Ili tuwe open-minded, yatupasa kujadili hoja ya mtu na si mtu husika ama personality yake!
Je, hoja ya chanjo za lazima ni halisi?
Kila mtu ana mapenzi yake katika hili, hilo halipingiki, lakini hilo halitufanyi kupuuza ukweli (facts) uliopo ama unaoweza kuwepo katika hoja hiyo.
Ukweli ni kwamba, zipo sera za kitabibu ambazo zinakubalika duniani kote katika utekelezaji wa chanjo za lazima ama sera nyingine zozote zile zinazohitaji utekelezaji wa lazima katika masuala ya kitabibu.
Ni kweli kwamba, watu wangependa kuamua kupata chanjo au hapana, lakini si kweli kwamba hakuna sera mbadala na za lazima za kitabibu ambazo zinaweza kutumika ili kukabiliana na janga lolote lile la kiafya tena hasa katika ngazi ya kidunia.