kikubwa. Serikali inaomba wanasiasa, viongozi wa dini na makundi mbalimbali yasaidie kampeni hiyo.

Wapinzani wa chanjo (anti-vaxxers) bado ni wengi. Wengine wana sababu zinazoeleweka lakini wengine wamezama kwenye conspiracies za kila namna. Haitusaidii. Lazima tujue ukweli na kuufuata. Mpaka sasa chanjo ndio “tiba” pekee inayoonyesha matumaini ya kupunguza maambukizi na athari (kuugua na vifo) za Covid-19.

Changamoto kubwa tulilo nalo ni kuhakikisha Watanzania wengi WANAKUBALI chanjo na WANAIPATA. Yanayotokea Kanda ya Ziwa na Mkoa wa Kilimanjaro ni dalili ya tishio kubwa linaloendelea kutukabili. Tunakoelekea kuna mashaka mengi.

Kama tunaamini tuna MBADALA WA CHANJO basi ndio uwe mjadala hapa. Wanaopinga chanjo waelezee mbadala wake unaoshawishi badala ya kuhangaika na SEMANTICS za Mbowe.

Yeye Mbowe anaona SULUHISHO ni wote tuchanje. Hiyo ndio point muhimu ya kauli yake. Ni maoni yake binafsi. Ukiisikiliza kwa makini kauli yake jinsi alivyolitumia neno “LAZIMA” ni kama SEMANTIKI tu. Kikubwa anataka serikali ione njia bora ya KUHAKIKISHA chanjo inapatikana kwa watu wote.
 
Kwenye kutoa maoni hakuna right or wrong - kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake. Ni kama A kusema kuwa na baiskeli ni bora kuliko kuwa na radio kwa sababu kama una mgonjwa unaweza kumbeba na kumpeleka hospitali na B akasema ni bora kuwa na radio kwa sababu unapata habari ambazo zinaweza kukusaidia hata kujua baiskeli zinauzwa wapi na ni bei gani.
MBOWE NI KIONGOZI WA CHAMA KIKUBWA SANA CHA UPINZANI. KAULI YAKE HAIWEZI KUFANANISHWA NA MAONI YA KAWAIDA TU YA MTU MWINGINE. KWANZA YEYE HAJATOA MAONI ILA KAMTAKA RAIS AAGIZE KILA MWANANCHI ACHANJWE.
 
Mmh! Abubakar utamfananisha na mbowe jiangalie vizur usizungumzie kitu ambacho hukielew
Unaona sasa ,kuitwa Alfan Issa unataka kujiona mwana wa Mariam na unaujua sana uislmu kuliko wengine. Nimeusoma uislamu na hadith za mtume. Na mfaamu Abubakar toka anakata waislamu vichwa kwa kua alikua hataki kusikia Adhana mpaka alipoucha ukafiri na kuupigania Uislam.
Una lingine?!
 
Narudia, katika hili, Mbowe kakosea sana na sijui nani kamshauri.

Ni vema arekebishe kauli au aifute.

Hizi chanjo bado zina utata mwingi hivyo si busara kuja na hiyo kauli unless kuna ambazo zineshathibitishwa kuwa hazina madhara kwa walio wengi.
Duuuh kweli umeamua kutumia haki yako ya kikatiba vizuri.
 
INTERESTING. Mbowe katoa maoni yake zimeanzishwa nyuzi kibao zilizoshiba kumshambulia. Wengine kwa point zinazoshawishi; wengine kwa kejeli za kisiasa tu kwani siku hizi hatuna bunge hivyo mpinzani mahiri kama Mbowe akiongea huko mitaani mahasimu wake wanamchangamkia kweli kweli! Inakuwa kama sherehe vile! Fursa adimu ya kumshushia Mbowe mipasho kama yote!

Pamoja na yote ya kisheria na yasiyo ya kisheria, MBOWE ANA HOJA MUHIMU. Ni juu yetu kuijadili kimipasho au kwa mantiki. Mbowe hana uwezo wa kulazimisha chanjo kwa kila mtu. Wala kauli yake haina uzito inaopewa. Muhimu, kauli ile ni kama USHAURI wa maana katika mapambano dhidi ya Covid-19.

Kwa wale wanaofuatilia kwa makini sana maendeleo ya mapambano dhidi ya Covid-19 duniani kuanzia data za maambukizi, kuugua na vifo, utendaji wa chanjo na hatua mbali mbali zinazochukuliwa na matokeo (impact) zake wataelewa. Kwa mfano, juzi UK wameamua kulegeza sana masharti ya kujikinga na Covid-19. Ni impact ya chanjo hiyo ndiyo iliyowapa kujiamini.

Marekani majimbo (States) yanapishana kwa hatua za kulegeza na kubana kutokana na hali halisi ya maambukizi, kuugua na vifo. Impact ya chanjo inavyoathiri data za matukio yote hayo na maamuzi inaonekana dhahiri. Wako wazi sana kwa data. Nafuu inayoletwa na chanjo ni kubwa sana. Haiwezi kupuuzwa. Marekani sasa wanahangaika kuhimiza kampeni ya watu kuchanja ili kuzuia variants zaidi zisiwaathiri kikubwa. Serikali inaomba wanasiasa, viongozi wa dini na makundi mbalimbali yasaidie kampeni hiyo.

Wapinzani wa chanjo (anti-vaxxers) bado ni wengi. Wengine wana sababu zinazoeleweka lakini wengine wamezama kwenye conspiracies za kila namna. Haitusaidii. Lazima tujue ukweli na kuufuata. Mpaka sasa chanjo ndio “tiba” pekee inayoonyesha matumaini ya kupunguza maambukizi na athari (kuugua na vifo) za Covid-19.

Changamoto kubwa tulilo nalo ni kuhakikisha Watanzania wengi WANAKUBALI chanjo na WANAIPATA. Yanayotokea Kanda ya Ziwa na Mkoa wa Kilimanjaro ni dalili ya tishio kubwa linaloendelea kutukabili. Tunakoelekea kuna mashaka mengi.

Kama tunaamini tuna MBADALA WA CHANJO basi ndio uwe mjadala hapa. Wanaopinga chanjo waelezee mbadala wake unaoshawishi badala ya kuhangaika na SEMANTICS za Mbowe.

Yeye Mbowe anaona SULUHISHO ni wote tuchanje. Hiyo ndio point muhimu ya kauli yake. Ni maoni yake binafsi. Ukiisikiliza kwa makini kauli yake jinsi alivyolitumia neno “LAZIMA” ni kama SEMANTIKI tu. Kikubwa anataka serikali ione njia bora ya KUHAKIKISHA chanjo inapatikana kwa watu wote.
Kwenye kuchukua tahadhari za kujikinga na corona ili kudhibiti maambukizi tumefeli tumeacha tu maambukizi yanazidi na serikali imesema kabisa kuwa haitotumia nguvu katika hilo, sasa tumeacha hilo la kudhibiti maambukizi tumeenda kukimbilia chanjo na tunataka iwe lazima na nasikia hizo chanjo zenyewe zilizoagizwa ni kiasi kidogo mno.
 
Unajua mbowe huwa hakosei na hua ni msimamo wa chama?
Sasa rukaruka aje akusikie unasema eti ni maoni yake.
Awe hakosei au alichosema uwe msimamo wa chama, kwa umma wa Watanzania bado ni "maoni tu" maana siyo sheria iliyotungwa na bunge au kanuni iliyotungwa na wizara au hata siyo sehemu ya sheria ndogo ndogo zilizotungwa na majiji au serikali za mitaa.
 
MBOWE NI KIONGOZI WA CHAMA KIKUBWA SANA CHA UPINZANI. KAULI YAKE HAIWEZI KUFANANISHWA NA MAONI YA KAWAIDA TU YA MTU MWINGINE. KWANZA YEYE HAJATOA MAONI ILA KAMTAKA RAIS AAGIZE KILA MWANANCHI ACHANJWE.
Sijasema kama yeye siyo kiongozi wa chama kikubwa sana cha upinzani. Kama ulifahamu context ya post yangu, ilikuwa ni kwa mchangiaji aliyekuwa akimkosowa na kusema hakupaswa kusema hivyo. Mimi nikasema alichokisema ni maoni na kwenye kutoa maoni ya nini kifanyike hakuna right or wrong. Pia kwa Tanzania, jambo ambalo linalosemwa, lakini halina nguvu ya kisheria haliwezi ku'bind' na kama ukisema kitu ambacho hakiwezi ku'bind' then siyo lazima kukikubali na ndiyo hoja yangu. In fact, hakusema "chanjo ni lazima" (na asingeweza kusema hivyo) bali alisema "chanjo iwe lazima" (kwa sababu anapendekeza). Kama huwezi kutofautisha maana ya maneno haya siyo kosa langu.
 
Fatma kama msemaji wa serikali vile..
Halafu Mbowe kama jiwe
Dah ..mambo yanabadilika so fast
But under the law, children must be immunized against 10 serious communicable diseases – diphtheria, Haemophilus influenzae Type B (bacterial meningitis), measles, mumps, pertussis (whooping cough), polio, rubella, tetanus, hepatitis B and chicken pox – if they want to attend public or private schools and child care
 
Back
Top Bottom